Ubatizo wa kweli ni Maji Mengi au Maji Machache?

Ubatizo wa kweli ni Maji Mengi au Maji Machache?

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,853
Reaction score
35,615
Maswali kwangu hua hayaishi nahitaji nipate ufahamu,

Ndugu zangu naomba nipewe elimu juu ya ubatizo wa kweli ni upi? Je, maji mengi au maji machache?
Maana haya mambo lazima tupeane elimu mapema ili watu wafahamu,

Najua waliobatizwa kwa maji mengi wataelezea na waliobatizwa kwa maji machache wataelezea ili nielewe,
 
Ubatizo ni kitendo cha imani tu yanii kuzaliwa mara ya pili kuacha maisha ya zamani na kuishi maisha mapya yaliomo ktk maandiko au maisha ya Yesu aliyoishi au yale aliyotufundisha, mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na lakushoto, mtu akikuibia TV mwachie na king'amuzi vitu kama hivyo mkuu.

NB kubatizwa maji mengi au machache siyo ishu kama hujui nn maana ya ubatizo
 
Maswali kwangu hua hayaishi nahitaji nipate ufahamu,
Ndugu zangu naomba nipewe elimu juu ya ubatizo wa kweli ni upi? Je maji mengi au maji machache?
Maana haya mambo lazima tupeane elimu mapema ili watu wafahamu,
Najua waliobatizwa kwa maji mengi wataelezea na waliobatizwa kwa maji machache wataelezea ili nielewe,
Ukweli ni nini?

Imani ya kila mtu ni ukweli wake anao uamini yeye Binafsi.

Ambao wana imani ya ubatizo wa maji mengi watakwambia ubatizo wa maji mengi ndio wa kweli kulingana na dini, dhehebu au wanacho kiamini wao na jinsi walivyo funzwa.

Ambao wana imani ya ubatizo wa maji machache watakwambia hivyo hivyo kulingana na imani yao kwamba ubatizo wa maji machache ndio wa ukweli..

Hapa kila mtu ata tetea imani yake, dini au dhehebu lake. Hamna ukweli zaidi ya Ubishi usio na mwisho.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Aaminiye na kubatizwa ataokoka. Swali zuri kabisa. Imani lazima iambatane na ubatizo sahihi. Neno ubatizo lenyewe kwenye lugha iliyotumia kuandika Biblia lina maana ya kuchovyo. Au kuzamisha na kuibua tena. Ndio maana unaposoma Biblia, unaona wote walibatizwa ubatizo wa maji mengi. Vifungu vya maandiko. Ukivihitaji vitakuja.
 
Asante kwa swali nzuri na nitajibu katika Jina lipitalo majina yote.

Ubatizo uwe wa maji mengi au machache hauna maana tena siku hizi za Agano Jipya! Kwanini?

Ubatizo maana yake ni kuzamishwa. Yohane Mbatizaji, mtu wa Agano la Kale alibatiza watu kwa maji (aliwazamisha watu kwenye maji) kuashiria toba na utakaso.

Yohane Mbatizaji baadaye akasema: Mimi nawabatiza kwa maji lakini huyo ajaye (Yesu Kristo) atawabatiza (atawazamisha) kwa Roho na Moto.

Hivyo basi ubatizo wa sasa (Agano Jipya) ni ubatizo (uzamisho) katika Roho na Moto na sio tena uzamisho katika maji.

Ndio kusema suala la ubatizo wa maji mengi au machache halina maana yoyote tena kwani siku hizi za Agano Jipya tunabatizwa (tunazanishwa) katika Roho na Moto na Yesu mwenyewe kwa njia ya imani!
 
Ukweli ni nini?

Imani ya kila mtu ni ukweli wake anao uamini yeye Binafsi.

Ambao wana imani ya ubatizo wa maji mengi watakwambia ubatizo wa maji mengi ndio wa kweli kulingana na dini, dhehebu au wanacho kiamini wao na jinsi walivyo funzwa.

Ambao wana imani ya ubatizo wa maji machache watakwambia hivyo hivyo kulingana na imani yao kwamba ubatizo wa maji machache ndio wa ukweli..

Hapa kila mtu ata tetea imani yake, dini au dhehebu lake. Hamna ukweli zaidi ya Ubishi usio na mwisho.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Yesu alibatizwa ubatizo upi?
 
Ubatizo wa kweli ameondoka nao magufuli.....
Alibatiza waumini wake kwa moto.
wache weeeeee hiyo mambo chungulia hapo chini [emoji116]
1.jpg
 
Ubatizo sahihi ni wa maji mengi, nje ya hapo hutapita langoni pa paradiso
 
Ubatizo sahihi ni wa maji mengi, nje ya hapo hutapita langoni pa paradiso
Ubatizo wa maji ni ishara ya nje ya mkristo kuonesha kwamba ameungana na kifo(kuzama) na kufufuka( kuibuka kutoka kwenye maji)
Hivyo Ubatizo ni zaidi ya kile watu wanavyofikiri...ubatizo Upo kiroho zaidi, as long as Umefanya usharika na Kifo na kufufuka na Yesu hapo unakuwa umebatizwa.
 
Back
Top Bottom