msumeno
JF-Expert Member
- Aug 3, 2009
- 2,826
- 1,730
Waungwana utaratibu wa Kupata Visa katika Ubalozi wa India safi sana kwa kweli wanastahili pongezi, kifupi hakuna longo longo. Nimengia kwenye website yao , nikajaza form nika print na kuweka picha ya ziada pamwe na viabatanisho anuai. Nilipofika langoni nikachukua namba, na wako fasta kweli kweli nilikua namba 8 lakini nilikaa pale kama dakika 15 tu nikaitwa.....Mhusika akafunua documents zangu na kwa sababu mimi sio Raia hapa ni resident tu akaipeleka document yangu kwa mkuu wake huko nikahojiwa in friendly way..... na baada ya kijiridhisha nikaambiwa nikalipia ... kifupi nilitumia saa 1 tu kukamilisha taratibu zote..... nasema bravo hawa jamaa maana hulipi kabla hawajaridhika na wewe tofauti na balozi zingine unaweza lipia hata mara tatu kila mara watakuja na kosa hili na lile .... lakini hawa jamaa kama hawajaridhika na wewe hawachukui pesa yako ..... Asante India