Ubakaji nyakati za wilayani Bunda

Ubakaji nyakati za wilayani Bunda

MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
777
Reaction score
912
Jamani,
Kwa masikitiko makubwa naleta uzi huu kwenu ili tusaidiane kutokomeza tatizo sugu na hatari linaloendelea Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara. Utangulizi: Mwaka jana (2015) wakati tukikaribia kwenye uchaguzi mkuu kulitokea tatizo la ajabu kwa familia kadhaa kuvamiwa usiku wa manane na wanawake katika familia hizo kubakwa kwa zamu wakati wanaume/waume zao wakiwa wamefungwa mikono na miguu/kutishiwa kwa silaha kama vile bunduki, mapanga, nk au wawapo safarini. Ninachokumbuka ni kuwa vyombo vya Ulinzi na Usalama wilayani hapo vilitoa taarifa kuwa hali hiyo ilisababishwa na uhasimu wa kisiasa kati ya CHADEMA na CCM wakati huo Wassira akiwa anapambana vikali na Esther Bulaya.
Moja ya matukio ninayokumbuka mpaka sasa ni pale Daktari maarufu wilayani hapo (jina limesitiriwa) alipovamiwa, kuwekwa chini ya ulinzi na kulazimishwa kushuhudia Mkewe na Mtoto wake wa Kike aliyekuwa likizo ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (jina kapuni) wakiwa wanabakwa kwa zamu ambapo kila aliposikia sauti ya Mtoto/Mke ikilalamika kwa maumivu alikuwa anainuka na kukutana na panga la kichwa kiasi kwamba hadi wabakaji wanafanikisha mpango wao yeye aliachwa akiwa mahututi kwa majeraha ya mapanga ya kichwani. Hivi ninavyoandika hapa mkewe ambaye pia ni Nesi kwenye moja ya hospitali kuu wilayani hapo anatembea kwa kuchechemea kwa maana kwamba alipata kilema cha kudumu kwenye ubakaji huo.
Mfano mwingine ni Mpiga Kinanda maarufu wa Kanisa Katoliki wilayani hapo(jina kapuni) ambaye alivamiwa, kuwekwa chini ya ulinzi na matokeo yake akashuhudia mkewe ambaye alikuwa na mtoto mchanga, dadaake aliyemtembelea toka Kigoma na binti wa Kazi wakibakwa huku akiwa hana la kufanya zaidi ya kubaki kuumia moyoni bila kuwa na uwezo wa kutoa msaada wowote. Kwa sasa ameihamisha familia yake toka Wilayani Bunda. Mifano ipo mingi!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bado balaa hili linaendelea wilayani humo pamoja na kuwa si jambo geni na pia kuna vyombo vya ulinzi na usalama kama zilivyo wilaya zingine.

Maswali ninayojiuliza na ningependa kila mmoja wetu kwenye jamvi hili kujiuliza au kuongeza mengine ni pamoja na:
  1. Ni kwa nini tatizo hili litokee wilayani Bunda pekee kati ya wilaya zote za Mkoa wa Mara na mikoa mingine ya Tanzania?
  2. Je, Wilayani Bunda hakuna hivi vyombo vya Ulinzi na Usalama kama maeneo mengine? kama vipo,
  3. Ni kwa nini vyombo hivi vishindwe kupambana na tatizo hili linaloumiza jamii kimwili na kisaikolojia? Na kama vyombo hivi vimeshindwa ni kwa nini visitoe taarifa sahihi kwa jamii na kuomba msaada ikiwa ni pamoja na kutangaza kuwa hili tayari ni janga wilayani humo?
  4. Je, ni watu wangapi (hasa wanawake) ambao wameshapata maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana hasa VVU ikiwa ni pamoja na kutoswa na waume zao au kuambiwa wasubiri vipimo ili waume zao wajiridhishe na afya zao kabla ya kuendelea kushirikiana nao katika tendo la ndoa? Hawa wanajisikiaje katika nchi hii ya AMANI?
  5. Je, viongozi katika ngazi ya Taifa hawafahamu tatizo hili lililopo Wilayani Bunda kwa muda mrefu sasa? Kama ndio, mbona wako kimya?
  6. ..............................................
Ni vyema sasa serikali kupitia vyombo vyake ifuatilie suala hili kwa undani wake ili kulitatua na sio kubaki kujinasibu kuwa ipo maakini katika kuilinda jamii inayoiongoza wakati kuna mambo ya ajabu na ya kutisha yanayotokea katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi hii bila kuwa ATTENDED na hivyo kusababisha madhara makubwa sana ndani ya jamii husika.
 
Sisi wa dar mliposikia tuna kabwa na panya road mlikuwa mnaongea sana.haya na ninyi pambaneni tuwaonee.
 
Duh....
Poleni sana wakazi wa Bunda kama kweli haya yanatokea basi ni hatari sana. Pamoja na kuiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kushughulikia suala hili, lakini pia wananchi wenyewe kupitia viongozi wa ngazi za chini wekeni utaratibu wa namna ya kukabiliana na suala hili maana yawezekana pamoja na dahana ya kuwa na msukumo wa hali ya kisiasa lakini pia inawezekana kukawa na maswala ya visasi na ujambazi.
 
So sad inasikitisha sana asikwambie mtu yaani polisi Jamii ndio wenye msaada kwenye baadhi ya maeneo japo kuna wahuni lakini afadhali co kama wale wengine
 
Kaeni kama kamati ya ulinzi hakuna muhalifu atokae mbali pigeni kura za siri kisha chukueni hatua hao wahalifu mnaishi nao.
 
Itisheni kura za siri kila myakabidhi Kwa mamlaka husika wasipoyafanyia Kazi muyapeleke ngazi za juu watayafanyia kazi
 
Kaeni kama kamati ya ulinzi hakuna muhalifu atokae mbali pigeni kura za siri kisha chukueni hatua hao wahalifu mnaishi nao.
Ahsante ila hili linahitaji usimamizi/uratibu. Ipo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambayo m'kiti wake ni DC, shida ya viongozi wetu wa sasa wana vipaumbele tofauti na vile vya jamii!
 
Mods, hiyo title ilikuwa inasomeka ".....nyakati za usiku...." Mbona neno usiku limetoweka halafu sioni option ya ku-edit title?
 
Back
Top Bottom