Naandika hili kwa huzuni na si kwa nia ya kuamsha hamasa ya kimapenzi. Ninaomba nisimulie visa vya mabinti wawili hawa;
Binti wa leo nimezoeana naye kwa muda mrefu saana. Nilikuwa ninasoma makala ya Ukeketaji na nikaelezea msimamo wangu juu ya hilo. Binti huyu akaanza kusimulia tukio lake. Akaanza kwa kusema yeye amekeketwa.
Aligundua kuwa amekeketwa baada ya kwenda kuoga na wenzake mtoni na kugundua maumbile yake ni tofauti na wenzake wakati wanachunguliana na wote wakiwa watoto. Alirudi nyumbani akamuuliza mama yake hali ile na mama yake alimueleza alivyozaliwa tu hata kabla kitovu hakijakatika akatahiriwa na bibi yake na wale wengine hawajatahiriwa. Aliona furaha saana.
Kadri alivyoendelea kusoma aligundua kitendo alichofanyiwa ni cha ukatili na kila siku anajuta. Anasema wazazi walifanya hivyo ili mtoto akikuwa asitoke nje ya ndoa na hana hakika kama hali hiyo inasaidia yoyote. Kwahiyo lengo ni kutunza heshima ya mtoto wao akiolewa. Kwa vyovyote vile ni kumfurahisha mwanaume na kuacha kovu kubwa na lenye kuumiza ndani ya nyoto za watu hawa.
Lazima tukubali, sisi si watu wakufurahishwa kwa mateso ya wengine. Ni zamu yetu kusema hapana na kwakuwa kwa jamii yetu tunaweza kushawashi tuwasaidie wale ambao huenda wakajuta mbeleni. Tusikubali. Poleni kwa wale yaliyowasibu haya.Huyu mwingine yeye alibakwa na mtoto wa mama yake mdogo. Yeye alikuwa anafanya kazi za ndani hapa nyumbani. Wale mabosi wake muda wa kuwepo nchini ulivyoisha walimuachia pesa ili ajiendeleze kimasomo. Binti akaamua kuishi na mama yake mdogo hapa Dar.
Kijana wa yule mama akawa analeta usumbufu na kuna siku yule mama akasafiri. Kijana akazama ndani akambaka kama mara tatu. Wakati huo binti ana miaka 17. Binti hakukubali kesho yake akaenda kwa jirani na taarifa zikaenda polisi. Binti kupima anamimba na pia tafrani ikaanza. Kama kawaida wanaume au jamii yetu tunatabia ya kulaumu wanawake. Akalaumiwa binti ni malaya na amejitongozesha.
Familia zikasambaratika mpaka kesho. Kule polisi, mlungula ukapita na jamaa akaachiwa. Binti akatoa ule ujauzito. Binti yule anasema kila mara huweweseka juu ya usiku ule jamaa alipombaka lakini huwa hasahau vile vyuma alivyoingiziwa wakati wa abortion. Ni miaka 7 imepita lakini haamini mwanaume hata mmoja na anaogopa. Kila asubuhi akiamka anawaza siku ile.
Nimeandika hili kuna wale ambao hupenda kutake advantage kwa wasichana wa kazi ambao hufanya mapenzi kwa kuwa wewe ni bosi wao na hawana uwezo wa kuamua. Pia kwa wale wanaowachukua watoto wa shule au wale waliopo chini yao makazini. Tuwasaidie watu wenye matatizo haya na tuungane kutengeneza jamii itakayoheshimiana.