Jakomhabari
Member
- Jul 29, 2015
- 26
- 15
Uamuzi wa aina ya shule mzazi angependa kumpeleka mtoto wake, inatokana na sababu nyingi. Mimi kama mzazi, kwa uelewa wangu, niliamua kumpeleka mwanangu katika shule ya kimataifa ili apate elimu kwa ajili ya uelewa wa mambo mbalimbali ya kimataifa (education for international understanding).
Pamoja na hilo, napenda mwanagu aweze kujijengea uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na mtu yeyote kutoka popote pale duniani, pasipokujiona mnyonge mbele ya mgeni yeyote (appreciate working in harmony with anybody without feeling inferior before foreigners).
Ila kwa sasa niko njia panda!. Najiuliza kama nitaweza kutimiza malengo yangu. Nimekutana na kikwazo katika mashule yetu yanayojiita “Ya Kimataifa”. Kikwazo ni UBAGUZI WA RANGI.
Kunashule kongwe zaidi hapa nchini ya kimataifa, ambayo mimi nimempeleka mwanangu baada ya kuona watoto wa marafiki zangu na baadhi ya ndugu wamesoma na kuhitimu katika shule hiyo, baadaye wakawa wanapata nafasi ya kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa.
Hata hivyo, hivi karibuni, kumetokea tabia chafu shuleni hapo ya baadhi ya wafanyakazi kuanza kupandikiza mbegu ya dhambi ya ubaguzi wa rangi (Racial discrimination). Kumekuwepo na tabia ya kuwaita wanafunzi kwa majina kama, "Negros, Mchina, Wazungu, Browns, Weusi, Waafrika, Wamarekani, Wahindi, na majina mengi kama hayo”.
Hii hali haijamkuta mwanangu, lakini ni jambo linalozungumzwa hapo shuleni, wanafunzi wanalalamika. Nimeambiwa kuwa uongozi wa shule imepewa taarifa, lakini wao hawajachukuwa hatua yoyote kwa sababu wanalinda jina au sifa ya shule yao.
Tabia hii mimi naona itakuwa ni kikwazo kikuu cha kuwafanya watoto wetu wasiweze kufikia malengo ya kupata elimu ya kimataifa. Wakipandikiziwa mbegu ya ubaguzi, wataendelea kubaguana hata baada ya kupata kazi zao na pia hawa watoto wetu weusi, watajiona wao ni wanyonge na wageni ni bora zaidi yao. Hii ni vita ambayo ni lazima tupambane ili tuwajengee wanetu uwezo wa kutowaogopa wageni kwa kigezo cha rangi yao.
Ushauri kwa wanaJamii Forum inakaribishwa.