kirengased
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 6,818
- 7,493
Na wakiteuliwa bado wanabaki kuwa Wapinzani?Izo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Tumia akili kidogo, utakua vipi ndani ya serikali ya Chama A ukatekeleza sera za Chama B. Kinachotakiwa ni mchango wako katika maendeleo ya Taifa bila kujali Chama ulichokua kwakua vyama vinapita Ila Taifa lipo tu.Na wakiteuliwa bado wanabaki kuwa Wapinzani?
Usiseme za kisiasa. Angalia anaezitoa ni nani. Rais wa nchi. Halafu baadae anakuja kusema maendeleo hayana vyama.Izo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Magufuli ni mkabila mkubwa na ni hatari kwa mshikamano wetu.Hizo ni kauli za ki siasa kwani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si alikua Mpinzani. Mbona Kuna mbaka manaibu waziri na nafasi nyingine mbalimbali serikalini wakitokea upinzani?
Watu wataelewana tu huku mtaani kwa hizi chuki zinazoendelea kujengwa na waheshimiwa.Salaam,
Wandugu, binafsi nimesikitishwa sana kwa kauli za kibaguzi zilizotolewa na mgombea mmoja wakati akimnadi Diwani wa chama chake asiyekubaliwa na wananchi.
Kwa kauli yake mgombea huyo wa Rais alitisha wananchi kwa kuwaambia wasipompa Diwani huyo ushindi wasimuulize yeye kuhusu maendeleo.
Isivyoeleweka Mgombea Urais huyo amekuwa akisema maendeleo hayana chama lakini anatoa mfano wa jinsi walivyoistopisha barabara ya lami kusudi isiingie eneo linaloongozwa na Wapinzani.
Unaposema hadharani huwezi kufanya kazi na Wapinzani maana yake una ubaguzi wa kiitikadi.
Pamoja na maendeleo tunayotafuta lazima tujue umoja wetu, haki na kuheshimiana ndiyo nguzo kuu za amani na utangamano.
Ni aibu kwa kiongozi mkubwa kutoa kauli za kivitisho ili kulazimisha yeye ama chama chake kuchaguliwa!
Ni muhimu tukakemea vitendo hivi visivyotuunganisha na kuuinua utaifa wetu na uzalendo Wetu.
La ukabila sasa linatetewa kwa nguvu zote... ukizikumbuka kauli "rais hawezi kutoka kaskazini... huyu sio mwenzotu na sasa kabila kubwa haliwezi tawaliwa na makabila madogo!!"Magu ni mkabila mkubwa na ni hatari kwa mshikamano wetu.