Ubaguzi katika hoteli za kitalii Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubaguzi katika hoteli za kitalii Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, Jun 1, 2012.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Ni mara nyingi nimekuwa nikiona au kusoma jinsi wawekezaji wanavyopewa nafasi zaidi na serikali kiasi cha kufikia hata kuwanyanyasa wananchi. Serikali imekuwa ikifumbia macho malalamiko ya wananchi na wananchi kuendelea kunyanyasika, kuumizwa na mara nyingine kupoteza maisha yao. Jambo hili limewafanya wananchi kutokuwa na imani na serikali kwamba iko upande wao. Cha kushangaza, wakiona wananchi wanaichukia serikali au kuhamia katika vyama vya upinzani, serikali inashangaa na kutoa maneno mengi bila kuelewa kuwa chanzo cha serikali kuchukiwa ni wao wenyewe.

  Mfano mmoja ni hii habari niliyoikuta Michuzi Blog kuhusu ubaguzi Zanzibar. Haiyamkini mwekezaji anaendelea kula na viongozi huku wananchi hawaruhusiwi hata kukanyaga hapo.

  MICHUZI: YALE YALEEEE.......
   
Loading...