Ubadhirifu Ofisi ya CAG

Hii kali. Yaani CAG nae mpigaji? Nahisi anapakwa matope au kuna mtu anatafutiwa kazi. Nitasubiri muda ufungue mengi...

Jamani eee! Binafsi naomba kufahamu ni kwa nini kila CAG anapoombwa ufafanuzi yeye anatoa kauli za vitisho? Tukumbuke wakati ule alipoandikwa kwa safari ya Kenya. Huyu ni Profesa. Huyu anastahili kuwa muelewa kwamba waandishi wananmpa nafasi ya kutoa taarifa ambayo ni balanced, lakini anaipoteza kwa kuamini yeye ni mtu mkubwa.

Nina wasi wasi kwamba mtu huyu uwezo wake kwa nafasi hiyo ni mdogo! Sina sababu ya mumtetea na hasa kwa kuelewa ni kizazi cha rais aliyepita. Aliyeamua kucheka na nyani.
 
wasiishie hapo kwa Prof. Asad, waende mbele zaidi kumuandika pia Dr. Dau!
 
Mhhhhh angekuwa mtu mwingine katajwa humu watu wangeamimi hizo tuhuma ziwe za kweli au uongo. Najiuliza kwa nini wadau wengi wanamkingia kifua jamaa. Something fishy😡
The guy is smart, kuanzia kote alikopita. waulize waliopita b.com pale mlimani watakuelezea uadilifu wa huyo jamaa.
 
huyu CAG yuko kidili zaidi. binafsi simkubali kamwe....
kwa kifupi credibility ya huyo jamaa inafahamika na kama ni uadilifu wake hauna mashaka. waliosoma B.Com pale USM know the person well, na sidhani kama aliwahi kumpendelea mtu kwa sababu ya yoyote ile. hebu tueleze hizo dili zake na sisi wengine tuzijue.
 
Hii kitu inajulikana ni ya kupikwa kwasababu ya chuki binafsi za watu baada ya mirija kuzibwa na prof
 
Hii ni vita ya wazi juu ya Prof.Assad!kuna sura hazitakiwi serikalini kwa njama za kuunga unga


Alisha pigwa bun sk nyingi watu wamekaa kimajungu haya ndio mabadiriko tuliyoyataka watz siyo watu kujifanya miungu watu kwenye ofis za umma
 
Ili kuondoa utata wa amefanya hajafanya basi achunguzwe. Kama anasingiziwa itaonekana, lakini kama ni kweli basi sheria ifuate mkondo wake. Kwa sasa hivi siwezi kumtetea au kumkingia mtu kifua hata kidogo.
 
Kweli Assad anaweza akawa amefanya makosa na sheria ichukue mkondo wake!
Vipi kuhusu muandishi na mtumishi wa umma wakifanya conspiracy na kutoa unataka za serikali? Huyu mtumishi anajua kuwa vipo vyombo halali kama PCCB au polisi ambao angeweza kuwapa hizo nyaraka kama vielelezo kwa kuwa zote ni taasisi za umma zinazozungatia maadili!
Kama CAG anakagua hadi ikulu na TISS kweli kutakuwa na usalama kwa taarifa za nchi ikiwa kuna mtumishi ambaye kuwepo tu ktk mahojiano na waandishi akaamua kupeleka taarifa za siri za ofisi!
Polisi na taasisi nyingine za usalama zinapaswa kudeal na muandishi ili a cooperate tumpate huyo mtumishi asiye na maadili!
Raisi na jopo lake wadeal na Assad, ingawa sina hakika kama ana power ya kumtengua!
 
Huyo mtaalam wa chuo cha ardhi ni mtaalam wa nini? Hii stori imekaa kimajungu tu mwandishi anataka kupigia mstari anayoyasema. Ukarabati unaweza kuwa hata wa 1bn inategemea na aina na ukubwa wa nyuma.
 
Naomba mnieleweshe wadau. Hivi ni nani anakagua hesabu sa CAG?
hakuna wa kukagua mahesabu ya CAG yeye anakagua mpaka ofisi ya raisi ni top authority kwenye ukaguzi wa mahesabu ya umma
 
hivi wewe mpuuzi unamjua zaidi Prof. Asad kuliko magufuli? eti umsaidie! maajabu haya.

SImjui hata mmoja wao na sihitaji kumjua na kuongelea kitu kinachohitaji details siyo lazima umjue mtu.Tunachokihitaji ni UKWELI wa hiyo scandal.Mimi kama Muhasibu inatia hasira kuona CAG anakiuka sheria za fedha anazopaswa kuzilinda.Sasa kama huyo anayejiita Prof anakiuka sheria na kanuni za fedha in short hafai kuwa CAG.Ndiyo shida ya kuwaweka academicians kwenye mambo ya utendaji.

Pole bado nitasimamia sentensi yangu hatuhitaji kujua dini ya mtu tunahitaji kuujua ukweli na huu ukweli umsaidie Bunge na JPM kufanya maamuzi.

Kama upuuzi basi hiyo taaluma anayoifanyia kazi huyo Prof.Assad huijui then kaa pembeni.Na pili ukishindwa kuweka hoja mawili kubali au acha vinginevyo usiite wengine waapuzi sababu tu hujajua maana ya hoja ya muhusika.
 
napendekeza wanaohusika wakanushe habari hii vinginevyo watu wataiamini. ikumbukwe kuwa ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ni ofisi nyeti sana katika kupambana na ubadhirifu wa mali za umma. kama kweli kapiga awajibike
 
Binafsi naona stori nzima imekaa kaa kifitina fitina hivi! Jamaa kakosa tenda ya kukarabati nyumba ya CAG alafu anatujia na stori ya kimangamushi!!
Ndugu kwanini naww usingejibu kwa Hoja?
 
Naona huko Mtanzania kuna mradi wa kumchafua Prof.Asad,walianza na kwenda nje bila kibali.Na huyo afisa wa CAG anayetumiwa tutampata tu,asidhani yupo salama
Kamanda unafurahia HELA kupigwa? sasa ikiwa kila Kiongozi anaeTumbuliwa watu mnasema majungu sasa itakuwaje?,au watumbuliwe wadogobtu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…