Nimesoma! Nimetishika! Nimebabaika kuona haya! Y
Zaidi nimeogopa sana kusikia eti Benki ya Posta imesimamisha sehemu ya watu wa management sio kwa tuhuma hizo la!Ila kwa kudhaniwa ndio waliotoa hizo habari wakati ni siri za kibenki. Hapo ndio nchi hii ilipofika!
Uchunguzi unaanza, SI WA UKWELI WA TUHUMA HIZI, bali WA NANI KAZITOA TUHUMA HIZI!!!
Hii maana yake ni wamba kila kilichosemwa ni sahihi ila mafisadi wametahayari no wanauliza "Hee wamejuaje?"
Nikiulizwa mahala wewe ni mtanzania leo, nitashawishika kusema La hasha! Sitaki kuhusishwa na watanzania wenye uchu, na upumbavu na jeuri ya Benki ya Posta..sitaki kuhusishwa na wezi hawa. Hivi hawana hata mwanasheria uchwara wa kuwapa mlengo wa kufata..au naye ni miongoni mwao?/..hivi mtuhumiwa napounda chombo kujichunguza sio kiini macho na kusaka uchawi. Watanzania wa leo ni wajinga kiasi hicho?!
Busara ndogo, ambazo nadiriki kusema waliopitisha maamuzi hayo hawana, zinaelekeza hivi: awali unaunda tume kuchunguza ukweli/uongo wa tuhuma, (tume huru kabisaa, tena hata BOT(!?) au reputable Audit company); then baada ya report, ikiainisha ni uongo, ndio unakuwa na base ya kutafuta mzushi mwenyewe; na ukikuta ni kweli, unadeal na MAFISADI hao!
Tufanyeje? tuache genge la watu liendelee kufanya maasi ya kifisadi? wakati ni huu...tuwaanike, na wakati huu sasa tuongezee nguvu kulisemea hili! wenye dhamana na kulifanyia kazi wasipolifanyia kazi, basi tuchukue hatua zaidi: tuliwakilishe kunakohusika..kwa nguvu zote..