Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
UBABE WA RAIS KIBAKI ULIKUWA KWA WANANCHI, ILA KWA MKEWE ALIKUWA POYOYO.
Mama Lucy Kibaki, mke wa aliyekuwa rais wa Kenya amefariki dunia muda mfupi uliopita huko Uingereza alipokuwa akitibiwa.
Naomba nichukue fursa hii kuwakumbusha ubabe wa marehemu kwa Mumewe Kibaki na kwa wakenya.
KWA WAKENYA.
Tunaambiwa mke au mume wa rais hawezi kufanya mambo kama vile yeye ni sehemu ya urais ama akafanya lolote kisa mwanandoa wake ni rais. Mke wa rais mara nyingi huwa karibu na jamii kwa kuonesha upendo na kujali.
*Lucy Kibaki mzibua mwanahabari
Ilikuwa tarehe 03/5/2005 Lucy Kibaki alipovamia ofisi za gazeti la Daily Nation, ambapo yeye na timu yake walingia katika ofisi hizo kwa mbwembwe na vurugu huku akilalama kwanini aliandikwa vibaya au isivyo. Songombigo lilopelekea kumnasa makofi mpiga picha wa gazeti hilo, kupora notebook, camera na tape recoder vilivyo tumika kuchukua timbwili lake la ASHA NGEDERE.
* Lucy Kibaki amnasa makofi mshereeshaji wa serikali.
Ilikuwa siku ya sherehe za uhuru wa Kenya terehe 12/12/2007 Lucy Kibaki alimpiga kofi msimamizi mkuu wa sherehe hiyo kisa katambulishwa kwa jina la Lucy Wambui badala ya jina la Lucy Kibaki.
Baada ya tukio hilo watu wa usalama wa taifa waliwanyang'anya camera waandishi wote na kufuta picha na rekodi zote kuhusiana na tukio lile. Hadi sasa ninavyo zungumza hakuna video wala picha ya tukio lile, na ni kwasababu enzi zile smartphone hazikuwako huku East Africa au hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa.
LUCY KIBAKI KWA MUMEWE.
Kibaki alikuwa ni moja kati ya marais wababe Afrika Mashariki na kati, lakini ubabe wake ulikuwa kwa wananchi na maafisa tu wa serikali, lakini kwa mkewe ilikuwa HAPANA, mzee hakuwa na sauti kabisa, sijui Lucy alimpa nini mzee Kibaki?
Media za Kenya zilikuwa zinaripoti kuwa mzee Kibaki anachepuka sana, njia kuu kaipotezea,,, waliandika sana, tena sana. Alichoamua Lucy ni kumlazimisha mumewe kuitisha wanahabari ikulu na kitangaza kama ana mwanamke au wanawake wengine au yuko peke yake Lucy.
Vile vyombo vilivyotangaza ile habari kuwa mzee anachepuka KTN na vinginevyo vilikuwepo. Mzee akatangaza kwa kwa Wakenya kuwa na mke mmoja tu na si mwingine bali Lucy. Wakaambiwa waulize maswali, wa KTN akauliza, na Lucy akaingilia kujibu, yaan, ile Press alikuwa kaindaa yeye kisha akamburuza mzee wa watu hadi kwa wana habari.
PUMZIKA KWA AMANI LUCY KIBAKI.
kwa video za vituko vya Lucy nitawawekea hapa ikiwemo na ile ya kuvamia gazeti la Daily Nation. kwa watu wangu wa nguvu kule whatsp sitawaangusha, tukutane kwenye group letu kisimaChaJangwani.
Njano5
whatsapp/call 0622845394