Ubabe ubabe zoeli la udahili UDSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubabe ubabe zoeli la udahili UDSM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lucchese DeCavalcante, Jan 20, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  MCHAKATO wa kuwarejesha chuoni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, umeanza rasmi chini ya ulinzi mkali huku wanafunzi watano wakishikiliwa na Polisi, wakidaiwa kutaka kusababisha uchochezi.

  Gazeti hili lilishuhudia jana zaidi ya wanafunzi 200 wakiwa wamejipanga kwenye mstari wa usajili ambako walitakiwa kuhakiki majina yao na kupewa fomu za udahili upya na vitambulisho vipya.

  Hata hivyo, hali ya usalama katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, haikuwa shwari asubuhi kutokana na baadhi ya wanafunzi wanaoaminika kutokamilisha masharti ya kurudi chuoni, kuonekana wakiwa wamebeba mabango huku wakiimba.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, polisi waliwakamata wanafunzi wanne waliobeba mabango hayo yenye maneno yanayoweza kuleta uchochezi kwa wanafunzi wengine.

  “Tumewakamata wanafunzi wanne na wapo kituo cha Polisi Oysterbay, kwa kuwa walibeba mabango tunayodhani yana ujumbe ambao ungeleta uchochezi na ushawishi kwa wenzao waweze kuandamana na kusababisha fujo,” alisema Kalunguyeye.

  Wanafunzi waliokamatwa ni Issa Paul, Sabinius Respicius, Bahati Alone na Titus Ndulla, wote wa mwaka wa tatu na mwanafunzi wa tano ambaye hakufahamika alikamatwa akidaiwa kutumia lugha chafu katika eneo la chuo.

  Baada ya kukamatwa kwa wanafunzi hao, gazeti hili lilishuhudia ulinzi ukiimarishwa eneo hilo kwa magari ya Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), moja likiwa na namba PT 0158 yakiwa na askari wenye silaha na karandinga namba STH 2568 likiegeshwa katika eneo la usajili.

  Awali akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema utaratibu wa usajili unakwenda vizuri kwa kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza pamoja na ulinzi na usalama kuimarika.

  Aliwasihi wanafunzi walioshindwa kutimiza masharti kukata rufaa kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ili rufaa zao zifanyiwe tathmini upya na ikithibitika hawana uwezo watarudishwa vyuoni.

  Aidha, alisisitiza kuwa wanafunzi ambao wamejaza fomu lakini hawakutimiza masharti, wakamilishe masharti hayo, kwa kuwa chuo hicho kimeongeza muda wa udahili hadi Januari 29 mwaka huu.

  Gazeti hili liliona moja ya fomu za masharti mapya kwa wanafunzi waliotimiza masharti ya kurudi chuoni ambapo wanatakiwa wawapo chuoni wasiingize mwanafunzi yeyote ambaye hajaruhusiwa kuingia hapo pia hakuna kufanya mkutano wowote katika eneo la chuo bila kibali.Masharti mengine ni kutogoma kuingia darasani wala kufanya maandamano yoyote katika eneo la chuo.

  Baadhi ya wanafunzi waliotimiza masharti walipongeza mchakato huo wa kuwarudisha vyuoni ila waliiomba Serikali kuwafikiria zaidi wale wanafunzi ambao hawana uwezo na kuwarejesha ili waendelee na masomo.

  Leyla Omary ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu alisema pamoja na kwamba masharti yaliyomo kwenye fomu za kudahiliwa upya ni magumu, wanafunzi wengine hawana budi kujitahidi kuyatimiza ili kuokoa muda wa masomo uliopotea.

  HabariLeo ilishuhudia katika eneo la Utawala, wanafunzi wote waliotimiza masharti na kuruhusiwa kuingia chuoni hapo pamoja na wafanyakazi wakiwa wamevaa vitambulisho vipya.
  Nao viongozi waliovuliwa madaraka wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho cha Mlimani (DARUSO), walitoa wiki moja kwa Serikali iwarudishe wanafunzi wote waliosimamishwa masomo vyuoni, la sivyo wataandamana na kufanya kitu ambacho kitawashangaza Watanzania.

  ‘Rais wa DARUSO’, Anthony Machibya, alisema kinachoendelea kwa sasa ni kuwarejesha watoto wa matajiri vyuoni na kuwatekeleza watoto wa masikini, hali ambayo Serikali hiyo haitakubaliana nayo kwani pamoja na kuvuliwa madaraka, wataendelea kutetea haki za wanafunzi wanyonge waliowaweka madarakani.

  “Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika,” alisema Machibya.

  Naye Katibu wa Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma Tanzania (UVEJUTA), Silinda David, aliwataka wanafunzi wote kurejea vyuoni pindi vyuo vitakapofunguliwa. “Na kwa taarifa tulizonazo wahadhiri nao wamegoma kuwafundisha wachache waliopo vyuoni hadi tutakaporejea.”

  Aidha, gazeti hili lilitembelea Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) ambako lilishuhudia wanafunzi wakidahiliwa upya wakiwa chini ya ulinzi mkali lakini hali ikiwa shwari. Nacho, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliitaka Serikali kuacha hujuma dhidi ya wanavyuo masikini.

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho, Erasto Tumbo, alisema anashangaa kuona Rais akikaa kimya bila kutoa tamko kuhusu wanafunzi masikini wanaoshindwa kurudi vyuoni kwa kukosa kutimiza masharti yakiwamo ya ulipaji wa gharama zote za mwisho
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2

 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  1232369221_chuo_2.jpg

  1232369221_chuo_3.jpg

  1232369221_chuo_5.jpg

  1232369221_chuo_6.jpg

  1232369221_chuo_7.jpg

  Kwa stahili hii tutafika kweli na hii ni haki kweli???
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tuwe makini katika elimu yetu tusiingize siasa ndani,wanafunzi wote warudi vyuoni na wote wapate mkopo wa 100% ili waweze kusoma kwa maendeleo ya TZ.Tukianza kubagua kwa kuangalia mwenye uwezo wa kulipia ndio asome na asiye uwezo asisome,dhambi hiyo ya ubaguzi itaitafuna TZ.
   
 5. b

  babalenu Member

  #5
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ama kweli binadamu ni wepesi kusahau! leo hii ndugu zetu watawala wameshiba na hawakumbuki tena kama kuna masikini ambaye hawezi kuikusanya hata laki moja kutimiza hiyo 40%. Dhuluma hii siku hiyo ya hesabu kutakuwa hakutoshi! naongea kama mdau ambaye nimepigika nimelipa hizo asilimia arobaini ili japo wadogo zangu warejee masomoni. mimi walau nina kamshahara jee watoto wa mkulima nadhani wataungana na wazazi wao tuu kulima na sio vinginevyo na matajiri waendelee kupeta.
   
 6. b

  babalenu Member

  #6
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa ni vigumu kuelewa nchi hii vipaumbele vyake ni nini! ukienda Hospitali pale Mwananyamala au muhimbili wagonjwa bado wanalala chini! sasa Uchumi huu utajengwa bila elimu wala afya bora? jamaani jamani ya Zimbabwe yasije kutukuta jamani chondechonde! naona tunacheza! historia inatuambia sisi bado ni masikini sasa mbona tunakandamizana wenyewe jamani? Mungu inusuru Tanzania, inusuru elimu ya juu? wazindue watawala wetu! Ma V8 lendcruiser tunayopishana nayo kila leo si dhani kama kuna mashindano ya mbio za magari mawaziri wanaelekea kushindana bali kutojuo kama tunauana wenyewe bila kujua. ni kweli tuko serious sisi?
   
 7. b

  babalenu Member

  #7
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mbona mnataka kuturudisha kule nyuma tulipokuwa na wasomi wachache! maana watu 2000 wasiporejea chuoni ina maana hapo umetengeneza wahalifu, wazururaji , wangapi?
   
 8. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  je mlio maofisini mnafanya nini?? hamkusoma UDSM?? leo nilipata nafasi ya kuongea na ndugu jamaa na marafiki kuusu hii issue majibu yao yalinivunja moyo kabisa..walianza oo serikali inavyofanya ni vizuri kwasababu wanafunzi wanakula hela kwenye ma baa, simu na starehe zingine...clearly watu wengi hapo dar are out of touch with the harsh realities of all this...hao watoto wa wakulima waende wapi? sitashangaa wizi na some form of terrorism ikianza ilimradi kuamsha jamii...
   
 9. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180

  "Unreflected life is not worthy living," alisema Socrates. Na hapa Tz tuanajitahidi kuishi maisha ya namna hiyo. Tumekwisha!
   
Loading...