Wiki iliyopita palikuwa na mjadala uliohusisha Sumatra, Taboa na Chama cha kutetea Abiria Chakua ukirushwa live na ITV. Hii leo kwa mujibu wa taarifa ya habari 20:00hrs palikuwa na mkutano uliohusisha Sumatra na Taboa ambapo katika mkutano huo Taboa walisusia na kutoka nje.
Katika mjadala wa wiki iliyopita Taboa kilio chao ilikuwa ni kuwataka Sumatra kupitia wizara ya uchukuzi, Polisi kupitia Mambo ya ndani washirikiane na Wadau wote wa usafiri kuona kuwa wapiga debe wanaondolewa kama players katika sekta hii kabisa. Taboa wanadai wapiga debe ni kero kwa wasafiri, wamiliki na hata wafanyakazi wao. Taboa katika madai yao wapiga debe ni wahusika wa moja kwa moja katika kuwaibia abiria hasa katika vipindi vya sikukuu na pia kuwaibia wamiliki katika siku zingine.
Ajabu ni kuwa Sumatra katika mdahalo ule walikwepa kabisa suala la Wapiga debe wala hawakuonyesha hata nia ya kutafuta ufumbuzi. Kwa maana nyingine labda wapiga debe wapo kwa ridhaa yao na kuwa labda upiga debe ni ajira halali.
Kwa mujibu wa taarifa ya leo tokea katika mkutano huo Sumatra wanashinikiza faini za kufikia 500,000/= hizi kutozwa kwa mmiliki kwa makosa ambayo ni ya dereva (mfano makosa ya mwendo kasi).
Hivi hata kwa common sense kwa nini Sumatra hawataki kuona mantiki hizi za wazi? Kwa nini makosa ya dereva yawe makosa ya mmiliki? Hivi mamlaka kama hizi zisizo weza ona hata logic ndogo ndogo kama hizi ni za nini katika zama za leo?