Sijawahi na naogopa kuwapuuza walioifikisha dunia hapa ilipo. Inawezekana walikuwa wajinga (hii ni kutokana labda na mazingira yao waliyokuwepo). Lakini bila shaka walikuwa "rational" ndio wakaweza kufanya tunayoyaona leo yamefanywa. Hawa watu waliopita wamegundua ndege, Computer, mifumo ya kuendesha serikali, mifumo ya kufanya maamuzi, nk, nk.
Sio kizazi cha leo kila kitu tunaona simple tu!
Kujenga majengo-simple tu. Kujenga reli-very simple! Kuwa na shirika la ndege ndege-very simple! Kujenga viwanda-very simple! Kutoa elimu bure-very simple! Kukusanya kodi-very simple! Kujenga uchumi-very simple! Kusimamia utumishi wa umma-very simple! Kukopa-very simple! Kusimamia bandari-very simple! Kuhamia kule-very simple! Kukabiliana na mimba za wanafunzi-very simple! Kukabiliana na changamoto za sekta za madini-very simple! Kukuza uchumi-very simple! Decision making process-very simple! Kuteua wasimamizi wa marndeleo katika county-very simple!
Matokeo yake ndio hayo ya expansion joints, karne ya 21 kujenga reli yenye kuishi miaka 100+ kwa spidi ya 160km/h, watendaji kukosa ubunifu wa kutatua kero za wananchi nk. Mimi hata 1+1 sijawahi kuiona simple kwa kweli.