Uasi wanukia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uasi wanukia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 23, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,152
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Uasi wanukia CCM
  • Vigogo watishana waziwazi

  na Waandishi wetu
  Tanzania Daima

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]HALI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imevurugika, ikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya kuanza kwa vikao vya Halmashauri Kuu (NEC), hapo Septemba 24, kwa ajili ya kuteua majina rasmi ya watakaowania nafasi za uongozi wa juu wa chama hicho.

  Habari za kuaminika zimebainisha kuwa, uhasama mkubwa umezikumba kambi mbili kubwa za wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, wale wa mtandao unaoaminika kukubalika na mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho, na ule unaojinasibu kuwa ni wapambanaji wa ufisadi.

  Uchunguzi wa Tanzania Daima kwa wiki nzima, umebaini kuwepo kwa vikao vingi vya siri baina ya makundi hayo, huku kundi moja likiwa limejizatiti kuhakikisha kuwa majina ya wagombea kutoka kundi jingine hayapitishwi.

  Hata hivyo, katika hatua inayoonesha hali mbaya ya mahusiano baina ya wajumbe wanaounda uongozi wa juu wa CCM ngazi ya taifa, mmoja wa wajumbe ambao wameomba tena kuwania nafasi ya NEC na ambaye anashikilia nyadhifa kadhaa za chama na serikali, alimtolea maneno makali katibu wa CCM wa mkoa mmoja (jina linahifadhiwa) baada ya kukutana uso kwa uso katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam juzi majira ya jioni.

  Kigogo huyo alisikika akimwonya katibu huyo kukaa mbali naye na kumwagiza akawaambie waliomtuma kufuta mara moja mbinu chafu walizoziandaa dhidi yake, la sivyo angelazimika kuanika kile alichokiita uchafu wote anaoujua dhidi yao kwa Watanzania.

  Kadhalika kiongozi huyo alikaririwa akisema kuwa haoni hasara tena ya kuendelea kuwa ndani ya chama kinachoongoza kwa majungu, fitina na chuki, huku akificha siri nyingi za uongo wa viongozi wengi.
  "Kawaambie, tena nakutuma ukawaambie hao waliokutuma, sitaki kufuatwa. Iwe mwanzo na mwisho, vinginevyo nitawaanika kwa Watanzania, ingawa najua mwenyekiti atasikitika.

  "Msione nimenyamaza, mkadhani sijui kile mnachokifanya dhidi yangu. Jaribuni kufuta jina langu, muone kama nanyi sitawaanika kwa Watanzania, wawajue mlivyo wachafu na sijui mtaweka wapi nyuso zenu," alisikika akisema kabla hajapanda gari lake na kuondoka.

  Wakati hayo yakijiri, kauli iliyotolewa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, mapema wiki hii kwamba hatakubali jina lake likatwe bila maelezo, imekikoroga vibaya chama hicho, na kuna taarifa kwamba kundi kubwa la viongozi kutoka mkoani Mara, linajiandaa kuchukua maamuzi magumu, ikiwa kikao cha Halmashauri Kuu kitabariki kuondolewa kwa jina lake.

  Habari kutoka mjini Musoma, zimedai kuwa hatua yoyote ya kukatwa kwa jina la mbunge huyo na mwanasheria maarufu hapa nchini, itakuwa mwanzo wa anguko kubwa la CCM mkoani humo hata kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

  Mkono hata hivyo, hakuwa tayari kuzungumzia jambo hilo alipotakiwa kufanya hivyo na gazeti hili, wala kukiri ama kukana kujua juu ya kuwepo kwa kundi la viongozi wanaomshabikia, waliojiandaa kuchukua maamuzi magumu ikiwa jina lake halitapitishwa.

  Mbunge huyo alikaririwa akieleza kushangazwa kwake na kukatwa kwa jina lake katika ngazi ya mkoa, na kudai kwamba hatakuwa tayari kukubali kirahisi hali hiyo, bila kuambiwa kosa lake katika ulingo wa siasa ndani ya chama hicho lililosababisha hali hiyo.

  Mtifuano mwingine uko katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu ambako mahasimu wakubwa wawili wanachuana.
  Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni inadaiwa anafanyiwa njama za kuenguliwa jina lake ikidaiwa kuwa ni kutokana na uhasama mkubwa alionao dhidi ya mbunge wa sasa, Dk. Titus Kamani.
  Wawili hawa wameshitakiana mahakamani kwa tuhuma za kutaka kuuana, zinazomkabili Dk. Kamani. Hali hiyo inakuja huku jina la Dk. Chegeni likidaiwa kukatwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Busega, Samuel Ngofilo, alikiri kuwepo kwa njama hizo alizoziita chafu zinazolenga kumchafua Dk. Chegeni ili asipitishwe na NEC kugombea wilayani humo.
  Dk. Chegeni pamoja na wagombea wengine watatu, ambao ni Kashen Fanuel, Miknes Mahela na Amos Onesmo, ndio wanawania u-NEC kupitia Wilaya ya Busega, katika Mkoa mpya wa Simiyu.

  "Kuna njama chafu zimeanza kufanywa kwa lengo la kumchafua Dk. Chegeni ili asipitishwe kugombea NEC katika wilaya yetu ya Busega. Kauli ya vijana Busega tunaka NEC itende haki. Dk. Chegeni ni mchapa kazi hodari na CCM wanalijua hili.
  "Kwa kutambua uchapakazi, ushawishi na uhodari wa kujenga na kutetea hoja kwa maslahi ya chama na jamii alionao Chegeni, ndiyo kilichotusukuma tumchukulie fomu ya kugombea NEC. Sasa kama NEC watakata jina lake, tuko tayari kuchukua maamuzi magumu. Hatuwezi kusema kama tutaenda Peoples au la, maana bado mapema mno," alisema.

  Aidha, Ngofilo alimtuhumu Dk. Kamani kwa madai ya kuandika barua kwenda kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, akiomba jina la Dk. Chegeni lisipitishwe kwenda ngazi ya taifa.
  "Siasa za namna hii sisi vijana wa Busega hatuzitaki. Tunachotaka ni kujenga chama chetu kwa kuwa na viongozi makini, hodari na imara katika kupigania maendeleo ya chama na Watanzania. Tunaisihi sana NEC ipuuze uzushi wa aina yoyote ile, na ituletee majina ya watu wanaokubalika kijamii," alisema Ngofilo.

  Alipopigiwa simu yake ya kiganjani juzi ili atoe ufafanuzi juu ya tuhuma hizo, Dk. Kamani alipokea simu na kusema kwa kifupi: "Baadaye" kisha akakata simu.
  Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms), akiombwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alikaa kimya hadi tunakwenda mitamboni.

  Kwa upande wake, Dk. Chegeni alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani ili azungumzie suala hilo la kuundiwa njama chafu kwa lengo la kumchafua, hakuweza kupatikana ambapo baadaye taarifa zilidai kwamba yuko safarini nchini Colombia.
  Kutoka mjini Kahama, habari zinasema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), jana waliungana na kushiriki katika hafla ya kuaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule binafsi ya Kwema Modern.

  Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, inaelezwa kuwa alialikwa ikiwa ni moja ya mikakati ya pamoja na Lembeli, huku kukiwa na taarifa kwamba majina ya wawili hao ni miongoni mwa yale yatakayofyekwa kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC.

  Duru za kisiasa zimebainisha kuwa wawili hao sasa wameamua kushikamana kwa dhati dhidi ya hila zinazoonekana kufanywa na viongozi wenzao ndani ya CCM, ambazo inadaiwa zimechangiwa na kile kinachoelezwa kauli zao tata ambazo zimekuwa mtaji kwa vyama vya upinzani.

  Wakati Sitta akikwaruzana na wenzake ndani ya CCM, Lembeli amekuwa na ‘ugomvi' wa muda mrefu na Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Hamis Mngeja.
  Imeelezwa kuwa wawili hao, wanawania uenyekiti wa chama hicho mkoa.
  Jijini Dar es Salaam, kumezuka tafrani kutoka kwa baadhi ya wagombea wanaodai kuwa majina yao yalienguliwa na kuwekwa mengine kwa maslahi binafsi ya makundi katika chama hicho.

  Katika uchaguzi uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii, kulizuka purukushani kubwa zilizotaka kusababisha kuchapana makonde kutokana na kuwepo kwa mizengwe katika uteuzi wa nafasi za uongozi.
  "Jina la kada aliyewahi kuwa Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na aliyewahi kuwa diwani katika Kata ya Ubungo liliondolewa kutokana na kushinikiza arudishwe Diwani wa Makurumla, Rajab Hassan," kilisema chanzo chetu.

  Kwa maelezo ya chanzo hicho, katika vikao vyote vya mkoa, sekretarieti, kamati ya maadili ya mkoa na kamati ya siasa ilimpendekeza kada huyo aliyeondolewa kwa kuwa ana sifa zote, lakini Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, John Guninita, alishinikiza jina la kada huyo kukatwa kwa maslahi binafsi ya makundi Mkoa wa Dar es Salaam.
  Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hata katika nafasi ya mkutano mkuu wa taifa, kulikuwa na matatizo kwa kuwa baadhi ya wajumbe walikuwa na maslahi yao binafsi.

  Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa, alisema kuwa anadhani kuwa wale wanaolalamika hawajui utaratibu wa vikao vya chini kuwa vinashughulika na matengenezo.
  Mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ametishia kuwazuia waandishi wa habari watakaotangaza habari ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa juu, kuingia ndani ya viwanja vya makao makuu ya chama hicho.
  Nape akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa wamewaelekeza walinzi wao kutoruhusu waandishi wa chombo kilichoandika habari za barabarani kuingia ndani ya jengo hilo.

  Alisema kwa muda wa siku tatu wamekuwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ambapo kazi yake kubwa ni kupokea taarifa ya mapendekezo kutoka wilayani na mikoani na kuziunganisha pamoja na kuziboresha.

  Alisema nafasi ambazo ziliombwa na zitajadiliwa na vikao hivyo ni wajumbe wa NEC kupitia wilaya na wale wa Zanzibar na Tanzania Bara, nafasi ya uenyekiti, katibu uenezi na uchumi wa mkoa na wagombea kutoka jumuiya mbalimbali za chama hicho.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Ndani ya CCM wamo hao? (rangi nyekundu)

  Hizi ni sarakasi tu za wanasiasa wachumia tumbo. Anaweka mkwara ili asikoseshwe ulaji.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,152
  Trophy Points: 280
  Wanajiita tu kwamba ni "wapambanaji wa ufisadi" wakati hakuna mafanikio yoyote ya hayo mapambano yao. Ufisadi ndani ya magamba na Serikali umeshamiri kupita kiasi na kuanza kutishia usalama wa nchi.

   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mpambanaji mwenyewe ni sita eti!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,145
  Trophy Points: 280
  Nilikua siamini kuwa ccm imekufa.
  Buriani jembe na nyundo
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,596
  Likes Received: 82,152
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi tunasubiri mazishi tu ya magamba ili wapotee kabisa katika anga za siasa Tanzania

   
 7. c

  chama JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndoto za alinacha hiki ni chama cha mapinduzi; waliondoka kina Mrema hapo mwendo mdundo asiyekubali maamuzi sahihi ya chama na aanze!

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 8. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mtakufa nyie ... CCM mtaiacha ikiwepo Daima
   
 9. A

  Andras Mahenge Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utamu utazidi baada ya siku mbili Mchakato utakapohitimishwa utaona kundi kubwa la magamba yakijitangaza kuvua magamba yao, wengine kwenda CCJ, Wengine M4C n.k..! Patamu...hapo!
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  jembe na nyundo vimeshakufa na kuzikwa siku nyingi tunataka kwenda kuchimba kaburi na kuchukua nyundo na jembe kwani mipini ilishaliwa.
  tumepata mteja wa vyuma chakavu.
  kwani wanadai kuwa vifaa vya mwalimu vilikuwa imara sana.
   
 11. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kumbe siku hizi uongozi ndani ya ccm ni vita na sio wito na Nia ya kuongoza kwa nidhamu na matwaji ya wanaNchi katika kura tena???

  Sent by chescomatunda using JamiiForums
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  baada ya tarehe 24 vitaibuka vituko vingi sana ndani ya CCM ngojeni muone...........
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Aisee siku ya kuizika hii laana inaitwa CCM, maisha yatakuwa si yale tena!!! raha mnooooooooooo
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wote tunajua hiyo ni brand name ya hao watu.
   
 15. Kanyapini

  Kanyapini JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vita ya panzi, furaha kwa kunguru!
   
 16. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nape akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa wamewaelekeza walinzi wao kutoruhusu waandishi wa chombo kilichoandika habari za barabarani kuingia ndani ya jengo hilo.
  Nape:
  1. Mlinzi atajuaje kama Mwandishi huyu anaandika habari za barabarani?
  2. Habari za Barabarani ni zipi?
  3. Habari ni haki ya msingi ya kila mwananchi swala la kwamba habari ni ya barabarani au Ndani ya ofisi hilo ni kazi ya msomaji kuchambua ndiyo maana kuna magazeti ya udaku
   
 17. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  NEC huwa ina wajumbe wangapi na wamegawanyikaje, kimikoa au majimbo?
   
 18. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ombeni uzuma ili mshuhudia kuwepo kwa CCM mbili nchini.
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pindi CCM kinapohamishia utaalam wake wa UCHAKACHUZI WA CHAGUZI ZA KITAIFA na kuamua kuitumia katika VITA VYA MAKUNDI mle ndani kudhibiti wengine wasifurukute huku wale wasio na ustahili wowote wakionekana kuvikwa taji; WaTanzania ule utabiri wa Mwalimu Nyerere kwa chama hiki hivi sasa ndio umewadio na tukae mkao wa kuona mazito yakijitokeza hivi karibuni.
   
 20. F

  FUSO JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,859
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  wewe inaonekana umekua juzi, sisi tulisoma vikao vyote vya ccm kuanzia tawi hadi taifa tena tukiwa primary, wakati huo bila kuwajua wajumbe wa vikao vya ccm basi somo la siasa unafeli.

  Tulikaririshwa as if katiba hiyo ilikuwa ya taifa.
   
Loading...