Uasi sasa wazidi kuizingira CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uasi sasa wazidi kuizingira CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 3, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Waandishi Wetu


  [​IMG]  Wilson Mukama, Katibu Mkuu wa CCM


  MKUTANO wa viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaoendelea Dar es Salaam umekumbwa na jaribio la kufanya uasi dhidi ya baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho, Raia Mwema imeelezwa.


  Taarifa zilizopatikana wiki hii zinasema jaribio hilo la uasi lilikosa nguvu ya kuungwa mkono na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, unaowahusisha Makamu wa Mwenyekiti, Pius Msekwa, wajumbe wa Sekretariati, wenyeviti wa mikoa na makatibu wa mikoa.


  Taarifa zinasema mwenyekiti wa mkoa mmoja mkubwa alijaribu kupenyeza ajenda zilizolenga kuwashambulia baadhi ya viongozi ambao wanatajwa kuathiri kundi lake katika mfumo mpya wa siasa za makundi unaoanza kuota mizizi katika CCM.

  Mwenyekiti huyo aliwashambulia baadhi ya viongozi wa Sekretariati ya CCM inayoongozwa na Wilson Mukama na akimlenga zaidi Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye hivi karibuni, Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Millya, alimfananisha na ugonjwa hatari wa saratani, unaokitafuna chama hicho.

  Nape anatajwa kuchukiwa na kundi mojawapo kati ya makundi ya CCM akidaiwa kupotosha dhana ya kujivua gamba kwa kuwataja hadharani watu wanaotakiwa kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya CCM ingawa yeye amekuwa akisema uamuzi huo si wa kwake binafsi bali ni wa vikao vya chama hicho.


  Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwamo wenyeviti wengine wa mikoa, hawakumuunga mkono mwenyekiti huyo kama ilivyotarajiwa, ikielezwa kuwa kikao kililenga zaidi kujadili utendaji wa chama kama taasisi badala ya kujadili watu.


  Taarifa zinasena wajumbe walikwepa kumuunga mkono mwenyekiti huyo wakitumia muda mwingi zaidi kuwasilisha ripoti zao kwa kuelezea masuala ya watumishi wa chama hicho na mwenendo wa wanachama wa kawaida.


  "Wajumbe walisema kwamba hakuna tatizo miongoni mwa wanachama wa kawaida. Tatizo lipo kwa viongozi wakuu, wakiwamo waandamizi ambao wamekuwa wakitoa kauli zinazowachanganya wanachama na wananchi kwa ujumla, kiasi cha watu kujiuliza kama kilichotamkwa na kiongozi husika ni msimamo wa chama au msimamo binafsi.


  "Lakini wengine wamezungumzia suala la mwenendo wa baadhi ya wanachama wetu kupenda fedha nyakati za uchaguzi. Katika baadhi ya maeneo wamekuwa wakifanya uchaguzi wa ndani iwe kura za maoni au mwingine, kwa kutegemea nani amewapa fedha. Tabia hii inakiathiri sana chama," anasema mtoa habari wetu.


  Mtoa habari huyo alieleza kuwa tatizo jingine lililobainishwa na wajumbe wengi kwenye kikao hicho ni chama hicho kutokuwa na kiongozi mmoja maalumu anayetoa matamko au kauli za chama kuliko ilivyo sasa kwa kila kiongozi kuweza kusema chochote na kikabeba taswira ya msimamo wa chama.


  Mkutano huo wa Msekwa na wenzake umelenga kupeana taarifa za hali halisi ya siasa ndani ya chama hicho lakini taarifa zaidi zinasema kumejitokeza hali ya kutowaamini baadhi ya viongozi wanaoshiriki mkutano huo wakitajwa kuhofiwa kuwasilisha mawazo yao binafsi au mawazo ya makundi wanayoyatumikia, ili kujenga picha kuwa hiyo ndiyo hali halisi ya kisiasa huko wanakotoka.

  Wasiwasi huo unajitokeza kwa kuzingatia kile kinachotajwa na baadhi ya viongozi wa CCM kwamba viongozi hao katika baadhi ya mikoa wamekuja kuwasilisha taarifa ya hali halisi ya kisiasa bila kuitisha vikao vya Kamati za Siasa ngazi ya Mkoa.

  Hata hivyo, mmoja wa viongozi anayeshiriki mkutano huo ametetea hali hiyo akisema makatibu wanao uwezo wa kutoa taarifa za hali halisi kwa kuwa ndio wakuu wa utendaji ngazi ya mikoa.

  Mwenendo wa kikao kilichofanyika jana Jumanne, ulithibitisha wasiwasi huo kutokana na baadhi ya viongozi kutoa kile kinachohusishwa na mawazo yao binafsi ambayo wamewahi kuyatoa mara kwa mara wakiwa mikoani.


  Taarifa kutoka kwenye kikao hicho zinaeleza kuwa hali si tulivu ndani ya CCM na kwamba kundi la viongozi wanaotakiwa kuvuliwa uongozi ndani ya chama hicho limeanza mapambano ya wazi dhidi ya viongozi wa kitaifa wanaopaswa kusimamia mchakato wa kujivua gamba uliopitishwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.


  Kikao hicho kilichoanza Jumatatu wiki hii kimethibitisha kuendelea kuwapo kwa hali ya mivutano kati ya viongozi na kwamba baadhi ya mikoa imeamua waziwazi kupigania baadhi ya watu badala ya chama kama taasisi yenye mifumo na kanuni zake.

  Raia Mwema
  imeelezwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho kuwa kile kilichokuwa kikitiliwa shaka na baadhi ya viongozi wengine CCM ngazi ya mikoa kuwa baadhi ya wenyeviti na makatibu watawasilisha mawazo yao binafsi na si hali halisi ya kisiasa mikoani, kimejidhihirisha.


  Awali, wakati wa maandalizi ya kikao hicho gazeti hili lilipata kuelezwa na baadhi ya viongozi wa ngazi ya mikoa kuwa hawana imani na wenzao hao (baadhi ya wenyeviti na makatibu wa mikoa) kwa kuwa watawasilisha mawazo yao binafsi au yale yanayozingatia mtazamo wa makundi yao kisiasa badala ya hali halisi ya kisiasa mikoani wanakotoka.


  "Tuna wasiwasi hawa makatibu na wenyeviti wengine ndiyo waloshiriki kuvuruga kura za maoni kwenye Uchaguzi Mkuu, mwaka jana, walikula pesa za watu na kuwaengua wale tuliowachagua na tukashindwa ubunge. Sasa hawa hawezi kutoa taarifa za kweli. Ni watuhumiwa hawa, wao ndiyo wavurugaji wa hali ya kisiasa ndani ya chama huku mikoani."


  "Tunajua wengine watatoa taarifa zilizoandaliwa na makundi yao ya kisiasa na si hali halisi ya siasa mkoani. Wamejijengea mifumo yao ya kulipana fedha na fadhila kwenye makundi yao ya kifisadi," alisema mmoja wa viongozi wa vijana kutoka mkoani Mbeya, ambaye hakutaka jina lake kuandikwa akisema si msemaji rasmi wa chama katika masuala ya kikao cha wenyeviti na makatibu.

  Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wamelieleza gazeti hili kuwa uwezekano wa wenyeviti na makatibu kutoa taarifa za uongo kwa manufaa binafsi au makundi wanayoyatumikia ni mkubwa kwa sababu hawakuitisha vikao vya Kamati za Siasa za Mkoa kabla ya kikao hicho cha Dar es Salaam, kilichofanyika wiki hii.


  "Huku kwetu hatujafanya kikao cha Kamati ya Siasa ambacho kingeweza kukusanya maoni ya jumla na halisi, ingawa ni kweli kamati hiyo inaweza kukasimu madaraka yake kwa Sekretariati yake ya Mkoa, lakini tunajua wakati mwingine hata hizi sekretariati ndizo zimeharibu mvuto wa chama kwa kujigeuza magenge ya ufisadi na mawakala wa mafisadi," alisema kiongozi mwingine wa Jumuiya ya Wazazi, mkoani Shinyanga.


  Katika kikao chake cha awali kati ya Msekwa na wenyeviti hao wa CCM, imeelezwa kuwa wengi waliweka bayana kuwa mchakato wa kura za maoni wa kuwapata wagombea ubunge, ulichangia kwa kiasi kikubwa kuvunja nguvu za chama hicho.


  Msekwa aliwaeleza waandishi wa habari Juzi Jumatatu kuwa, suala la kura za maoni limetajwa na wenyeviti hao kama tatizo lililokivuruga chama hicho, ambako kadi feki za uanachama wa chama hicho zilitengenezwa kwa kuhusisha mtandao wa baadhi ya viongozi wa CCM waliotaka wagombea wao kushinda kura za maoni.


  Uhalifu huo wa kutengeneza hadi kadi feki za uanachama wa chama hicho ni wa aina yake katika historia ya CCM, chama ambacho kilitokana na muungano wa Afro Shiraz (ASP), kutoka Zanzibar na Tanganyika African Union (TANU) kutoka Tanzania Bara, mwaka 1977.


  Katika hatua nyingine, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahitaji kujiimarisha zaidi katika mikakati ya kisiasa na hasa kwa kutekeleza siasa za kiungwana, zisizokuwa wagawa Watanzania, ikibainika kuwa mijadala ya ndani ya CCM imekuwa ikihusisha makosa ya CHADEMA, kama ilivyokuwa awali, CHADEMA kujinufaisha na makosa ya CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

  Kwa muda mrefu, mtaji wa CHADEMA umekuwa ni makosa ya CCM katika masuala ya kisiasa na hata uendeshaji wa Serikali ambayo kwa baadhi ya Watanzania imejijengea taswira ya kutokuwa na ukali wa kutosha katika kupinga ufisadi.
  Taarifa za uhakika sasa zinaeleza kuwa kati ya mambo ambayo CCM inayafanya kwa tahadhari huku ikitambua uwepo wa CHADEMA ni mpango wake wa kujivua gamba, ambao tayari Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, imekwishakubainisha baadhi ya viongozi wanaopaswa kujivua madaraka.

  Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwapo kwa wabunge zaidi ya 20 walioko tayari kukihama chama hicho endapo mpango wake wa kujisafisha na kukamilisha mageuzi ya ndani hautafanyika hasa kwa kuwaondoa baadhi ya viongozi wasio waadilifu. Inaelezwa kuwa uwezekano huo ni kati ya masuala yanayotazamzwa jicho la karibu na uongozi wa sasa wa CCM.

  Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mpango huo wa kujivua gamba na mwelekeo wa jumla wa CCM sasa unaandaliwa kile kinachoitwa "political road map" (ramani elekezi kisiasa), ambao hata hivyo, kutokana na hali kutokuwa tulivu ndani ya chama hicho katika ngazi ya uongozi, utekelezaji wake unaweza kwa mgumu.


  Inaelezwa kwamba CCM imekuwa ikiathirika zaidi na migogoro ya ndani kwa upande wa Tanzania Bara tofauti na hali ilivyo kwa upande wa Zanzibar, ambako uzoefu unaonesha kuwa mpasuko umekuwa ukijitokeza wakati wa kumtafuta mgombea urais visiwani humo kwa tiketi ya CCM.


  Msekwa amenukuliwa akiwaeleza waandishi wa habari Jumatatu wiki hii, Dar es Salaam, wakati wa mapumziko ya kikao kati yake na wenyeviti wa mikoa wa CCM akisema wamepokea taarifa za hali halisi ya kisiasa na amani mikoani na kwamba hicho si kikao cha kimaamuzi.

   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jamani tuongee ukweli hizi siasa za gamba hawa jamaa hawaziwezi
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  makoleo chepeto sululu zote zimevunjka magamba yameng'ang'ania viunoni,namwaminia Chenge slow killer
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Acha wapasuane, nzuri sana hiyo! Huyo Mwenyekiti wa mko "mkubwa" atakuwa Guninita tu,aminia sana jamaaa
   
 5. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tulijua haya yanakuja, na bado yataendelea.

  Nilisema hapa wakati Nape anatalii huko majuu, wenzake wanapanga mikakati hapa ya kummaliza. Bahati mbaya hana mtetezi wa ndani kama wenzake Chiligati na Mwigulu.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/187648-ripoti-ya-ajabu-ya-nape-huko-houston-2.html

  Mukama na Msekwa wanajaribu kuzima kidogo mambo kwa kisingizio cha kupokea taarifa za utendaji, lakini hiyo haikuwa sababu ya wao kuitisha hiki kikao. Hili bado linaendela na litawasumbua sana.

  Makatibu wengi wako kimya japo hawakubaliani na mengi ya Nape na Chiligati. Ukimya wao unatokana na kuwa nafasi zao ni za kuteuliwa, wakifungua midomo wanaweza kujikuta nje au kuhamishwa vituo.

  Wenyeviti hawa watasema sana bila woga, kwani nafasi zao ni za kuchaguliwa na uchaguzi mwingine ni hadi 2012. Kuwafukuza uenyekiti/uwanachama itakuwa balaa juu ya balaa. Hilo haliwezekani na halitatokea.

  Moja wapo wa mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wakati wa kuelekea uchaguzi wa 2012, kelele na vikwazo viwe havipo. Kambi itakayoibuka kidedea hiyo 2012 itakuwa na nafasi nzuri sana ya kuweka mgombea wa CCM 2015. Nape, Chiligati na sasa kaingizwa Sitta watakuwa na hali ngumu sana kuelekea hiyo 2012. Hapo sasa ndiyo patakuwa patamu.
   
 6. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CCM, "Dhana ya ubaguzi itawamaliza", siyo maneno yangu hayo, ni maneno ya Mwalimu.
   
 7. R

  Real Masai Senior Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ntafurahi sana kama kundi la NEPI na wenziwe wakitoswa uchaguzi wa 2012
   
 8. K

  Kiti JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Waacheni Wafu wawazike marehemu
   
Loading...