Uasi hauishi kwa kuombana msamaha. Ni suala la muda tu na timing kwa pande zote mbili

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
227
597
Na Thadei Ole Mushi.

Kwa kweli Sisi CCM tumekasirika sana kwa Chadema kutokuwafukuza hawa wabunge. Tuna hasira mno hakuna kitu nilikuwa nakitamani mimi na wanaccm wengine kama kufukuzwa kwa hawa wajamaa.

Mmeonyesha ukomavu wa hali ya juu sana na mmepata faida zifuatazo.

1. Mngewafukuza mngelipoteza haya majimbo kabisa. Hali ya mambo na jinsi chaguzi zilivyo kwa sasa ni vigumu sana kwa chadema kushinda mbele ya CCM Mpya. Mngewafukuza haya majimbo mngeyapoteza moja kwa moja.

2. Aina ya Wabunge ambao mlikuwa muwafukuze (Komu na Kubenea) ni watu ambao wanakijua chama sana na haswa siri za Chama. MTU kama Komu huyu alikuwa mkurugenzi wa fedha na Uchumi Chadema anajua mambo mengi kuhusu maswala ya fedha ndani ya Chama. Ukimfukuza ni sawasawa na kutaka kujivua nguo mwenyewe pindi atakapoamua kuweka mambo ambayo hayajulikani hadharani.

3. Mmefanikiwa kutuliza Joto ndani ya Chama, wanachama walianza kupasuka kutokana na issue hii. Kitendo cha wao kuomba msamaha na kubakizwa kimetuliza na kuwaleta wanachama pamoja.

Kwa haya matatu hongereni sana, Ila maswali yanayobakia ni muhimu pia kutazamwa.

1. Vipi kuhusu mapendekezo ya Komu kuwa Mbowe achunguzwe na TAKUKURU kuhusu Ruzuku je pendekezo hili wanaweza kulizuia?

Kwa mujibu wa Clip ya mazungumzo yao iliyovuja, Komu anasikika akisema Upande wa Serikali ni dhaifu na hawajui ni wapi wanatakiwa washughulike na Mbowe. Kwa maelezo yake inaonekana kwamba kama TAKUKURU watatimiza wajibu wao ipasavyo basi Mbowe ana Kesi ya Kujibu kuhusu Ruzuku. Huyu anayeongea hivi ni mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa CHADEMA.

TAKUKURU wanataka ushahidi gani tena kuhusu swala hili? Nitashangaa kama mpaka sasa hawajafunhua jalada la uchunguzi kuondoa sintofahamu hii kwenye jamii. Kwa hili Komu katusaidia sana na hasara hii aliyowapatia hata kama kaomba msamaha bado itawagharimu tu.

2. Uasi huwa hauishi mpaka utekelezwe, kuna kitu cha kujiuliza hapa.... Komu na kubenea walikuwa na mgogoro na nani? Je huo mgogoro umesha?

Kubenea na Komu ni dhahiri kuwa hawawezi tena daima kuwa na mahusiano ya kuaminika kati yao na Mbowe na Meya Jacob. Kilichofanyika hapa ni kuondoa joto lililokuwa linafuka ndani ya chama.

Rohoni bado wanaendelea na mipango yao na kwa vyovyote vile wataitekeleza pindi tu wanatakapopata nafasi.

3. Upande wa Mbowe na Meya Jacob hawajaimaliza hii vita. Hawa Kina Kubenea na Komu wanapaswa kuishi kwa tahadhari kubwa sana ndani ya Chadema.

Mbowe si mtu wa kuchezea hata kidogo, hakuna ambaye aliwahi kushinda vita na Mbowe hata siku moja hasa vita ya Uenyekiti.

Mbowe ana Fitna Kali sana kama aliweza kuwadhibiti kwa pamoja Kitila, Zitto na Mwigamba ushirika ambao ulikuwa na watu smart kama Zitto na Kitila itakuwa kwa Komu na Kubenea?

Hawa ni swala la Muda tu, kama hawatakwenda kumwangukia Mbowe Magotini na kuomba msamaha wa dhati basi ushauri ninaowapa ni kuhama chama tu vinginevyo kitakachowapata kitakuwa ni cha kusimulia vizazi vijavyo.

Na kama TAKUKURU wataanza kumshughulikia Mbowe dhahiri kina Komu watapaswa kuwajibika moja kwa moja.

Ngoja tuone.

Ole Mushi.
0712702602
 
Mwanasiasa pekee nimuaminiye Tanzania ni LISSU, haijarishi akawa na mapungufu mangapi ila Lissu ni mfano wa kuigwa kwa wote.
 
Mwanasiasa pekee nimuaminiye Tanzania ni LISSU, haijarishi akawa na mapungufu mangapi ila Lissu ni mfano wa kuigwa kwa wote.
Unamzungumzia Lissuu huyu alisemaga Lowasaa ni fisadi papa na hasafishiki...hahahaha..Lissuu huyu aliyekuwa akiwasaidia Acassia kuipiga serikali ili waendelee kuiba madini yetu...shwainnnnnnnyyyy...jinga sana...
 
Mwanasiasa pekee nimuaminiye Tanzania ni LISSU, haijarishi akawa na mapungufu mangapi ila Lissu ni mfano wa kuigwa kwa wote.
Lissu mwenyewe haaminiki ndugu..yeye ndio aliandaa orodha ya mafisadi akamtaja na lowasa kuwa ni fisadi mkuu..akazunguka na chopa nchi nzima kumtangaza lowasa fisadi kwa miaka nane..lowasa alipochukua fomu ya urais kupitia ccm, akaibuka tena akasema hiyo ni hatari sana kumpa nafasi ya urais lowasa..lowasa alipohamia kwao yeye akawa wa kwanza kumnadi majukwaani kuwa anafaa urais..
So mwanasiasa usimuamini..tundulissu atawaacha katika saa ambayo hamjategemea..anaweza kwenda hata act..uwe mguu pande mguu sawa tu
 
mbona hata gekuli mlisema alizaa na mbowe lakini juzi mkamwita shujaa?
 
Unamzungumzia Lissuu huyu alisemaga Lowasaa ni fisadi papa na hasafishiki...hahahaha..Lissuu huyu aliyekuwa akiwasaidia Acassia kuipiga serikali ili waendelee kuiba madini yetu...shwainnnnnnnyyyy...jinga sana...
Mikataba mibovu ya madini mliipitisha wenyewe kwa raha zenu. Sheria mbovu za madini mlipitisha wenyewe akiwemo huyo anaejiita mzalendo namba moja, kwa vifijo na nderemo, baada ya kuwatoa nje ya Bunge Lissu na wenzie walipokuwa wakizipinga kutokana na madhara yake kwa nchi yetu. Katika hali hii ninashuku uwezo wako wa kuelewa na kutafakari mambo ya msingi, ni duni sana.
Anaesababisha tuendelee kuibiwa kama taifa ni nyie CCM. Mtajihidi kunyakuwa 'ushindi', na kutisha watu kwa uharamia, utekaji na mauaji, LAKINI historia imeshathibitisha kuwa hakuna mwenye uwezo wa kukimbia milele. Angalia Sadam, Gadafi, Chausesco wa Rumania, Slobodon na wengine walioishi kwa ubabe/maonevu walikoishia.
Saa yakaribia ambapo matendo yenu ndio yanakuja kuwaumbua na kuwasuta. Adui wa uchumi wa nchi hii atawekwa hadharani. Na nyie wote mliokuwa mkila nae na kumtukuza, mtamkana. Amen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom