Uandishi wa filamu COVID-19 'Owning the Nerative'

mzawahalisi

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
752
237
Habari za Masiku ndugu zangu? Msiniambie ni mbaya kwasababu ya Corona kwakuwa janga likishakuwa la wengi tunainuka juu ya hilo na kuhakikisha tunasonga mbele no matter what. (Waswahili tunamsemo: Kifo cha wengi ni Harusi@*&$ Sijui hawa wazee walimaanisha nini)

UJUMBE WA JANGA LA COVID 19.
Tupambane kwa njia zote tulishinde hili janga. kwa kuanzia kuepuka kukutana na watu(ACHA SOCIALISATION Isipokuwa kwa njia za kielektroniki), kunawa mikono, kuvaa mask, leso, juba ama chochote kitakacho kinga kusambaa kwa majimaji yako pindi unapoongea, unapopiga chafya ama kukohoa ili kuwalinda wengine, maana njia pekee ya binadamu kulishinda hili janga ni kila binadamu kujiaminisha ameathirika na kujizuia kuambukiza wengine. Njia yoyote ambayo ukiiwaza unaona itakusaidia kuepukana na hili janga we ifate tu ilimradi haihatarishi maisha ya watu wengine. Maana Mungu alitupa akili ili tuzitumie kuyamudu mazingira yetu.

MADA KUU
Katika hili Janga La Corona tunapata mda mrefu wa kukaa na kutafakari Mambo Mengi sana hata ambayo sio taaluma zetu. Jana Nimejikuta nawaza
juu ya filamu zitakazo toka baada ya hili janga.
Nikaanza kupata imaginations kuwa hili Janga ninavyo pamba moto pale Marekani, wale watunzi wa Filamu wa Holly wood wanafanya nini? watunzi wa Fillamu wa Seul Korea wanafanya nini? Watunzi wa Filamu pale Beijing wanafanya nini mda huu ambapo serikali ya china inapotangaza Kuelekea kwenye ushindi dhidi ya Corona?

Majibu niliyopata wale wa Holly wood wanafanya kila liwezekanalo wapate inside story ya vikao vya Dr Fauci na timu yake, strategies, na Visa vya hapa na pale kuendelea kujazilizia series ambayo katika maandishi inaweza kuwa ishafika season three mpaka sasa. hawachezi mbali na watumishi wa ikulu ambao masikio yao yanapenya kwenye vikao vya Trump.Hawa jamaa Wako so diverse kiasi kwamba hili janga litazalisha Maelfu ya Maandiko ya Movie yote yakipambana kupata funding na mwisho wa siku zitapatikana mamia ya Movies yenye angle tofauti tofauti juu ya janga hili. Natarajia kuona movies za conspiracy theories, ushujaa wa kimarekani, arrogance ya kiamerica na jinsi ilivyochangia kuenea zaidi kwa janga hilo, juu ya CIA walivyoshiriki katika mapambano dhidi ya janga hili, na Memgine mengi yenye kubeba American narative ya hii story. Hawa walengwa wao ni Dunia nzima kwa maana wanaamini wao ndio story teller wa dunia nzima na wamefanikiwa kuiaminisha Dunia hivyo.

Pale Seul Korea najua sasa hivi watunzi wanagonga Hodi katika maofisi ya wawekezaji na kupiga mamia ya simu kuhakikisha maandiko yao yanapata wawekezaji ili waweze kuproduce heroic movies zenye hadithi ya mapenzi katikati ya vita dhidi COVID 19 na mengine mengi yenye kubeba Narative ya Kikorea. Hawa walengwa wao ni kwanza korea(Both North and South) pili America. nyie wengine mnajikuta tu kwa bahati nzuri.

Hapo Beijing akili yangu inaniambia production ya Bonge la movie la kichina lenye visa vya Kishujaa, mapenzi, kujitoa, uzalendo, vifoo, resilience na Mshikamano wa Watu wachina wakipita katika janga la Corona na kuwaacha wapinzania wao wakijing'ata vidole lishapata bajeti kamili na uzalishaji upo njiani kuanza wakati wowote. Hawa hadhira yao ni Wao wenyewe ndio Maana Hizi movie zitakuwa katika Lugha ya Kichina, ukibaatika basi unapata yenye subtittle ya Kiingereza na Kifansa. Halafu secondary target ni USA na dunia nzima katika harakati za kujenga taswira ya Kimataifa.

Hapo sijenda Italy, Ufaransa, UK na Germany.
Sasa nikarudi Nyumbani ndipo nikapata msukumo wa kuja kutumia jukwaa hili.
Nilipojiuliza waandishi wangu wa Bongo Movie sasa hivi wanafanya nini? Kiukweli kila nikiwaza najikuta napotelea gizani tu sipati jibu la wazi. Maana nilipojiuliza wanafanya nini likaja swali kwani ni akina nani? hilo likaleta hisia nyingine wana taaluma gani? Nikajiuliza huwa wanahamasishwa na nini waandikapo tamthilia zao? (the driving force ya uandishi Bongo movie) Hilo likanikumbusha gape kubwa lililopo kati ya wanataaluma wa sanaa wa Kitanzania na wasanii wenyewe wanaofanya sanaa. Wanaataaluma wakiandika na Kuzalisha movie inakuwa "too formal and robotic" kiasi kwamba inaboa kutazama, wasanii wetu wakiandika movie yes wanafanikiwa kwa sehemu ndogo ya hadhira yao, ila mtu anayetafakari akiangalia inavyoanza anahadithia mpaka itakavyoisha... Hii imenifanya nione Haja ya kutoa wito kwa hizi Pande mbili kuungana na Kufanya kazi pamoja.

Lakini ikabidi nirudie wazo kuu la kujiuliza hao wote wale makanjanja, wataaluma na vipaji vilivyokosa taaluma lakini ndio vinavyoandika na angalau wamelimudu soko wanawaza nini nyakati hizi? wanafanya nini muda huu?
Sasa sijajua wanafanya kazi nnje ya uwezo wa maono yangu ama wamekaa wanatunga insta clips za Corona, ama wanamalizia project zao za penzi la shangazi na jini nsyuba kwakweli imaginations zangu zimekwama katika hili.

Basi nikasikia ndani ya nafsi yangu kuwaita na kuwauliza yafuatayo:

WANATAALUMA YA SANAA
Wasomi wetu wanaomaliza kwenye vitivo vya Sanaa MLIMANI na ma profesa wao wanamchango gani katika sanaa yetu ya Filamu? chuo cha sanaa bagamoyo kinamchango gani katika kuhakikisha Tanzania inamiliki stori zake na vizazi vyetu na vijavyo vitapata sikiliza hadithi zenye maana na malengo katika taifa lao? Je wameanza mchakato wa kukusanya taarifa muhimu zingali za moto kabla hazijaanza kubadilika na kubadilishwa?
Bahati mbaya siwajui ningewatumia haya maswali inbox, ila natumia jukwaa hili kama watasoma naomba wanitoe tongotongo, kama unawajua nisaidie kufikisha maswali haya kwao ikiwezekana nipate majibu kwenye Comment section hapo Chini.

Kila taifa linaandika Historia yake kwa ajili ya hadhira yake kwa ajili ya kulijenga zaidi hilo taifa, kulipambanua uhodari wa hilo taifa kwa vizazi vyao vya sasa na vijavyo,
Ukiacha taifa lako kuhadithiwa na watu wa taifa lengine, vizazi vya taifa lako litabakia kuwa watumwa wa fikra kwa mtunzi na mwandishi wa stori hizo maana hajawahi na haitotokea mtunzi wa mataifa hayo kuliandikia vyema taifa la Mwingine dhidi ya taifa lake na watu wake binafsi.

Huu ni mda wa Kujifungia sehemu zenye utulivu kuandika kwa weledi wa hali ya Juu kwa kutumia facts zilizopo kwenye open source kama internet bali pia ni mda wa kuwa karibu kimawasiliano na wapambanaji wetu wa janga hili kwa Taifa letu ilikupata taarifa za ndani mbazo wanakubali kushare na wewe. ni kazi ya muandishi kupush harder kupata taarifa zinazokaribiana na Ukweli ambazo ataziwekea na vionjo ili kupatikana kwa story yenye kuvutia mtazamaji.
Ni wakati wa kuwatafuta wataalamu wenye ufahamu kwenye kila nyanja unayotaka kugusia kwenye filamu yako na kutengeneza panel ya kupitia maandiko yako hata kwa njia ya mtandao ili unachoandika kisije kuwa kichekesho kwa watu wa fani husika na watafiti. Na Kuhakikisha wataalamu hao wanahudhuria uzalishaji wa movie hiyo ili kuzuia matukio ya "Dokta kuonekana akichoma sindano mgonjwa wa kawaida na nesi akiandika prescription."

Wataalamu wetu wenye taaluma Mkishaandika ni kukaa chini na waandishi wa sasa ili waweke maudambwidambwi yao na Vionjo vyao maana wao ndio wanajua soko linataka nini, lakini wataalamu mnakuwa mmeshajenga msingi wa dhima nzima ya Filamu hisika.

WAANDISHI WETU WA FILAMU
Nyinyi ndio mmeshika soko na mna soko kubwa kweli kweli. Niwashauri Kuwatumia wataalamu hao hapo juu muwatafute uzuri vyuo vipo karibu, fata hao maprofesa na Madokta vijana. waite mkae chini muandike maandiko yatakayo beba picha halisi ya mapambano dhidi ya Gonjwa Hili.

Pia mnaweza tumia umaarufu wenu reach out kwa Potential investors wawekeze kwwnye filamu zenu. Maana kama nyimba ua Dakika 5 inafanyiwa investment ya milioni 50 mpaka 100, Filamu siinatakiwa iwe na bajeti ya Bilioni kabisa? Kaeni chini na wataalamu ya mambo ya Fenda, Maafisa mikopo na Matajiri wa Jiji. Amini nawaambia Mkiweza Zalisha Movie Nzuri yenye kumbukumbu sahihi na zinazikaribiana sana na Ukweli basi watu wenu na vizazi na Vizazi vitawashukuru na Hiyo filamu itaishi miaka Mia itatazamwa na vizazi na vizazi.

Kumbuka janga hili ni janga kubwa kuikumba dunia katika kipindi hiki cha Miaka karibia 71 tokea vita ya pili ya Dunia. One in a Century Pandemic.

WIZARA YA HABARI SANAA NA MICHEZO.
Hizi ni aina ya movei ambazo serikali lazima itie mkono wake katika kuhakikisha taifa kama taifa lina milikistory yake. Ni swala la kitamaduni, kijamii katika kujengea taifa letu mtazamo wa kujitambua wenyewe na magumu taifa letu linayopitia na namna kizazi hiki kilivyopambana kuhakikisha tunalishinda hili janga na tunaendelea kulijenga taifa kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili nao wajue wanawajibu wa kuhakikisha wanayatunza watakayo yakuta na kujenga zaidi ili kuridhisha vizazi baada ya vyao. Hivyo ndivyo taifa linavyojengwa kwa mioyo kwa kila kizazi kutambua wanajukumu juu ya taifa lao kwa ajili yao na vizazi vijavyo.

Lakini nitoe tahadhari; movie hiyo isije kuwa hadithi ya kusadikika yenye upande mmoja tu wa shilingi. Itapoteza effect ya adrenaline rush kwa watazamji. kwa maana Binadamu kwa asili tulivyoubwa sio wakamilifu. tunafanya maamuzi mazuri na mabaya.Na yote ni muhimu yakaonekana kwenye Tamthilia husika ili kuleta uhalisia.
Kwa sasa niishie Hapa.

Dah! Muda wa kufanya mazoeizi kidogo kuhakikisha mwili upo fit kupambana na Stress za Corona Umefika ngoja nikakimbie kwanza nitarudi Baadae..
 
Back
Top Bottom