Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Leo ni siku ya mchezo wa mwisho wa kundi la AFCON, mjadala mkubwa haupo tena uwanjani bali pia kwenye vyombo vya habari. Leo asubuhi baadhi ya waandishi wa Clouds FM wamejikuta wakilaumiwa kwa kile kinachoonekana kama kulazimisha matumaini yasiyo na msingi kwa Watanzania.
Asubuhi ya leo kwenye kipindi cha Power Breakfast nikasikia mahojiano baina ya mwandishi mmoja wa kituo cha Clouds FM akiwahoji wananchi kuhusu game ya leo. Aisee huyo Dickson Masanja sio mwandishi kabsa.
Clouds FM mmefeli sana kwa Dickson Masanja, we bwana mkubwa badala ya kuwasilisha uhalisia wa kiwango cha timu ya taifa ya Tanzania, umechagua kusukuma simulizi linaloilinganisha Tanzania na mataifa yenye nguvu na uzoefu mkubwa barani Afrika kama Tunisia? Serious!?
Wananchi si wajinga kama waandishi wengi wanavyodhania. Wanaona uchezaji, wanafahamu mapungufu, na wanatambua tofauti ya viwango. Tatizo linapokuja pale ambapo waandishi wanapofanya mahojiano kwa mtindo wa kushinikiza—wakihitaji kusikia jibu moja tu: kwamba Taifa Stars itafuzu ama Taifa Stars ndio Bingwa wa AFCON mwaka huu. Huu si uandishi wa habari huru; ni propaganda isiyo na msingi wowote.
Uandishi wa habari wa michezo unapaswa kujengwa juu ya ukweli, takwimu, na uchambuzi wa kitaalamu futailieni waandishi wengine wanaozungumza ukweli. Kukataa kukiri udhaifu wa timu ni kuwakosea heshima mashabiki na wachezaji wenyewe, we dogo unadai kuwa kwenye game ya Nigeria tulicheza vizuri na tukicheza vile leo tutafuzu.
Kama taifa, tuna wajibu wa kuikubali hali halisi ya soka letu: bado tuko safarini, bado tunajifunza, na bado hatujafikia kiwango cha vigogo wa Afrika. Waandishi wanapaswa kuwa sauti ya uhalisia, si walazimishaji wa ndoto za Mchana. Dickson Masanja wewe sio mwandishi wa habari kabsa, yaani badala ya kuuliza watu msimamo wao we jamaa unalazimisha watu waitazame Taifa Stars ikiwa na kiwango cha juu kuzidi timu ya taifa ya Tunisia.