Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 5,768
- 21,871
UANAUME WA MIJINI NDIO JINA SAHIHI
Naomba kabla sijaanza kuelezea chochote ni-declare interest kwamba mimi sio mwanaume wa Dar na wala sijazaliwa mjini/jijini.
Kwanza kabisa naomba nijifanye mimi binafsi kama case study ya hili jambo. Nina takribani miaka miwili (2) tangu nije kwenye moja ya majiji makubwa hapa Tz lililopo kanda ya mashariki. Maisha yangu yote nimezaliwa na kukulia kijijini kama nilivyoeleza hapo mwanzo.
Naomba niseme tuu kwamba maisha ya mjini na kijijni(vijiji vya sasa) yametofautiana kitu kimoja tuu, aina za kazi. Kijijini kazi kuu ni kilimo na ufugaji, wakati kwa wenzetu wa mijini kuna aina lukuki za kazi kuanzia kazi ngumu sana mpaka kazi rahisi kabisa zisizotumia nguvu nyingi.
Hii tofauti ya kazi ndiyo inayofanya pia aina ya milo itafautiane. Huwezi kumpikia mwanaume aliyetoka shamba ugali wa sembe na akala akaridhika ili kesho aende shamba tena, never. Au huwezi kumpikia dona kibosile wa mjini anayefanya kaz masaa 8 huku anapigwa kiyoyozi masaa yote. Anaweza kula dona mlo wa mchana lakini sidhani kama usiku utamlisha dona tena.
Sasa basi, mimi kama mwanaume wa kijijini nilikuja na negative attitudes kuhusiana na hii myth ya wanaume wa Dar. Nilivyofika jijini nikajifanya sili chips wala ndugu zake na chips, nikaendelea na dona zangu kama kawaida mchana na usiku. Lakini bahati mbaya/nzuri nikawa sifanyi kazi ngumu kama zile za kijjini. Baada ya miezi 6 madhara ya kula heavy meals without doing heavy works zikaanza kuonekana. Kakitambi kakaanza kuchomoka from nowhere wakati nilikuwa sina dalili ya kitambi.
Nikajisemea labda ni kuridhika tuu sababu vijipesa navyo vilianza kunitembelea kiaina. Baada ya mwaka hali ikazid kuwa mbaya, kitambi ndo kikazid utadhan mimi ndio bosi wakati bosi hana hata dalili ya kitambi. Kufika hapo ikawa hamna namna zaidi ya kuomba ushauri wa kupunguza mwili. Nikashauriwa kupunguza kula vyakula vya wanga na hata kama nakula basi ni kwa kiasi kidogo sana.
Nashukuru baada ya miezi 3 nikawa nimepunguza 10kg only through diet. Hapa napanga kuanza mazoez ya kukaza tumbo tuu mana mwili usharudi hali yake.
Ushauri kwa wanaume wa mikaoni tunaohamia mijini, kama utakuwa unafanya kazi laini basi epuka kula ile milo yetu ya mama bhoke leta na chungu chote bali kula kiasi tuu. Usiogope kuitwa mwanaume wa Dar kwani mwili ni wako. Kula chochote lkn hakikisha ni balanced diet.