Huyu dada tulianza mahusiano nilpokuwa mkoani kwao kikazi. Baada ya kumaliza kazi nikaenda mkoa mwingine siku zikapita akaja kunipigia simu kuniambia nimtumie nauli anifuate nilipo. Nilimtumia cha kushangaza danadana zikawa nyingi hakuweza kuja nikamwabia anirudishie ile pesa akawa mkali hadi kanitukana sana mm nikawa mpole na namba yake nikaifuta. Nikaenda mkoa mwingine kufanya kazi siku moja napigiwa simu na namba ngeni nikamuuliza we nani akajibu kwajina lake. Aliniuliza uko wapi nkikamwambia mji nilokuwepo akasema na mimi nipo hapa naomba nije kukuona ikamwambia karibu.
Alipofika kaniambia twende nilipokuwa nimefikia tukaenda tukajikumbusha yetu ya enzi nikamuuliza kwann ulinitukana akasema ilikuwa ni chitting mbona nimeamua kukutafuta? Najiuliza kumbe nyie akina dada huwamnatikisa kiberti muone kama kimejaa au hakijajaa?