Wasalaaam,
Ni kijana wa umri wa miaka 23 sasa, nategemea kumaliza elimu yangu ya juu tarehe 16 June mwaka huu.Kifamilia mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, mmoja ni marehemu (wakiume) ko tumebaki wawili mimi na dada yangu mdogo, baba pia ni marehemu ila mama yupo.
Uamuzi wangu kuwa nataka kuoa sasa niendeleze familia/ukoo maana katika ukoo mimi pekee ndio mjukuu wa kiume naeweza uendeleza wote ni wakike. Nimepata binti wa Kisukuma umri miaka 19, hajaenda skuli, mweusi, mwembamba mrefu, adabu anayo, nataka kumfanya mama watoto.
Kaka/dada/baba/mama/ zangu nipeni ushauri juu ya uamuzi wangu natakamama yangu acheze na wajukuu wake maana ni mpweke sana alifiwa mume(baba yangu) na mtoto(mdogo wangu) ndani ya mwezi mmoja.