Uamuzi wangu ndo umeniponza Suraiya

Uamuzi wangu ndo umeniponza Suraiya

Joined
Jul 26, 2015
Posts
49
Reaction score
30
SIMULIZI YA MAPENZI : SURAIYA
MTUNZI : KALAMU NA KARATASI
MAWASILIANO: 0655 08 02 90
MSAMBAZAJI:KALAMU NA KARATASI FOUNDATION
SEHEMU YA KWANZA
Barua Pepe: kalamunakaratasi@gmail.com


Akiwa mwenye huzuni na simanzi kubwa,…nakumbuka aliniomba nipate walau dakika mbili au tatu hivi za kuzungumza nae,ili tu kama kuna lolote amenikosea nimsamehe nami kwa yote nilomkosea tayari amenisamehe.
Nilionekana mgumu na nisiyetaka kujua lolote kumuhusu yeye…pamoja na msisitizo wenye hisia kali aliouweka kwangu.
Alinisihi sana juu ya jambo hilo..tena ili kuthibitisha msamaha wangu kwake,akaniomba nihudhurie siku ya harusi yake ,ambayo alikwenda funga ndoa na Mwanaume mwingine…
kiukweli sikuwa na ujasiri kama ambavyo nilkuwa nao siku za awali za kukutana kwetu.
Yaani…kuhudhuria sherehe ya harusi ya binti ambae nilikuwa nae kimahusiano?..halafu Eti!anaolewa na mwingine…??Hapana Nilishindwa…!!
Asubuhi ya siku ya ndoa tukajikuta tumepata dakika chache za kuzungumza.
Na sehemu hii ya mazungumzo yetu,imebaki kuwa ni kovu na kidonda ambacho sijui ni lini khasa kitafutika katika Maisha yangu.

“Leo Naolewa Jamaal…,lakini tambua bado nakupenda sana na siku zote nitazidi kukupenda”
“Nilijitahidi kwa kiasi na kadiri ya uwezo wangu…Lakini vyote nilivyovionesha kwako vimekuwa kazi bure na umeshindwa kabisa kunielewa”
“Naolewa ilihali nikiwa sifahamu kabisa ni nini kilikusibu,kiasi hata ukachukua uamuzi uliouchukua..!sielewi..!! labda Mungu pekee ndie anaejua jambo hili…”
“Nilikusihi sana tukutane…lakini hata dakika moja hukunipa na mbaya zaidi hukujua hata ni nini nilichotaka kukwambia ukakataa”…
Jamaal..!Kwa Muda Tumekuwa wote katika Mahusiano,hivyo nakujua vizuri nawe naimani unanijua.
”Nakuomba sana,tena ikibidi iwe ni zaidi ya sana..Mateso ulionipa iwe mwisho kwangu,tafadhali usije mfanyia bint mwingine katika hii Dunia …Niahidi Jamaal, hata kwa kimoyomoyo tu inatosha ,kuwa hutofanya hivi kwa mwanamke mwingine katika Maisha yako….”
“Narudia tena kama kuna jambo lolote nilikukosea… naomba kwa dhati kabisa ya Moyo wangu unisamehe na zaidi uniombee Maisha mema huko niendako,na utambue kwamba nimefanya hivi kwa upendo tu nilionao kwako na si vinginevyo”..
Nina mengi ambayo nilitamani nikwambie kama tu ungalinipa nafasi ya kukutana nawe,Lakini ndio hivyo Muda wangu umekwisha na sasa natakiwa kujiandaa kwa ajili ya kwenda kufunga NDOA….Kuwa na Maisha mema Jamaal….!!!
Alikata simu na ukawa ndio MWISHO wa kuisikia tena sauti yake binti Yule.
*************************​
“Kila nikimkumbuka kwa jinsi alivyokuwa akijitahidi kuzidisha ukaribu wake kwangu,uwa sina la kufanya zaidi ya kusikitika na Kubaki nikijilaumu mwenyewe kwa Uamuzi mbovu niliouchukua kwa binti huyu”.
Awali sikujua na kuthamini upendo wake kwangu,labda kwa kuwa bado nilikuwa ningali katika maumivu ya penzi lililopita Kutokana na kile alichonitenda mwanamke niliyekuwa nae hapo awali...
Lakini hata kama!!”
Hivi nini kilichangia kiasi hata nikafikia hatua ya kutoa maamuzi yale??!!”
Maamuzi ambayo hata hivi sasa.. bado yangali yakinigharimu Moyoni..
Kiasi kuzua maswali ambayo pamoja na kukuna kichwa ka namna zote nijuazo, bado sijayapatia majawabu yake ndugu Msikilizaji.
***********​
Siku ile alilia..Alilia kilio ambacho hatokuja kulia tena katika Maisha yake kama ambavyo alilia siku ile.
Ni siku ambayo niliuchukua Uamuzi wa kumwambia kuwa siko tayari kufunga nae Ndoa na kuishi wote kama Mke na Mume.
Hakuamini alichokisikia na bado aliendelea kunisisitiza niache Utani wa namna ile, kwa kuwa hatua tuliyokuwa tumefikia ilikuwa ni mambo machache tu yamebaki ili nikamilishe Uhalali wa kuitwa mume kwake, nae Mke kwangu…
Bila kigugumizi wala kusita nikayarejea tena maneno ambayo nilimweleza hapo awali,kuwa siko tayari kufunga nae pingu za Maisha..
Baada ya kumaliza kusema hayo…Sikuweza kusikia chochote toka upande wa pili ambao nilikuwa nazungumza nao kwa simu, zaidi ya mlipuko wa kilio mithili ya simba alojeruhiwa na risasi…
Na muda mfupi tu kupita… nilipigiwa simu na nambari ambayo ilikuwa ya moja wa marafiki zake chuoni pale.
Baada ya kupokea aliniambia,
”Shem hali ya Mchumba wako ni mbaya kwani tunashangaa tu amepoteza fahamu baada ya kukata simu yako kwani umemfanya nini??”
Kutaka kuonesha kwamba mimi ni Rijali na Jasiri nilimjibu kwa urahisi tu shem wangu huyo….”Hakuna kitu shemeji…atakuwa tu salama..”sikutaka mazungumzo mengi nae nikakakata simu.
Sikujua kilichoendelea na wala sikujishughulisha kulijua hilo
lakini wingi wa simu na jumbe fupi toka kwa ndugu zake waliokuwa wakinifahamu nazo zilizidi kunipa taarifa ya wapi uamuzi wangu umefika….Japo sikujishughulisha kuwajibu au hata kupokea simu zao,lakini khabari nilikuwa nayo.
**************​
Binti huyu Nilikutana nae katika Mazingira ya shuleni kwao hapa Jijini..ambapo yeye alikuwa kidato cha tano,na mimi nilifika pale kwa ajili ya shughuli zangu za kikazi.
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale,tukajikuta tumebadilisha namba na ahadi nyingi za kutafutana mara tu baada ya yeye kurejea likizo kwani alikuwa akisoma bweni.
Miezi sita baada ya kuwa tumeonana….Ni kama alisimama katika msimamo wake,kwani kama tulivyopanga…kweli alinitafuta na ukurasa wa mapenzi yangu na yeye tukawa tumeufungua rasmi..
“Penzi changa lina raha yake jamani..Kila nilichohitaji nilikipata na hata kama hakuwa nacho yeye basi hata kwa kuazima kwa mwenzie alifanya hivyo,ilimradi tu niwe nacho… ”
Hakusita kuwa muwazi kwa kila ambacho alikifanya na kuniomba kuwa msahuri na mwongozo pale ambapo nitaona hayuko sawa.
Nami sikumkatalia nilimuitika kama ambavyo alihitaji.
Tulipenda kukutana mara kwa mara katika moja ya bustani zenye utulivu hapa mjini.Na ni wakati huo tulijikuta tukiutumia kubadilishana mawili matatu yaliyohusu maisha na uhusiano wetu kwa ujumla .
Mipango ilienda mbali kiasi kufikia hatua ya kujiita wachumba na ahadi nyingi za kuja kuoana na hatimae kuwa pamoja kimaisha nazo zilifuatia.
Ni mengi alikuwa nayo…Lakini miongoni mwa tabia alizokuwa nazo na bado ni ngumu kufutika akilini mwangu..!,
“Ni ile tabia yake ya kupenda kulia kwa haraka pale ambapo ilitokea nimemkosea au amenikosea…na alikuwa mwepesi sana wa kumwaga chozi lake huku akiniomba msamaha …Sijui ni kwa nini… lakini binafsi nilijikuta nikiipenda.
Maisha yaliendelea…na baadae alimaliza kidato cha sita na kufaulu kwenda chuo kikuu.
Nazikumbuka sana kumbukumbu hizi kwake,…
”Honey nisome chuo gani?”
Ni miongoni mwa maswali muhimu ambayo niliulizwa nae ikiwa ni sehemu tu ya kuoneshana mahaba..
Hakusita kutekeleza kile ambacho nilimwambia kama ushauri aliouomba kwangu…
Harakati za kwenda chuo zilikamilika,nae kutakiwa kuwasili mapema kwa ajili ya usajili na taratibu nyingine za kichuo.
SIKU namsindikiza kituoni tukiwa tunaagana dakika chache kabla ya basi kuanza safari,nilimuahidi ahadi ambayo hadi leo sitosita kusema mara kwa mara kuwa ingali inanigharimu Maishani mwangu msikilizaji.
“Kasome mpenzi wangu..na muda si mrefu nitakwenda nyumbani kwa ajili ya kutoa posa na mipango mingine nadhani tutafanya mara utakaporejea likizo..”
nilimwambia maneno haya,nae hakusita kunijibu
“Nimekuelewa Laaziizi wangu,ila naomba tuwe wa kwanza kutekeleza maneno yetu kwa vitendo zaidi,kuliko maneno matupu…”
“In shaa llah”,Nilimjibu na kushuka nje ya basi na dakika chache..haooo wakaanza safari,Moyoni niliumia lakini ndio hivyo ningelifanyaje…?!
********
Suala la kwenda kwa wazazi wake halikuwa na shida na kwakuwa tulikuwa dini moja,hicho ndo khasa kigezo kikubwa walichokiangalia..Posa ilikubaliwa na tulianza maandalizi ya ndoa.
Ilikuwa ni zaidi ya furaha pale ambapo nilimueleza bibie juu ya kulikamilisha zoezi lile kwa wazazi wake,kwa kuwa bado alikuwa chuoni mjini morogoro..
Tukaweka mipango kuwa ndoa iwe mwezi wa tisa mara tu,atakaporejea kwa ajili ya likizo ndefu iliyoambatana na masomo yake ya vitendo,ambayo kutokana na uwepo wa jambo hilo…aliomba kuyafanyia hapahapa jijini.
Suraiya…Japo uliolewa lakini sijui nini khasa kinanifanya nikae nikikukumbuka kila mara nituliapo….??
Sitaki nikulinganishe na mwanamke ambae alianza kabla yako..kwani wewe u tofauti kabisa na yeye
SIJUI kwa nini nilikufananisha KIASI hata kukuunganisha na machungu aliyonipa mwenzako Mwarabu.
Kwa nini Suraiyah…

MSOMAJI…NI KWA NINI JAMAAL ANASISITIZA KUTOKUMFANANISHA SURAIYA NA MWARABU??...NI NANI HUYO MWARABU
USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA PILI YA KISA HIKI KITAMU CHENYE KUSISIMUA NA MAFUNZO MBALIMBALI NDANI YAKE KIITWACHO
“SURAIYA”
KUKIPATA KWA UKAMILIFU WAKE AUDIO/MAANDISHI TUWASILIANE 0655 08 02 90
 
Ukiendeleza uniite, hadithi inanigusa
 
Back
Top Bottom