Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,153
- 2,753
Kwa vile alishateua baraza la mawaziri na kuwaapisha angewaacha kila mmoja ashughulike na kuongea kwa namna anavyoweza kwa yaliyotokea Octoba 29 kwa kadiri ya wizara yake ilivyoguswa ingetosha kwa sasa
Kwa vile ameshaunda "tume ya kumuandalia taarifa" ya yaliyotokea octoba 29, alipaswa kujiweka kando kwa muda na swala hilo
Kwa vile alishatoa pole na kukiri kuwa watu waliuliwa wakati anazindua "Bunge lake", angeendelea na majukumu mengine kwasababu nchi inahitaji utekelezaji wa mambo mengi kuliko hiki kinachoendelea
Najaribu kuwaza, haya majibizano yataisha lini? Hizi ngonjera zitakoma lini? Tume ikikamilisha taarifa ataongea nini? Mawaziri waongelee nini kwa sasa? Waziri Mkuu aongelee nini kwa sasa?
Na kubwa kuliko, ikitokea tume ikaja na taarifa kinzani na haya anayoongea itakuwaje?
Kwa namna anavyoliongelea jambo lililotokea octoba 29, tume aliyoiunda itapata wapi ujasiri wa kwenda nje na kile anachokiongea wakati yeye ndio mwenye vyanzo vyote vya taarifa?
Nadhani angeshauriwa aendelee na majukumu mengine na kama anashauku ya kuliongelea asubiri kidogo tu atayasema siku tume itakapokamilisha taarifa yake