Kwangu mimi uaminifu katika mapenzi ni mirage. A hope or wish that you cannot make happen because it is not realistic.
but nisemapo uaminifu namaanisha upo moyoni mwa mtu you can't talk on somebody's position so to you lazima uwe unajua is it realistic or not? naamin huwez kumsemea mtu kamwe daima. hapa tuongelee nafsi zetu.
Hata kwenye nafsi zetu watu huwa ni wagumu sana kujitazama, kujikosoa, na kukiri utovu wao wa uaminifu. Kama hawatatafuta justification ya huo utovu basi watakuwa kwenye denial tu.
Hata kwenye nafsi zetu watu huwa ni wagumu sana kujitazama, kujikosoa, na kukiri utovu wao wa uaminifu. Kama hawatatafuta justification ya huo utovu basi watakuwa kwenye denial tu.
Haya maisha kwa kweli hayako fair.. Unakuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na unapokuwa nae unakuwa huwazi wala huna mpango na wale wengine wanaokufungia break.. Sasa tatizo linakuja kumbe mpenzi uliyenaye kwanza sio mwaminifu pili hana hata mpango na wewe! Mpaka uje ushtuke muda umeshaenda na wale waliokuwa wanakupigia honi huwaoni tena maana ngozi teyari imesha sinyaa huna mvuto teeeeena! Lol.. UMEPOTEZA MUDA WAKO BUREEEE!!!
Kabla sijachangia naomba kujua mtu anaposema yeye muaminifu huwa anamaanisha nini?
Sijui kwa nini umeleta somo gumu usiku huu tena Ijumaa mwanzo wa wikend............Hivi kuwa mwaminifu ni
1. kutokuwa na "mtu wa pembeni" au
2. moyo ulio ulio msafi usio na rekodi ya kuvunja uaminifu ama
3. Moyo mweupe kama theluji usioweza hata kufikiria kuvunja uaminifu
ma brother hujakua usiseme kabisa platozoom. haya uaminifu hauko established kweye kutokucheat la hasha hata kwenye kusema ukweli unapomkosea mpenzi wako. usemapo moyo mweupe hapo sikuelewi so sijaweza kujibu
Kwanza futa kauli yako (red) usinifukuzie ndege bure............Hata mimi sikatai uaminifu unatakiwa kwenye angle zote, na hapo unaweza kurudi kwenye orodha yangu....ili uwe mwaminifu ni criteria gani zinatazmwa (au za kujitizamia) kwa mtazamo wako........kwamba hapa kwenye hivi vigezo hivi mimi kweli ni mwaminifu
dada cathe kwanza waitwa chit chat. haya ngoja ni define uamnifu ni ile hali ya kuwa mkweli kimatendo katika nyanja yeyote ile. inapokuja kwenye mahusiano basi neno hili huweza kujumuishwa si tu kwa kutokuwa mzizi la hasha bali hata kuwa mkweli unapokosea jambo.
orait, vipi kama nakuwa mkweli, sio mzinzi na bado mwenzangu haniamini? Mi naona huo uaminifu ukamilike lazima uhusishe pande mbili. Na upande wa pili yaani mwenzi wako ndio atakuperceive kama wewe ni mwaminifu au lah. Kuna watu wazinzi na wanasema uongo lakini bado wanaonekana ni waaminifu mbele ya wapenzi wao. Huoni kama uaminifu ni vile wanavyokuperceive wengine na si wewe unavyojiona?
Halafu chit chat nimepita dada ila nimeshindwa cha kujibu. Heading yao imenistua sana. Nimetoka kimya kimya.