mAgaziJuTO.
Senior Member
- Feb 22, 2014
- 119
- 37
Mimi ni mwalimu wa kawaida(msingi)Mshahara(soma posho) wangu kutokana na kufuta ujinga watoto wa kinyamwanga ni Tgts C1 ukitoa makato yote+deni la faidika ninabaki na 163,250 mkononi.Nina mke na watoto wawili+mama mzazi.Nimepanga uswahilini ambapo ninalipia 30,000 kwa mwezi(ukitoa kwenye 163,250 kinachobaki ndicho changu).mwezi uliopita nilipokea mshahara(soma posho)tarehe 26,hadi kufikia tar.10 april sikuwa na kitu,hivyo kutoka hapo hadi leo tar 20 naishi kwa mikopo na mizinga.Hadi leo nina deni lisilopungua 70,000 hivyo hadi kufikia mshahara(soma posho)sijui nitakuwa nimebaki na kiasi gani!hivyo nataka kujua,ualimu ni KAZI au SHUGHULI?
sio wakati wa kulalamika ni wakati wa kuangalia ni jinsi gani utaweza kupambana na maisha halafu umesema unamkopo uliolea nini? au kama vipi acha kazi na unakoelekea utakuwa tapeli,kwel kazi ya ualimu ina mshahara mdogo ila kuwa hata mjasiriamali
Nyumba usio lala hujui kunguni wake kote nishida tupu vumilia utatoka kimaisha
Sent from my iPhone using JamiiForums
sasa wewe unampa ushauri au unamponda!kweli wizara ya elimu imeingiliwa mwalimu mzima hujui kuandika unafundisha nini wanafunzi mnaferisha wanafunzi sababu ya kwanza ni nyie
nani kakudanganya kuwa mshahara unakutoa kimaisha badala ya kufungua biashara na kubana matumizi hata upewe milion kama mtu wa pombe haisaidii unalalamika mshahara mdogo hutaki kujiendeleza unategemea ulipwe kiasi gani tukulipe milion wakati darasa la saba soma tutakuongeza mshahara kwa kufuatana na elimu yako kama unaona kazi acha kazi kalime au nenda ulaya ukawe mbeba mabox na sio kuja kulalamika hapa JF jitu zima na watoto wafanyaje
mwalimu gani unaandika ivyo?
Usishangae,ualimu ni kimbilio la waliofeli. Div 4 ndio pass mark zinazohitajika.