Uagizaji wa mafuta wamkera MAKAMBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uagizaji wa mafuta wamkera MAKAMBA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ground Zero, Mar 28, 2012.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba akizungumza na waandishi kuhusu mipang.jpg
  Patricia Kimelemeta Aziza Masoud
  MFUMO wa uagizaji wa mafuta wa pamoja(PAC), umedaiwa kuwa na upungufu katika kanuni zake baada ya kushindwa kuwasili kwa shehena ya kwanza ya mafuta yenye tani laki sita mwishoni mwa mwezi uliopita. Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati wa Nishati na Madini, Januari Makamba alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na wadau wa mafuta jana.
  Makamba alisema kuwa,kamati yake imebaini kuwapo kwa upungufu katika baadhi ya kanuni zinazosababisha kushindwa hata kushusha bei ya bidhaa hiyo kama walivyoahidiwa awali. Alisema, kanuni hizo zimetungwa na kupitishwa na Waziri mwenye dhamana jambo ambalo limesababisha kampuni za wazawa kushindwa kuingia kwenye ushindani wa uagizaji wa mafuta huku ikitoa kipaumbele kwa kampuni za kigeni.

  "Kuna baadhi ya kanuni katika mfumo huu zina upungufu, hii inatokana na kuzipa nguvu kampuni za kigeni kushinda zabuni na kuzibana kampuni za wazawa, jambo ambalo linaweza kusababisha migongano ya hapa na pale," alisema Makamba. Aliongeza kutokana na hali hiyo, kamati yake imetoa mapendekezo ya kuitaka serikali kushirikiana nao ili kuzipitia kanuni hizo na kuzifanyia marekebisho katika vipengele ambavyo vinaonekana vina matatizo ili vifanyiwe marekebisho.

  Alisema mbali na hilo, kamati hiyo pia imeitaka serikali kuboresha miumbonu ya bandari ambayo inasababisha kushindwa kupokea shehena za meli zaidi ya sita kwa wakati mmoja. "Mzigo ulioagizwa mkubwa, ni tani laki sita, lakini miundombinu ya bandari ni mibovu, na kwamba haiwezi kupokea shehena ya meli za mafuta zaidi ya sita, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa waliwahi kuupitisha kabla ya kuangalia vituo hivyo,"aliongeza.
  Alibainisha kutokana na hali hiyo, mpaka sasa mafuta hayo yameshindwa kuwasili, na kwamba PAC imeshindwa kushusha bei ya mafuta kama walivyoahidi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, tatizo la mafuta bado lipo pale pale.

  Alisema kutokana na hali hiyo kamati yake , itatoa mapendekezo kwa serikali ili ihakikishe kuwa kila upande unanufaika ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya bandari ili iweze kuchukua idadi kubwa ya meli zitakazoshusha bidhaa hiyo kwa wingi,jambo linaweza kusaidia kushusha bei .

  Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Petrol nchini, Godwin Samuel alisema kuwa, kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kunatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia. "Ikiwa bei ya mafuta itapungua katika soko la Dunia, na kwamba bei ya usafirishaji itapungua, bei ya bidhaa hiyo katika soko la hapa nchini inaweza kupungua,lakini mfumo huo ni mzuri na kwamba hauna matatizo yoyote yale,"alibainisha.
  Source: Makamba adai mfumo wa uagizaji mafuta wa pamoja una upungufu[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. GY

  GY JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sasa hilo jina la makamba herufi kubwa za nini.....au ndo mambo yetu ya stupid publicity
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,847
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Let Him try his lack!! May be something can happen!! We are the oppressed class!! Always we pray for God to intervene!!
   
 4. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  makamba = big ropes? Or big fishes known as kamba?
   
 5. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  PAC= PIC Ltd? Hivi kwani meli lazima zishushe zote kwa wakati mmoja?
  TPA wanajenga boya hilo, toka mwaka jana.
  Hizi rushwa zingine jamani zinatia kichefuchefu.
  Hata bei ya mafuta ikiongezeka, lazima Tz ipungue eti?
   
 6. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kukereka na kutekeleza ni mambo mawili tofauti, Watz wanataka action sio porojo.
  I wish JWTZ lichukue nchi kama miaka 5 hivi.
   
 7. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama wananchi tunakerwa na walio kwenye uongozi eti nao wanakerwa sasa nani achukue hatua?
   
 8. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Watanzania mnadanganywa bei haiwezi kushuka kwa hiyo "Bulk Oil imports" kwasababu zifuatazo.

  1. Bei ya oil ni ya Kitaifa huwezi kuongea tu na mtu akakupa Bei. Bei inabadilika kila siku na kuna soko la oil ambalo bei inashuka na kupanda kila siku kwa sababu tofauti. Hivyo mtu akikwambia ananunua kwa Bulk na bei inashuka si kweli kwani soko hilohilo lina China, Brazil, USA na China!.
  2. Tanzania tuna magari yasiyozidi Milioni moja (1M Cars) tu sasa hiyo bulk ni ipi wakati mji mmoja hapa Houston, TX tuna magari milioni mbili?. Ni kwanini huyo muuzaji auze mafuta kwa bei ya chini kwa Tanzania?

  Hizi ni mbinu kama tulivyosema mwanzo za waziri wa nishati kula 10% na kampuni kuwa na Oligopoly. Bei badala ya kushuka itapanda kwasababu hakuna ushindani!!.

  Makamba naye alikuwa mjinga kukubali huu upuuzi! Zitto ningemwelewa lakini Makamba amekaa nje anajua hili!!
   
Loading...