UAE inavyozidisha ushawishi Afrika, Tanzania

UAE inavyozidisha ushawishi Afrika, Tanzania

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,919
Reaction score
3,248
DPWorld.jpg



Kumekuwa na ongezeko la ushawisho wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa Bara la Afrika kupitia biashara, uwekezaji, na ushirikiano wa kiusalama na kujijengea nafasi kama mshirika mkuu katika barani humo.

UAE inaiona Afrika kama eneo lenye umuhimu wa kimkakati, ambapo ushiriki wake unasukumwa na masuala ya usalama, biashara, na dhamira ya kushiriki katika uundaji wa mustakabali wa bara hilo.

Maeneo Muhimu ya Ushawishi wa UAE Barani Afrika ni pamoja na Biashara na Uwekezaji, ambapo imekuwa kitovu kikuu cha biashara kwa Afrika, ikiwezesha usafirishaji wa bidhaa kutoka Afrika kwenda masoko ya kimataifa. Pia imewekeza kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi mbalimbali za Afrika, hasa kwenye sekta za madini, mafuta, miundombinu, usafirishaji, na kilimo.

Katika usafirishaji na Miundombinu, UAE imekuwa na uwepo mkubwa Afrika kupitia kampuni kama DP World, ambayo imejenga bandari na miundombinu ya usafirishaji katika nchi kadhaa za Afrika.

Kwa Sekta ya Nishati, UAE inashiriki kikamilifu katika sekta ya nishati barani Afrika, ikijumuisha mafuta na gesi, nishati mbadala, na madini muhimu. Ushiriki huu unachochewa na dhamira ya UAE kuwa kiongozi wa kimataifa katika mpito wa nishati na rasilimali zake kubwa za kifedha.

Katika Ushirikiano wa Kiusalama, UAE imekuwa ikiboresha ushirikiano wake wa kiusalama na nchi za Afrika, hasa Afrika Mashariki, Afrika Kaskazini, na ukanda wa Sahel. Ushirikiano huu unajumuisha uuzaji wa silaha na mipango ya mafunzo.

UAE pia imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu kwa nchi mbalimbali za Afrika, ikichangia maendeleo na utulivu katika kanda.

Tanzania

Tangu Rais Samia Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Machi 2021 ushawishi wa UAE nchini Tanzania umeonngezeka kwa kasi, licha ya ya kuwepo kwa ushirikiano wa awali.

Katika biashara, mnamo mwaka 2022, biashara isiyo ya mafuta kati ya UAE na Tanzania ilifikia Dola za Marekani bilioni 2.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI): Kufikia mapema 2024, UAE ilikuwa miongoni mwa nchi tano bora zaidi zinazowekeza moja kwa moja nchini Tanzania, ikiwa na jumla ya uwekezaji wa takribani Dola 991.5 milioni za Marekani (zaidi ya Sh2.66 trilioni).

Kampuni ya DP World kutoka Dubai ilipata mkataba wa miaka 30 wa kuendesha sehemu nne za Bandari ya Dar es Salaam.

Katika sekta ya nishati, kampuni ya Masdar kutoka UAE imewekeza Dola milioni 181 za Marekani (zaidi ya Sh486.16 bilioni) katika kuendeleza miradi ya umeme wa jua na upepo yenye jumla ya megawati 2,000 nchini Tanzania, kusaidia malengo ya Taifa ya nishati mbadala.

Katika madini na usafirishaji, Septemba 2024, kampuni ya GSG Energies kutoka UAE ilitangaza mpango wa kuwekeza Dola milioni 500 katika sekta za usafirishaji na madini nchini Tanzania.

DP World ilivyozua mzozo

Oktoba 22, 2023 Serikali iliingia makubaliano na DP World kupitia mikataba mitatu iliyosainiwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika bandari hiyo kwa miaka 30.

Tukio hilo lilizua mzozo mkubwa nchini, ambapo baadhi ya wanasheria, wanaharakati wa kisiasa na kiuchumi walipinga suala hilo na kufanya kuwa mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari.

Miongoni mwa waliokuwa wapinzani wa ushirikiano huo ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi ambaye akiwa na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mkataba wa kampuni hiyo. Hata hivyo, walishindwa katika kesi hiyo.

Ndipo mapema mwaka 2024, DP World ilipoanza kazi, ambapo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) iliikabidhi Bandari ya Dar es Salaam kwa kampuni hiyo ili kuendana na ongezeko la mizigo inayohudumiwa.

Hewa ukaa

Desemba 2023 Tanzania ilisaini saini mkataba wa moja ya miradi mikubwa ya mikopo ya kaboni inayotokana na ardhi Afrika Mashariki.

Mradi huo unahusisha hifadhi sita za kitaifa, zenye ukubwa wa hekta milioni 1.8 (ekari milioni 4.4) ambazo ni Burigi-Chato, Uwanda wa Katavi, Mto Ugalla, Mkomazi, Mkondo wa Gombe na Milima ya Mahale

Tanzania, ambayo ina raslimali ya misitu ya karibu hekta milioni 48, imeibuka kuwa moja ya washiriki wa Afrika wanaoongoza katika biashara ya kimataifa ya mikopo ya kaboni.

Mkataba huo ulisainiwa wakati viongozi wa dunia wakiwa Dubai kwa mkutano wa COP28 unaolenga kutafuta njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Pesa zinazolipwa na shirika zinakusudiwa kwenda kwenye miradi ya kupunguza kaboni, kwa hivyo kwa kila tani ya kaboni dioksidi (CO2) iliyotolewa, mkopo unawakilisha tani ya CO2 ambayo ilinaswa.

Mkataba huo mpya ni muungano kati ya wakala wa usimamizi wa mbuga za wanyama nchini Tanzania, Tanapa, na kampuni ya Carbon Tanzania, inayopatikana nchini.

Baadhi ya mapato kutokana na mauzo ya mikopo ya kaboni yataenda kwa Tanapa na Serikali za mitaa, Carbon Tanzania ilisema Alhamisi.

Mbali na kuwezesha biashara ya mikopo ya kaboni, mradi pia "utazingatia ulinzi, uhifadhi, na usimamizi ulioimarishwa wa maeneo haya ya hifadhi ya taifa, kulinda mazingira yao ya asili na rasilimali muhimu za wanyamapori", kampuni hiyo iliongeza.

Mradi huo utapata ufadhili wa ziada kutoka kwa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), kampuni ya kilimo na viwanda inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa Kitanzania, Mohammed Dewji.

Awali Februari 2024, Tanzania iliingia makubaliano ya awali kwa ajili ya mpango mkubwa zaidi wa biashara ya hewa ukaa (carbon credit), unaohusisha eneo la hekta milioni 8.1, ambalo ni takriban asilimia 8 ya eneo lote la ardhi ya Tanzania.

Makubaliano ya Februari yalifikiwa na kampuni ya Blue Carbon, kampuni ya Falme za Kiarabu (UAE) inayodai kutoa suluhisho la uhifadhi wa mazingira na miradi ya kuondoa hewa ukaa kwa kutumia mbinu za kisasa.

Kampuni ya Blue Carbon imekumbwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wanaharakati wa mazingira.

Soma zaidi

Makubaliano ya kibiashara

Tukio la Mei 5, 2025 la utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Shirikisho la Vyama vya Biashara na Viwanda vya UAE na Barazala la Taifa la Biashara kuhusu uanzishwaji wa Baraza la Pamoja la Biashara kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Tanzania, ndi mwendeleo wa ushawishi huo wa Waraabu.

Tukio hilo lilifanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam likishuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Abdullah Bin Zayed Al Nahyan.

Baada ya ttukio hilo, Rais Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Medali ya Mother of the Nation Order (Medali ya Mama wa Taifa) kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan.

Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu Jijini Dar es Salaam Mei 5, 2025.

Medali hiyo ni moja kati ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na hutolewa kutambua mchango Kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake.

Mzozo wa Ngorongoro

tangu miaka ya 1990, baada ya Kampuni ya Otterlo Business Corporation (OBC) inayojishughulisha na kuandaa safari za uwindaji wa wanyamapori kwa ajili ya familia za kifalme kutoka Falme za Kiarabu, kukodishwa kilomita za mraba 1,500 za ardhi inayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Rais Samia alipoingia madarakani alianzisha mkakati wa kuwahamisha wafugaji wa Kimasai wanaoishi katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) na Wilaya ya Ngorongoro na kuwapeleka kupelekwa Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, kwa kile kilichoelezwa ni kulinda mazingira katika hifadhi hiyo.

Hata hivyo baada ya malalamiko mengi, Serikali imeanza kufanya tathmini ya uhamishaji huo.
 
"""uandishi wak tu wewe mwamba unaonesha kuna kitu hakipo sawa kichwani.
Ni kama vile mtu ambae ameugua kwa muda mrefu halafu akapona
."""
 
Naam hawa ndio wanao pendekeza huyu awe rais.
Hata baada ya kelele za ukosefu wa haki, kawa kiziwi kutekeleza matakwa yao.
 
Back
Top Bottom