Ua gani

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1>rangi yako ya waridi,nzuri kama samawati.
Nikahisi ni zawadi,ilojawa na swifati.
Kumbe siyo maridadi,wewe kama afiriti.
Ua hili ua gani,kila mtu alichuma.
2>vijana hadi watoto,wanapenda kulichuma.
Hadi wala misokoto,walichuma kama sima.
Ningekupa mkong'oto,ila sitaka lawama.
Ua hili ua gani,kila mtu alichuma.
3>wengi waliniambia,ua hili ni balaa.
Sikutaka wasikia,nikajifanya kichaa.
Ila leo najutia,hadi nahisi kinyaa.
Ua hili ua gani,kila mtu alichuma.
4>ua sasa lachukiza,lachukiza linakera.
Limekuwa kama giza,msimamo wa bendera.
Tena sitolichunguza,nitaliacha segera.
Ua hili au gani,kila mtu alichuma.
5>ua tena silitaki,chooni nenda litupa.
Lanuka kama samaki,sitolifata kwa pupa.
Nalinda yangu hamaki,nitoe hasira papa.
Ua hili ua gani,kila mtu alichuma.
Shairi=UA GANI.
Mtunzi=IDD NINGA wa Tengeru Arusha.
0755519736.
 

duh bro unaonekana una kipaji cha iyo mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…