Kwani hata Fisadi nambari one Kikwete anatusikilizia lini tutaingia Mitaani Kumng'oa
watanzania na hasa viongozi wetu tumekumbwaa na ka ugonjwa kabaya sana "kusikilizia". Ule msemo maarufu "tafakari chukua hatua" is just for jokes kwenye pombe, au kwenye sherehe na sometimes mikwala ili mtoa mkwala aonekane yuko siriaz!
hebu fikiria:
1. Tuhuma za wiki hii kuhusu jairo na wizara yake - jairo "anasikilizia" nini say raisi ataamua, polisi pia "wanasikilizia" wataamrishwa lini ili nao wafanye uchunguzi, takukuru baada ya kusikilizia kwa mara ya kwanza eti wanachukua hatua ambazo muda si mrefu tutagundua ni bora wangeendelea "kusikilizia".
2. Tatizo la umeme - wananchi "wanasikilizia" serikali itasema na kuamua nini, tanesco "wanaisikilizia" wizara na wizara nayo "inasikilizia".
3. Ubadhirifu katika ununuzi wa rada - pamoja na ushahidi woteunaooonyesha jinsi akina chenge walivyohusika lakini polisi wetu hawawezi hata kuanza uchunguzi kwa sababu "wanasikilizia", takukuru wanendelea "kusikilizia" kwa kisingizio walishafanya uchunguzi, dpp "anasikilizia" na sisi wananchi "tunasikilizia".
4. Sakata la dowans ndiyo usiseme maana hilo hata mkulu alikuwa "anasikilizia"
5. Epa, meremeta, kagoda, deep green etc., wahalifu wake "wanasikilizia", takukuru, dpp wanaendelea "kusikilizia" hata pinda na jk wanatusikilizia sisi wananchi huku nasi tukiwa "tunaisikilizia" serikali.
Kifupi tumekuwa taifa la kusikilizia, mawaziri wetu wanasikilizia, watendaji wa wizara "wanasikilizia" mamlaka husika "zinasikilizia", wananchi "tunasikilizia". Just for your homework show me a country inayoendesha mambo kwa kusikilizia halafu"ikaendelea". Anywayz watanzania tumeamua kuwa watu wa "kusikilizia" basi tuendelee "kusikilizia" hatustahili kumlaumu mtu kwa sababu "ndivyo tulivyo" watu wa "kusikilizia".
Na sisi tunasikilizia nani ataanzisha mapambano ya kumng'oa.
Na sisi tunasikilizia nani ataanzisha mapambano ya kumng'oa.
Nchi makini inayofanya maamuzi magumu ndio hii
kweli nimeamini kweli kama watu wanaiba halafu mpaka leo bado watu wapo ofisini
Nyambala, ndiyo maana hawaishi kutuletea hadithi na misemo. Wanajua tutawasikiliaza tu.Ukiachilia mambo mengi uliyoorodhesha si unaona ngonjera za Jairo, yaani kiongozi mwendamizi wa serikali ana tuhuma za kutoa rushwa kwa watunga sheria bado anapewa likizo ili uchunguzi wa katibu mkuu Luhanjo ufanyike. Lini CAG amewahi kwafikisha wala mapesa au watoa rushwa mahakamani? Luhanjo anasema ametoa siku 10, halafu siku za Jairo kujibu hazijulikani, wa TZ watakuwa wanasikiliza. Mbona Mwakalebela alikamatwa hapo hapo. Luhanjo anataka tumsikilize ili adanganye umma kwa vifungu vya ajabu vya sheria, ili kulindana tu.
Maneno yanayotupumbaza; Mkakati, mchanganuo, tunalifanyia kazi, sheria zifuatwe, mamlaka ya juu, tahmini, uchunguzi wa kina.
Tunatakiwa tuanze na wanaoficha uvundo kama katibu mkuu kiongozi, DPP, DCI, PCCB,IGP.
Hawa ndio wanatumika kuficha uhalifu kwa maneno ya kuudhi.Badala ya kuwasikiliza tuwaambie hatudanganyiki, na hili naanza na katibu mkuu kiongozi.
Tusiposema basi kusikiliza tutaendelea kuwa masikini na wanyonge kila siku. Kwanini tusiazamie kuwa hakuna kuwasikiliza tena? Maamuzi magumu hayaishii kwenye vyama, sisi wananchi ni wakati sasa tuchukue maamuzi magumu dhidi ya wadanganyifu.