TZ na chakula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TZ na chakula

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizotaka, Feb 10, 2012.

 1. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, kwa upande wangu vituko hapa nyumbani haviishi, sijui kama hawa watu tunawaita viongozi huwa wanafikiria vyema kabla ya maamuzi wanayoamua na kuulazimisha uma uamini ni sahihi na kukubaliana nao bila kupingwa, yani zidumu fikra zao. Kituko kipya sinukuu naelezea tu nilivyoipata taarifa " Tanzania imefanywa chanzo cha uzalishaji chakula na itakuwa inakiuza chakula hichi WFP na itaanza kuuza takriban tani 90000 kwa WFP kusaidia nchi zenye njaa.

  Hiki ni kituko, tumeanza lini kuzalisha chakula kingi kiasi hiki hapa nchini? kwa kilimo kipi? cha powertiller? ni hiki hiki cha kutegemea mvua? cha mapeasant. Unga wa ugali Pinda kachemsha umeshindikana kushuka bei, mahindi yanauzwa kimagendo nje ya nchi ilhali muda wowote njaa itatangazwa kwa baadhi ya mikoa, Tabora wamesha onyesha wasiwasi wao. Sasa basi kwa juhudi zipi za serikali tunaweza kuuza mitani yoote hiyo ya mahindi nje?

  Tena ikiongezeka kwa malaki, kutoka tani 200,000 hadi tani 500,000 kwa muda mfupi tuu, serikali imeanzisha wapi mashamba mapya au wamejenga wapi mabwawa ya kuhifadhia maji ya kumwagilia? Hiki ndo tuliambiwa raisi anaongea na lile shabiki la ushoga huko Davos, manake maghembi nae alikuwepo kwenye msafara. Hawa WFP watasaidia nini katika maendeleo ya kilimo hapa nchini?

  Wataruhusu ruzuku ya mafuta kwa matreka yatakayolima mahekari ya ardhi? Ruzuku ya kweli ya mbolea na pembejeo muhimu? soko la uhakika WFP sio ishu hata kenya ni soko la uhakika, karamoja Uganda ni soko la uhakika, soko la ndani nim la uhakika, mi nadhani huyu Profesa hajui anachofanya ni kuhangaika kujida tunaweza wakati hatuwezi, hii misifa inatusaidia nini. Tunamuuzia chakula nani?

  Hapa nymbani kimetosha? Mbona hakishuki bei? mvua akikosekana tuu njaa, tusidanganyane Prof. Wadau huu si uongo huu?:A S embarassed:
   
Loading...