TZ Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Kama ulikua haujui ni wakati wako sasa wa kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya chaguzi mbalimbali za Tanzania. Nchi yetu inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post).

Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 35 F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Katika hili hakuna miujiza, kama wewe ni mgombea wingi wa kura zako halali kuliko wagombea wengine unaochuana nao utakupa ridhaa ya kutangazwa na Tume kuwa mshindi. Pia ni vema tukakumbuka kuwa Chaguzi za Tanzania zinasimamiwa na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia; -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
  2. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya 1985) Sura ya 343
  3. Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Na. 4 ya 1979) Sura ya 292
  4. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya (Na. 7 ya 1982) Sura ya 287
  5. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji ( Na. 8 ya 1982) Sura ya 288
  6. Sheria ya gharama za Uchaguzi
  7. Sheria ya Uraia Na 6 ya 1995
Nawatakia siku njema.
 
Aina hii ya uchaguzi inaitwa "Simple majority" wengi wape tofauti na Kenya wao" majority" maana yake lazima upate zaidi ya nusu ya kura zote (50% +1).
 
Aina hii ya uchaguzi inaitwa "Simple majority" wengi wape tofauti na Kenya wao" majority" maana yake lazima upate zaidi ya nusu ya kura zote (50% +1).

ha ha ha we wawapi nao wajifunze kwetu na hizo asilimia zao vurugu mtindo mmoja,
Uchaguzi wa TZ mwaka 2015 Vyama 8 ndo vinaonekana vilikua na mchuano

  1. ACT mgombea wake Kura 98,763
  2. ADC alipata kura 66,049
  3. CCM mgombea alipata kura 8,882,935
  4. CHADEMA alipata kura 6,072,848
  5. CHAUMA kura 49,256
  6. NRA kura 8,028
  7. TLP alipata Kura 8,198 na
  8. UPDP mgombea wao kura 7,785
Kwa akili yako wewe hapo unaona mgombea wa chama gani ni mshindi?
 
Pigo kwa Bavicha sidhani kama hujua hili..

Nadhani Mwenyekiti wa CCM haijui hii Sheria maana amewapiga Mkwara wakurugenzi waliowatangaza wapinzani kushinda uchaguzi.Muanze kumuelimisha huyu kwanaza ndipo mje kwa wapinzania.
 
Soma vizuri andiko, mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko wagombea wote anatangazwa na Tume kuwa mshindi Full stop

Hujanijibu bado,Kupitia alichosema Mwenyekiti wako au hajui sheria?? na Kupitia senetensi yako kwamba mwenye haki ya kutangaza matokeo ni Mkurugezi na yule aliyetangazwa ndiyo mshindi.

Tumeona majimbo mengi wapinzani walishinda aliyetangazwa ni aliyeshindwa,na mpaka kesi nyingine Hakimu kaomba radhi kwamba wasameheane na wasilipe gharama za kesi sababu Mkurugenzi alitangaza aliyeshindwa.

Jibu swali hivyo ukitangazwa hata kama hujashinda ndiyo mshindi??Maana umetangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye kwa asilimi 100 ni kada wa CCM
 
Sheria?? mara mwenyekiti wako?? mbona unaenda mbele na kurudi nyuma??????

Mwenyekiti wako wa CCM amewashangaa wakurugenzi mnaowalipa mishara kwa kutumia kodi zetu,wanaopewa posho na magari pamoja na ulizni kwa kodi zetu kwanini watangaze wapinzani wameshinda UCHAGUZI??Na akawauliza kama wanaakili kweli.Sasa swali langu ni kweli mshindi nidye anayetangazwa au ni mgombea mwenye chama cha mkurugenzi au Mwenyekiti wako wa CCM hajui sheria za uchaguzi??
 
Kama ulikua haujui ni wakati wako sasa wa kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya chaguzi mbalimbali za Tanzania. Nchi yetu inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post).

Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 35 F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Katika hili hakuna miujiza, kama wewe ni mgombea wingi wa kula zako halali kuliko wagombea wengine unaochuana nao utakupa ridhaa ya kutangazwa na Tume kuwa mshindi. Pia ni vema tukakumbuka kuwa Chaguzi za Tanzania zinasimamiwa na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia; -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
  2. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya 1985) Sura ya 343
  3. Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Na. 4 ya 1979) Sura ya 292
  4. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya (Na. 7 ya 1982) Sura ya 287
  5. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji ( Na. 8 ya 1982) Sura ya 288
  6. Sheria ya gharama za Uchaguzi
  7. Sheria ya Uraia Na 6 ya 1995
Nawatakia siku njema.
unawaandaa watu kwa uchaguzi wa keshokutwa !! (2020)
 
Back
Top Bottom