TZ Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi

Ukweli humuweka mtu kuwa huru,ni kweli lakini Tanzania hatuna uhuru tena.Umechukuliwa na Mwenyekiti wenu wa Chama Cha Mabwepande

Facts and figures zakae sawa mkuu, Sijui kama kwenye Orodha ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuna Chama cha Mabwepande let be serious tunapojadili issues!
 
1+1= 2 sio 11 hesabu hazina ubabe!
Nadhani ulikuwa unaangalia luninga kipindi lubuva akitangaza matokeo. Idadi ya wapigaji mgawanyo na asilimia. Je takwimu zilikuwa sawa? Kama siyo ndiyo ubabe wenyewe. Haiwezekani mwenye kura nyingi awe na asilimia ndogo. Haiwezekani kura zizidi wapiga kura
 
Nadhani ulikuwa unaangalia luninga kipindi lubuva akitangaza matokeo. Idadi ya wapigaji mgawanyo na asilimia. Je takwimu zilikuwa sawa? Kama siyo ndiyo ubabe wenyewe. Haiwezekani mwenye kura nyingi awe na asilimia ndogo. Haiwezekani kura zizidi wapiga kura

Uzuri kila Chama cha Siasa kilikua na nakala za matokeo yake yote ya Udiwani, Ubunge na Urais kuanzia ngazi ya Kata, jimbo hadi Taifa. Pia kila Chama kilikua na Mawakala katika vituo vyote nchi nzima. Waliokua na malalamiko walikwenda Mahakamani kupata ufumbuzi na haki ilitendeka kwa pande zote ni kwa vyama vyote 8 vilivyokuwa na wagombea sio vyama vya upinzani tu vilikua na malalamiko hata CCM walikua na malalamiko na walienda Mahakamani angalia Kesi ya Mhe. Esther Bulaya na Steven Wasira pia angalia jimbo la Tanga mjia aliyeshindwa Omari Nundu (CCM) Vs Mhe. Cassim Mbarouk wa CUF aliyeshinda nafasi ya Ubunge.
 
Let's say katika uchanguzi wa mwaka 2020, kutakuwa na wagombea 6 kutoka CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, UDP na ACT-wazalendo

MATOKEO
1.CCM 35%
2.CHADEMA 25%
3.CUF 15%
4.ACT 10%
5.NCCR-MAGEUZI 7.5%
6.UDP7.5%

Hivi kweli hapa msindi atakua CCM? Jibu ni NDIO kulingana na katiba yetu, na CCM watashangilia na kuimba "hiyenaa hiyenaa CCM numbarii wani" na mshindi wa urais atasema tumewashinda kwa kishindo cha sunami. Kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Katiba yetu inavyo sema mradi umewashinda wenzako kwa kura halali (Simple majority) utatangwazwa mshindi. Hii ni hatari sana sana kwa uhai wa taifa letu, hali hii inaweza ikalitumbukiza taifa kwenye machafuko makubwa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Tuombe kwa mola haya yasitokee, na tunaweza kuyakwepa haya kwa kubadilisha katiba na kuweka mshindi lazima apate 50% +1%. Hapa kutakua na uhalali wa ushindi, kwa sababu mshindi atakua amechanguliwa na watanzania zaidi ya nusu.
Au vyama kufanya muungano (coalition) e.g CCM na 35% ambayo imepata kura nyingi lakini hajavuka threshold kutafuta chama au vyama rafiki kama UDP 7.5% na CUF ya Lipumba 15% na kupata jumla ya 35%+7.5%+15%=57.5% hii ni zaidi ya 50%+1% na kufanya coalition goverment (My take kwa sababu CCM wamelewa madaraka hawawezi kufanya hivi, kwani wanaamini wao ndio wenye hati miliki ya nchi hii au wamekabithiwa na mola wetu kuitawala Tanzania hadi milele). Mimi ningewashauri wasome historia na wafungue macho kuangalia alama za nyakati.
Muhimu sana tukubali matokeo ya Urais yakapingwa mahakamani, hii itawafanya ambao hawakurithika na matokeo kama yalivyotangazwa na tume ya uchaguzi kwenda mahakamani kudai haki zao, kuliko kwenda mabarabarani au msituni.
Nchi zote zilizostaarabika duniani zinafuata kati ya njia moja au zote nilizo zitaja hapo juu. Njia tunayotembelea sisi wa Tanzania imelazimishwa na CCM ilikuihakikishia usindi wa milele, lakini hawajui hii nikama "a timing bomb" litakuja kulipuka tu siku moja. Tuombe mungu yasitokee uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Matokeo ya Urais yatapingajwe Mahakamani? na nani wa kuyapinga wakati ameshindwa uchaguzi?
 
Soma vizuri Sheria za nchi yako zinazosimamia masuala mbalimbali utaelewa tu. Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa Sura 292 , Sehemu ya uteuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi na wafanyakazi wengine 7.-(1) Inaeleza kuwa Kwa madhumuni ya Uchaguzi wowote utakaofanyika chini ya Sheria hii kila Mkurugenzi wa jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya atakua Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo inapofika wakati wa Uchaguzi.

Wakurugenzi hawa kabla ya kutekeleza majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanakula Kiapo cha kujitoa kusema wao sio wanachama wa chama chochote cha Siasa na wanapokiuka kiapo sheria iko wazi ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani. Pale ambapo wananchi wanapeleka ushahidi kwamba msimamizi huyo kwa mujibu wa cheo chake (MKURUGENZI) hawezi kutekeleza majukumu ya Uchaguzi anawekwa pembeni na mtu mwingine huteuliwa kutekeleza jukumu hilo imeshafanyika Moshi, Manyara, Tanga na maeneo mengine baada ya wananchi na wadau kupeleka uthibitisho wa Wakurugenzi kushindwa kusimamia majukumu yao!
Tatizo unasema jingine na huku yanafanyika mengine...Kwanini Wakurugenzi wasimamie Uchaguzi wakati wao sio watumishi wa Tume ya Uchaguzi? Am not disobeying the law but opposing an oppressive law
 
Soma vizuri andiko, mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko wagombea wote anatangazwa na Tume kuwa mshindi Full stop
mku kuna tofauti ya mshindi na mshindi halali........ kushinda na kutangazwa ni vitu viwili tofauti nlikuwepo jimbo la mbagala 2015 ile wiki baada ya uchaguzi nakumbuka mshindi hakutangazwa hadi walipoconsult kwa WAKUBWA na indeed wakamtangaza MSHINDI wao wa ccm na yule wa cuf akaambiwa aende mahakamani full stop!!!!!

so usiseme tu mwenye kura nyingi hutangazwa mshindi wwe sema huwa Nec Inaamua nani imtangaze mshindi ila sio wananchi
 
Uzuri kila Chama cha Siasa kilikua na nakala za matokeo yake yote ya Udiwani, Ubunge na Urais kuanzia ngazi ya Kata, jimbo hadi Taifa. Pia kila Chama kilikua na Mawakala katika vituo vyote nchi nzima. Waliokua na malalamiko walikwenda Mahakamani kupata ufumbuzi na haki ilitendeka kwa pande zote ni kwa vyama vyote 8 vilivyokuwa na wagombea sio vyama vya upinzani tu vilikua na malalamiko hata CCM walikua na malalamiko na walienda Mahakamani angalia Kesi ya Mhe. Esther Bulaya na Steven Wasira pia angalia jimbo la Tanga mjia aliyeshindwa Omari Nundu (CCM) Vs Mhe. Cassim Mbarouk wa CUF aliyeshinda nafasi ya Ubunge.
Hahhahhahaha nyie jamaa bwana hao wapinzani walishinda kesi coz walikuwa kwenye defensive side na kwa mazingira ya kawaida tu mpinzani ni ngumu sana kuiba kura maana hta kituo cha kuhesabia kura tu lazma azuiwe getini ila waccm wanaingiaga.... pia kuhusu hizo nakala kina naftali na wenje na kafulila wote walikuwa nazo ila walipata nni mwishoni??? nyie ccm mnajua kabxa mahakamani hamuwezi shindwa kesi ndio maana huwa mnapora kma kule kyerwa au kwela afu mnasema tu NENDA MAHAKAMANI mkijua hakuna litakalo tokea!!!!
 
Matokeo ya Urais yatapingajwe Mahakamani? na nani wa kuyapinga wakati ameshindwa uchaguzi?
Sasa kma mtu analalamika kaibiwa kma seif au slaa wataenda wapi kudai haki zao na kuweka ushahidi!!! kila cku ccm mnasemaga wapinzani wanalalamika wameibiwa kura ssa kwanni msiruhusu twende mahakamani ili mtuumbue huko na tujue nani mkweli na nani muongo
 
Back
Top Bottom