TZ Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi

kuna Sheria mpa ya magufuli ambayo akikuteua kuwa mkurugendi wa wilaya au Tume ya uchaguzi, inatakiwa kwenye uchaguzi wowote umtangaze mgombea wa CCM hata kama ameshindwa. "mkurugenzi tunakupa gari na ulinzi pamoja na posho na bado unatangaza wapinzani wameshinda" mwisho wa kunukuu
 
Mwenyekiti wako wa CCM amewashangaa wakurugenzi mnaowalipa mishara kwa kutumia kodi zetu,wanaopewa posho na magari pamoja na ulizni kwa kodi zetu kwanini watangaze wapinzani wameshinda UCHAGUZI??Na akawauliza kama wanaakili kweli.Sasa swali langu ni kweli mshindi nidye anayetangazwa au ni mgombea mwenye chama cha mkurugenzi au Mwenyekiti wako wa CCM hajui sheria za uchaguzi??
Ni kweli mkuu katamka hvyo?
 
Hujanijibu bado,Kupitia alichosema Mwenyekiti wako au hajui sheria?? na Kupitia senetensi yako kwamba mwenye haki ya kutangaza matokeo ni Mkurugezi na yule aliyetangazwa ndiyo mshindi.

Tumeona majimbo mengi wapinzani walishinda aliyetangazwa ni aliyeshindwa,na mpaka kesi nyingine Hakimu kaomba radhi kwamba wasameheane na wasilipe gharama za kesi sababu Mkurugenzi alitangaza aliyeshindwa.

Jibu swali hivyo ukitangazwa hata kama hujashinda ndiyo mshindi??Maana umetangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye kwa asilimi 100 ni kada wa CCM

Sio vibaya ukatutajia hayo majimbo mengi
 
Mkurugenzi sio mtumishi wa NEC sasa inakuaje atangaze au kushiriki katika Uchaguzi? Huu ni mpango pia wa kuiba ushindi wa watu tunayo mifano mingi tu
 
Let's say katika uchanguzi wa mwaka 2020, kutakuwa na wagombea 6 kutoka CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, UDP na ACT-wazalendo

MATOKEO
1.CCM 35%
2.CHADEMA 25%
3.CUF 15%
4.ACT 10%
5.NCCR-MAGEUZI 7.5%
6.UDP7.5%

Hivi kweli hapa msindi atakua CCM? Jibu ni NDIO kulingana na katiba yetu, na CCM watashangilia na kuimba "hiyenaa hiyenaa CCM numbarii wani" na mshindi wa urais atasema tumewashinda kwa kishindo cha sunami. Kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Katiba yetu inavyo sema mradi umewashinda wenzako kwa kura halali (Simple majority) utatangwazwa mshindi. Hii ni hatari sana sana kwa uhai wa taifa letu, hali hii inaweza ikalitumbukiza taifa kwenye machafuko makubwa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Tuombe kwa mola haya yasitokee, na tunaweza kuyakwepa haya kwa kubadilisha katiba na kuweka mshindi lazima apate 50% +1%. Hapa kutakua na uhalali wa ushindi, kwa sababu mshindi atakua amechanguliwa na watanzania zaidi ya nusu.
Au vyama kufanya muungano (coalition) e.g CCM na 35% ambayo imepata kura nyingi lakini hajavuka threshold kutafuta chama au vyama rafiki kama UDP 7.5% na CUF ya Lipumba 15% na kupata jumla ya 35%+7.5%+15%=57.5% hii ni zaidi ya 50%+1% na kufanya coalition goverment (My take kwa sababu CCM wamelewa madaraka hawawezi kufanya hivi, kwani wanaamini wao ndio wenye hati miliki ya nchi hii au wamekabithiwa na mola wetu kuitawala Tanzania hadi milele). Mimi ningewashauri wasome historia na wafungue macho kuangalia alama za nyakati.
Muhimu sana tukubali matokeo ya Urais yakapingwa mahakamani, hii itawafanya ambao hawakurithika na matokeo kama yalivyotangazwa na tume ya uchaguzi kwenda mahakamani kudai haki zao, kuliko kwenda mabarabarani au msituni.
Nchi zote zilizostaarabika duniani zinafuata kati ya njia moja au zote nilizo zitaja hapo juu. Njia tunayotembelea sisi wa Tanzania imelazimishwa na CCM ilikuihakikishia usindi wa milele, lakini hawajui hii nikama "a timing bomb" litakuja kulipuka tu siku moja. Tuombe mungu yasitokee uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
 
Kama ulikua haujui ni wakati wako sasa wa kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya chaguzi mbalimbali za Tanzania. Nchi yetu inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post).

Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 35 F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Katika hili hakuna miujiza, kama wewe ni mgombea wingi wa kura zako halali kuliko wagombea wengine unaochuana nao utakupa ridhaa ya kutangazwa na Tume kuwa mshindi. Pia ni vema tukakumbuka kuwa Chaguzi za Tanzania zinasimamiwa na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia; -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
  2. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya 1985) Sura ya 343
  3. Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Na. 4 ya 1979) Sura ya 292
  4. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya (Na. 7 ya 1982) Sura ya 287
  5. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji ( Na. 8 ya 1982) Sura ya 288
  6. Sheria ya gharama za Uchaguzi
  7. Sheria ya Uraia Na 6 ya 1995
Nawatakia siku njema.
Nani alikuambia kwamba ni lazima apate nyingi kuliko wenzake? Unajua ni sababu IPI inayofanya matokeo ya urais yasipingwe mahakamani?
 
Nani alikuambia kwamba ni lazima apate nyingi kuliko wenzake? Unajua ni sababu IPI inayofanya matokeo ya urais yasipingwe mahakamani?

Sio mimi ninayesema ni KATIBA nenda kasome uielewe! utajua kwa nini matokeo hayapingwi.
 
Mkurugenzi sio mtumishi wa NEC sasa inakuaje atangaze au kushiriki katika Uchaguzi? Huu ni mpango pia wa kuiba ushindi wa watu tunayo mifano mingi tu

Soma vizuri Sheria za nchi yako zinazosimamia masuala mbalimbali utaelewa tu. Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa Sura 292 , Sehemu ya uteuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi na wafanyakazi wengine 7.-(1) Inaeleza kuwa Kwa madhumuni ya Uchaguzi wowote utakaofanyika chini ya Sheria hii kila Mkurugenzi wa jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya atakua Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo inapofika wakati wa Uchaguzi.

Wakurugenzi hawa kabla ya kutekeleza majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanakula Kiapo cha kujitoa kusema wao sio wanachama wa chama chochote cha Siasa na wanapokiuka kiapo sheria iko wazi ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani. Pale ambapo wananchi wanapeleka ushahidi kwamba msimamizi huyo kwa mujibu wa cheo chake (MKURUGENZI) hawezi kutekeleza majukumu ya Uchaguzi anawekwa pembeni na mtu mwingine huteuliwa kutekeleza jukumu hilo imeshafanyika Moshi, Manyara, Tanga na maeneo mengine baada ya wananchi na wadau kupeleka uthibitisho wa Wakurugenzi kushindwa kusimamia majukumu yao!
 
Kama ulikua haujui ni wakati wako sasa wa kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya chaguzi mbalimbali za Tanzania. Nchi yetu inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post).

Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 35 F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Katika hili hakuna miujiza, kama wewe ni mgombea wingi wa kura zako halali kuliko wagombea wengine unaochuana nao utakupa ridhaa ya kutangazwa na Tume kuwa mshindi. Pia ni vema tukakumbuka kuwa Chaguzi za Tanzania zinasimamiwa na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia; -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
  2. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya 1985) Sura ya 343
  3. Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Na. 4 ya 1979) Sura ya 292
  4. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya (Na. 7 ya 1982) Sura ya 287
  5. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji ( Na. 8 ya 1982) Sura ya 288
  6. Sheria ya gharama za Uchaguzi
  7. Sheria ya Uraia Na 6 ya 1995
Nawatakia siku njema.
Kwa sheria na hakk ni sawa ila kwa ubabe na unafiki si sawa. Ikiwa 1+1=2 ila unaambiwa jibu lazima liwe 11 utajibuje
 
Back
Top Bottom