Ndugu zetu wanazidi kufa yote shauri ya utajiri kwa njia ya mkato, hizi kesi kwa watanzania katika kipindi cha hivi karibuni zimezidi mno.
Serikali na Media inabidi zitumie muda zaidi kuelimisha jamii juu ya hili tatizo.
Laiti ingelikuwa statistics za wasafirishaji wote wa Kitanzania waliokufa kwa staili hii zitapatikana, kuanzia Bongo, India, Iran, Pakistan, Afghanistan, UK, USA, Italy, Greece,Bulgaria, Turkey,Holland, Switzerland, South Africa, Sweden, Denmark, Dubai,Thailand, China, Brazil nk naamini baadhi ya vijana wangelisita kuingia huko. Hizi sehemu zote haya matukio yametokea lakini tunadharau kwa vile ni Aibu na tunajidanganya kwamba ni vijana wachache kwa hio sio tatizo kubwa!
Ukweli hili tatizo ni kubwa sana katika jamii yetu, nadhani hivi sasa sisi tuko nyuma ya Wanaijeria tu. Drug Barons wa kweli kama Russian mafias na Colombians hawasafirishi vikete sijui tumboni kama hawa wajinga. Sijui ni ukosefu wa kuelewa madhara yake ama ndio umasikini?