Twendeni na Ally Mayay kwenye urais wa TFF

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Mimi napenda sana soka. Kuna uchaguzi wa TFF mwezi Agosti, 2025. Nawashauri wajumbe watakaomchagua Rais wa TFF wamchague Ally Mayay ili awe Rais kwa kipindi kijacho. Rais anayemaliza muda wake amevuruga sana soka la Tanzania, na anatuhumiwa kwa upendeleo na ameshindwa kusimamia fedha za TFF mpaka timu kadhaa mpaka sasa wanaidai TFF malipo yao. Rais wa sasa hafai na asichaguliwe katika nafasi ya Rais wa TFF.
 
Mfanyakazi wa sehemu nyeti unapeleka kwenye mpira hatari sana
 
Mimi napenda sana soka. Kuna uchaguzi wa TFF mwezi Agosti, 2025. Nawashauri wajumbe watakaomchagua Rais wa TFF wamchague Ally Mayay ili awe Rais kwa kipindi kijacho. Rais anayemaliza muda wake amevuruga sana soka la Tanzania, na anatuhumiwa kwa upendeleo na ameshindwa kusimamia fedha za TFF mpaka timu kadhaa mpaka sasa wanaidai TFF malipo yao. Rais wa sasa hafai na asichaguliwe katika nafasi ya Rais wa TFF.

Huu uchaguzi unafanyika mkoa gani? kwanini? ukimaliza kujibu utakuwa umepata jibu kuu. Kwa njaa za wajumbe, Ally hana uwezo wa kushinda.
 
WELLS CARRY-A ameshahonga wajumbe kila mkoa ili wamu endorse na amewapiga mkwara wasije wakafanya endorsement kwa mgombea mwingine

Huu uchaguzi wanaenda kumuidhinisha tu sidhani kama atapata mchuano mkali sana JAPO BINAFSI NAHITAJI MABADILIKO PALE TFF
 
Naona mnajisahaulisha ..Ally Mayay alishindwa kwa kura nyingi uchaguzi uliofanyika Dodoma👇👇

Wallace Karia ni wa kupelekwa mahakamani na kufungwa kutokana na matumizi yake mabaya ya madaraka. Na siyo wa kuendelea kupewa nafasi nyingine ya kujigeuza kuwa rais wa milele na pia mungu mtu paleTFF.
 
Afu kwann TFF haijawah kuongozaa na wachezaji wa mpira wa zamani.?!
Eto'o ni rais wa fecafoo ambayo ni TFF ya kule cameroon.

Hapa sasa vigezo vimewekewa mafigisu ili watu wagwaye....si wamejua pana ulaji...huingiliwi....hufukuziki.....hukaguliwi.....

Hamna lolote bwana, hapo hata wewe unaweza...kwani Eto'o alipata mashahada lini....

Ndo yaleyale ya CCM, kuamini kwamba msomi yeyote asiye mtumishi wa umma hana uwezo wa kusimamia uchaguzi kwa ufanisi...
 
Huu uchaguzi unafanyika mkoa gani? kwanini? ukimaliza kujibu utakuwa umepata jibu kuu. Kwa njaa za wajumbe, Ally hana uwezo wa kushinda.
Hiyo ni project ya Serikali. Nikukumbushe tuu Ndolanga alikuwa na nguvu kuliko kiongozi yeyote wa FAT na TFF ya sasa lakini pale Serikali ilipomchoka alitoka kwa kura hata baada ya kununua wajumbe wote.
 
WELLS CARRY-A ameshahonga wajumbe kila mkoa ili wamu endorse na amewapiga mkwara wasije wakafanya endorsement kwa mgombea mwingine

Huu uchaguzi wanaenda kumuidhinisha tu sidhani kama atapata mchuano mkali sana JAPO BINAFSI NAHITAJI MABADILIKO PALE TFF
Hata Ndolanga alifanya hivyo hivyo,Serikali ikawapa kazi maalumu wakuu wa mikoa na wilaya kufanya kazi yake,mwisho Ndolanga alipigwa chini kwa kura za wazi kabisa.
 
Sioni kama Karia amefikia hatua ya kuchukiwa kama ilivyokuwa kwa Ndolanga ambaye alikutwa na kesi kadhaa za ufisadi, BMT wakamshindwa, ndipo ikabidi sasa itumike nguvu.
 
Hakuna wakumshinda Karia, akiwa kwenye kinyang'anyiro. Inabidi kumpa shinikizo asigombee!
Hivi vyama vya mpira ni kama cult flani hivi, incumbents wanajenga himaya hawawezi ng'oka. Refer, Ndolanga, Malinzi, Wambura
 
mayai atatufaa zaidi na akizungua tunayagonga tunayakaanga tunayala
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom