Twende polepole

Twende polepole

kunowa

Member
Joined
Oct 30, 2024
Posts
49
Reaction score
61
Kaka umesema upo CCM tangu 2000. Hebu tueleze uchaguzi wa mwaka 2010 CCM ilitoa form ngapi za uraisi? Mwaka 2020 zilizalishwa form ngapi? Mbona hukuachia ngazi?.

Lakini umesema mchakato wa katiba mpya "wahuni'' walivuruga maoni ya wananchi, wewe na walipanga pia kuhujumu uchaguzi mkuu, wewe na wenzio mukaamua kwenda kupambana dhidi ya wahuni, na kweli mukashinda.

Lakini cha kushangaza ninyi waungwana muliposhinda mukasema katiba mpya sio agenda yenu. Sasa wahuni sio nyie kweli?

Polepole mbona unaongea tofauti na dhamira iliyopo moyoni kwako?

Muda utaongea!
 
Anawaada wajinga wachachee ila pole pole ndio yule yule wa CCM ,Hana mabadiliko yyt na hkn mabadiliko yyt atayeleta baada yakusema anayoyasemea ss 🤔🤔
 
Jamaa hana akili kabisa, alifaa kuwa balozi wa nyumba kumi, taifa limepoteza fedha kupeleka mzoga mpaka Cuba
 
Kuna rumors ziliwahikuwepo humu kuwa watu walitaka wawe maraisi wa Kisumu wao na genge Lao wakaandaa pesa nyingi kutimiza hilo jambo, baada ya Kiongozi kufa hili kundi halikufa na bado lilibaki na ndoto zilezile. Sasa naona wajanja wenzao wakausoma mchezo wakaja na form moja. Form moja ilikuwa KO kwao!
 
Jamaa hana akili kabisa, alifaa kuwa balozi wa nyumba kumi
Hii ikigeuzwa upande wa pili unakuwa unakata tawi ulilokanyaga!!! Unakumbuka utaratibu wa kupata na kumteua mtu awe Balozi? Kama kumbukumbu zipo chutama Sasa, watoto wanakaribia.
 
Kaka umesema upo CCM tangu 2000. Hebu tueleze uchaguzi wa mwaka 2010 CCM ilitoa form ngapi za uraisi? Mwaka 2020 zilizalishwa form ngapi? Mbona hukuachia ngazi?. Lakini umesema mchakato wa katiba mpya "wahuni'' walivuruga maoni ya wananchi, wewe na walipanga pia kuhujumu uchaguzi mkuu, wewe na wenzio mukaamua kwenda kupambana dhidi ya wahuni, na kweli mukashinda. Lakini cha kushangaza ninyi waungwana muliposhinda mukasema katiba mpya sio agenda yenu. Sasa wahuni sio nyie kweli? Pole pole mbona unaongea tofauti na dhamira iliyopo moyoni kwako?
Muda utaongea!
Unaweza kukasiriki na kumtukana Polepole humu kisha forum ikakufungia.Polepole anatuona sisi kama hamnazo na kumbukumbu hatuna
 
Kaka umesema upo CCM tangu 2000. Hebu tueleze uchaguzi wa mwaka 2010 CCM ilitoa form ngapi za uraisi? Mwaka 2020 zilizalishwa form ngapi? Mbona hukuachia ngazi?. Lakini umesema mchakato wa katiba mpya "wahuni'' walivuruga maoni ya wananchi, wewe na walipanga pia kuhujumu uchaguzi mkuu, wewe na wenzio mukaamua kwenda kupambana dhidi ya wahuni, na kweli mukashinda. Lakini cha kushangaza ninyi waungwana muliposhinda mukasema katiba mpya sio agenda yenu. Sasa wahuni sio nyie kweli? Pole pole mbona unaongea tofauti na dhamira iliyopo moyoni kwako?
Muda utaongea!
Samia amekua Rais baada ya Magufuli kufariki...Hivyo sio Rais wa Awamu ya Tano
Mwaka huu ndo tungepata Rais wa Awamu ya sita...Hivyo CCM wangeandaa mgombea wao kwa kumpitisha katika vikao halali ikiwemo kura za maoni.

Samia kama anajiamini angeruhusu kuwepo kwa kura za maoni mwaka huu.

Halafu 2030 tungesema busara zitumike apite bila kupingwa
 
Back
Top Bottom