Twende na ACT Wazalendo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
628
1,561
TWENDE NA ACT WAZALENDO.
1
Juwa ei sii tii, ni chama cha Wazalendo
Chapigania jamii, kwa kauli na vitendo,
Uchao hakitulii, kazi kunadi upendo
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
2
Mlengo kati kushoto, ndiyo itikadi yake,
Taifa yake mapato, kwa uzuri yatumike,
Pasiwepo na uzito, huduma kote zifike,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
3
Vimbegu vya ujamaa, pamwe kujitegemea,
Chamani zimezagaa, punde zitajiotea,
Popote takapokaa, uone zilivyomea.
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
4
Chama kinayauhisha, yaliyofutwa kwa raba,
Na tena kinatukumbusha, yaliyozikwa Zanziba,
Ni Azmio la Arusha, pengole hatujaziba,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
5
Kwa hili hapana shaka, tunastahili adhaba,
Nyerere alitutaka, haraka tufanye toba,
Werevu tulojivika, kila ndia sasa miba,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
6
Hichi chama mabadala, kwa vyama vya upinzani,
Pia na kwa chama dola, kilicho' madarakani,
Chama hakita tawala, kitashika usukani,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
7
Chama kina mikakati, si chama cha matukio,
Muda mrefu na kati, na huu tulio nao,
Hichi chama sikiwati, kwani cha maendeleo,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
8
Zitto ndiye kiongozi, Mama Anna mwenyekiti,
Lenda salama jahazi, mawimbi yachanwa kati,
Kusi ama kaskazi, usukani hauwati,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
9
Kwa vijana tumefuzu, waongoza bila tabu,
Tunaye Patrick Mbozu, Edna naye Shaibu,
Kwa kazi ni makauzu, kutamba tuna sababu,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.
10
Mwisho ndimi Rangimoto, mwanachama kindakindaki,
Leo ninatowa wito, mjiunge chama hiki,
Pamoja tushike fito, tujenge nchi ya haki,
Jiunge sasa ACT, tujenge taifa letu.

20 February 2017 Jumatatu.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 Morogoro.
 
Back
Top Bottom