Twakupongeza (CAG) Prof. Mussa Juma Assad

Mamabolo

Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
32
Reaction score
8
Kwa mabadiliko ya kitaasisi uliyoyasimamia kwa kipindi kifupi kwenye ofisi yako hadi sasa, sisi tuliokuwa na shauku hiyo tunakupongeza. Endelea kufanya kazi kwa utalaam na weledi wako katika discourse yako ya kusaidia usimamizi thabiti wa rasilimali za walipa kodi wetu.

Tunakushukuru sana pia kwa uhamisho wa hivi karibuni wa waliokuwa wapinga mabadiliko katika ofisi yako imara. Watumishi wajue kuwa utumishi wa umma ni jambo ambalo linasimamiwa na serikali na siyo watu binafsi. Endelea kuvunja mifumo mibovu iliyojengeka katika taasisi zetu.

Prof Assad, fanya kazi bwana watanzania wameona mafanikio yako tayari hata kama wapo wavivu wachache wasiopenda mabadiliko na kasi kubwa ya utendaji.
 
Kwa mabadiliko ya kitaasisi uliyoyasimamia kwa kipindi kifupi kwenye ofisi yako hadi sasa, sisi tuliokuwa na shauku hiyo tunakupongeza. Endelea kufanya kazi kwa utalaam na weledi wako katika discourse yako ya kusaidia usimamizi thabiti wa rasilimali za walipa kodi wetu.

Tunakushukuru sana pia kwa uhamisho wa hivi karibuni wa waliokuwa wapinga mabadiliko katika ofisi yako imara. Watumishi wajue kuwa utumishi wa umma ni jambo ambalo linasimamiwa na serikali na siyo watu binafsi. Endelea kuvunja mifumo mibovu iliyojengeka katika taasisi zetu.

Prof Assad, fanya kazi bwana watanzania wameona mafanikio yako tayari hata kama wapo wavivu wachache wasiopenda mabadiliko na kasi kubwa ya utendaji.[/QUOTE

Hongera zake prof... ila hilo jina lako bana aagh!!
 
Pro. huyu alimtaja Magufuri kama Fisadi papa, kwa Kuuza nyumba za serikali pamoja naUfisadi wa karibu Bili. 576 kwenye wizara ya Miundo mbinu.

Pia juzi PPRA imetoa Upotevu wa Sh. Mili 976.3 kwa kuwalipa wakandarasi hewa.
 
...baada ya kipindi kirefu kupita, pamoja na yote mnayoyasema juu ya JK, ukweli utajulikana amejitahidi sana kutengeneza mabadiliko na kuwa fair kwa pande nyingi. Tatizo lilikuwa ni kila anayepewa anarudia yale yale, ila taratibu wazalendo wanaanza kurudi kwenye system. Sio kipindi kirefu kama wao wanaosema "mtaisoma namba" na mtamuelewa tu JK baada ya kuona alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake, na wengine waendelee alipoishia
 
Hii nchi bwana,kama ufisadi wa namna I umefanyika kwenye wizara ya mfuatiliaji asiye na makandokando,hii ni hatari,bora ukawa wachukue I nchi wananchi wapate kunufaika na raslimali zao
 
....hili swala la uuzwaji wa nyumba, ilikuwa ni kuwakomesha hao wenzetu wa nje wenye mapesa yao, mzee BWM alisema "...kwa hiyo mimi ni raisi nitatoka hapa, hili eneo la oysterbay loote hatakuwepo mwafrika humu...." otherwise mnaopiga kelele kuhusu hili kwa sasa msingekuwa hata huko mijini. Anyways pamoja na nia nzuri ya BWM kuhusu swala hili, labda utekelezaji wake ulikuwa na shida, ila in the long term it is 100X better kupoteza hiyo USD 976.3 kwa sasa ila ardhi hiyo iko kwa watz kuliko kuwa tungeiweka mikononi mwa matajiri wachache. WTF is wrong with Tanzanians mkisaidiwa mnalalamika, mkiachwa kwenye level playing field you can't compete, you go again with complaining!

https://www.youtube.com/watch?v=LofQGOS0bCM
 
Shikamoo magodfather....unapewa maelekezo ufanyaje sio kwamba utumie taaluma na busara zako kufanya kazi za umma.

Hongera Prof. Assad...jitahidi kamwe kutoyumbishwa kwa sababu za kisiasa
 
mkuu wenye uelewa wetu tunaelewa alichofanya JK. lakini hao jamaa wa vidole juu wambeya kweli, wanajifanya hamnazo kabisa japokuwa wanaona kwa macho yao aliyoyafanya JK.

...baada ya kipindi kirefu kupita, pamoja na yote mnayoyasema juu ya JK, ukweli utajulikana amejitahidi sana kutengeneza mabadiliko na kuwa fair kwa pande nyingi. Tatizo lilikuwa ni kila anayepewa anarudia yale yale, ila taratibu wazalendo wanaanza kurudi kwenye system. Sio kipindi kirefu kama wao wanaosema "mtaisoma namba" na mtamuelewa tu JK baada ya kuona alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake, na wengine waendelee alipoishia
 
ukimpata mwislamu alie ishika dini ukampa kazi yako, lazima aifanye katika ubora ulio tukuka. Nampa hongera Pro.

Dr Dau amejishushia heshima yake kama Dr Miogo.
 
Pamoja na hongera kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi kifupi hebu kwa busara, hekima, utashi na uadilifu wake aende Manispaa ya Kinondoni akaisafishe kwani imejaa wizi na dhuluma za ajabu si kwa watumishi wake tu bali hata kwa raia tunaotaka huduma pale. Huwa najiuliza ni nani anayewalinda wezi hawa pale manispaa? Nyaraka zinanyofolewa kwenye mafaili ya watumishi hasa walimu kwa kuwa madai yao huliwa na wachache pale. Hebu asaidie hili ili kuleta ufanisi kama ulivyo kwenye halmashauri nyinginezo. Ni ombi lakini.
 
Pro. huyu alimtaja Magufuri kama Fisadi papa, kwa Kuuza nyumba za serikali pamoja naUfisadi wa karibu Bili. 576 kwenye wizara ya Miundo mbinu.

Pia juzi PPRA imetoa Upotevu wa Sh. Mili 976.3 kwa kuwalipa wakandarasi hewa.

Mambo mengine kwa uelewa wa kawaida yanaweza kukwaza lkn kama uko vizuri haisumbui kwani kwa muundo wa usimamizi wa fedha za umma (government financial management hierarchy) accounting officer ndiye mwenye dhamana yaani "doctrine of personal accountability" hivyo huwa hainiingii akilini jambo sensitive kama hili tukaishia kulijadili kisiasa wakati kimuundo wawajibikaji wapo na tunataka kulihalalisha kisiasa siasa tu.
 
ukimpata mwislamu alie ishika dini ukampa kazi yako, lazima aifanye katika ubora ulio tukuka. Nampa hongera Pro.

Dr Dau amejishushia heshima yake kama Dr Miogo.
kiukweli prof namkubali sana na kwa watu waelewa ni busara kumpongeza aliemteua kwa uwezo wa kulijua hilo na kwa dhana hiyo mteuzi si mshirika ufisadi kwani lazima angesheki sana kuteua, angalia hata mtangulizi wake utouh hakufanya mzaha ktk kazi. kwa nchi yetu nadhani tatizo bado lipo kwa wanasiasa wetu uelewa wao wao finyu sana kufikia hata kuwakataa watendaji bora wa serikali na hasa baada ya kupewa fedha kama tuonavyo leo mafisadi kugeuka mashujaa majukwaani na kwa jeuri ya wokovu bandia
 
Pro. huyu alimtaja Magufuri kama Fisadi papa, kwa Kuuza nyumba za serikali pamoja naUfisadi wa karibu Bili. 576 kwenye wizara ya Miundo mbinu.

Pia juzi PPRA imetoa Upotevu wa Sh. Mili 976.3 kwa kuwalipa wakandarasi hewa.
Harafu kuna viazi wanasema eti makomeo mwadilifu nyambafffffgg zao
 
....hili swala la uuzwaji wa nyumba, ilikuwa ni kuwakomesha hao wenzetu wa nje wenye mapesa yao, mzee BWM alisema "...kwa hiyo mimi ni raisi nitatoka hapa, hili eneo la oysterbay loote hatakuwepo mwafrika humu...." otherwise mnaopiga kelele kuhusu hili kwa sasa msingekuwa hata huko mijini. Anyways pamoja na nia nzuri ya BWM kuhusu swala hili, labda utekelezaji wake ulikuwa na shida, ila in the long term it is 100X better kupoteza hiyo USD 976.3 kwa sasa ila ardhi hiyo iko kwa watz kuliko kuwa tungeiweka mikononi mwa matajiri wachache. WTF is wrong with Tanzanians mkisaidiwa mnalalamika, mkiachwa kwenye level playing field you can't compete, you go again with complaining!

Hii ni laana kubwa inayotutafuna na itaendelea kututafuna. Kazi yetu kubwa ni kulalamika dhidi ya kila kitu. Nadhani ndiyo maana tumedelevelop thick lips kutokana na utaalam wetu wa kulalama kutwa kucha dhidi ya kila kitu.
 
Back
Top Bottom