twa shauriwa kuacha ukabila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

twa shauriwa kuacha ukabila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JosM, May 29, 2009.

 1. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nimeikuta hii kwenye mjadala mmoja huko kwenye net nikaona niiweke hapa mbele yenu
  huyu mtu anasema ni mkenya na alikuwa anachangia mada ya ukosefu wa umakini kwa wanasheria[hasa ofisi ya dpp]katika kuandaa mashtaka,mtu mmoja akaingiza mambo ya uchaguzi wa busanda na chadema, jamaa akaamua kutoa uvivu kwa dizaini hii hapa chini, kilichonifanya niiweke hapa ni hizo data zake pale chini jinsi tunavyoibiwa


  Watu wengine bwana mada inaelezea jambo lingine wao wanaelezea ujinga wa uchaguzi kule Busanda wa kununua shahada za wananchi.Ndugu hapu juu unapodai CHADEMA ni chama cha wachagga ina maana Dr Slaa na Zitto Kabe ni Wachagga?.Msipende kubeza viongozi ambao wanatetea mali za taifa kwa kuwa nyie tayari mnapata maisha bora.Kwa hiyo watu wa Kilimanjaro waliopo CCM wao sio Wachagga. Au unataka kutuambia CCM ni chama cha watu gani?.Mimi nilishawaambia Watanzania bila kubadili utawala nchi hii watoto wenu watachapwa bakora ndio wapata mlo wa mchana.Rais wa nchi masikini kabisa Duniani anafanya safari za Kenda nje ya nchi mara tisa kwa mwaka akiambatana na watu arobaini lakini wananchi wanakufa kwa njaa,na maradhi mnaona sawa tu.Toka Kibaki aingie madarakani amesafiri mara ngapi?.Mnachelelea tu nchi kuwa masikini huku mkiweke ukabila mbele kwa ajili ya wivu.Mimi ni mtu kutoka Kenya lakini kwa kuwa nimekulia Tanzania na naona Mateso mnayopata lazima niwe na huruma.Msipoamka Watanzania mtasababisha watoto na wajukuu wenu waishi maisha ya tabua sana.Waziri wa Kenya akikosea Wananchi au Wabunge wenzake haruhusiwi kuingia ukumbi wa Bunge nyie Mawaziri na Wabunge takribani wote ni waizi lakini wanaingia Bungeni kutetea masilahi yao mnaona swa tu.Poleni sana.Kumbukeni yule muimbaji wenu alisema siku huwa hazirudi nyuma.Mtakumbuka maneno yangi ninayowaambia majirani zangu.Kenya haturuhusu huu ujinga na ndio maana tunajitosheleza kwa mambo yale muhimu.
  Tanzania mmepata Uhuru wenu mbeleni sana nadhani 1961 lakini hadi leo mtu akipata ajali lazima apelekwe Kenyatta Hospital ni mambo ya aibu sana.Mko na mali mingi sana lakini mnawaachia wageni wanazihamisha wakisaidiana na viongozi wenu walafi.Acheni mambo ya Ukabila kwani ndiyo yametuletea sisi matatizo.Nionavyo mimi bila kuwa na Kiongozi toka kabila zenye maendeleo Tanzania mtafika karne ya 22 mkiwa mumeachiwa mashimo na wanyama wote watakuwa wako Ulaya.Kwa taarifa nilizonazo kuna Zoo kule Ulaya na Marekani kumejaa wanyama kutoka Tanzania.Fungua website hii hapa chini uone Tanzania ilivyoporwa mali nyingi na wageni [http://www.americazoo.com/animalsinthezoo.shtml]
  [http://nationalzoo.si.edu/Animals/PhotoGallery/AfricanSavanna/7.cfm]
  []] - Worldnews Network
  Toka lini hawa Wazungu wakawa na wanyama kutoka Serengeti,Mikumi na Ngorongoro tukiachilia Park zenu zingine zenye wanyama wazuri sana.Viongozi wenu watawamalizeni.Fungueni macho na masikio yenu.Madini ndio usiseme.Kama mlikuwa mnayachimba wenyewe Tanzania ingekuwa kama South Africa. Maduka ya Gemstone ulaya yamejaa madini toka Tanzania.
  [http://tanzanite-gemstone.com/history.php]
  []Internet Advertising Website Design Marketing Promotion by A1AWEB Daytona Beach Florida, A1AWEB.com
  []Giant Red Spinel Crystal Discovered in East Africa
  [http://www.thejewelryhut.com/html/gemstone_education-garnet.html]
  Mtabaki mnawabeza viongozi wa upinzani kumbe wao wana malengo mazuri.Hakuna Kiongozi aliye madarakani Tanzania ambaye hana shea kwenye makampuni haya ya nje.Poleni sana kama mmeridhika na maisha mliyo nayo.
   
Loading...