Kwa hizo tech ulizotaja Oled ni nzuri zaidi ikifuatiwa na Qled, led kisha Lcd ya kawaida Tuki assume mambo mengine yapo sawa.
TV ambayo Sony mwenyewe katengeneza panel yake hata kama ni Led itakuwa nzuri kuliko Boss ama Oiling na wa China wengine. Unaweza kuta Panel ya kampuni kubwa ni Lcd lakini I najitahidi kwenye contrast, black nzuri.
Tatizo moja siku hizi ni kwamba haya makampuni makubwa Yana outsource vifaa vyao vya bei rahisi, unakuta TV za Sony ama Samsung za bei rahisi rahisi zimetengenezwa tu huko China na kampuni nyengine zikabandikwa logo ya Samsung au Sony, kwa situation kama Hii unaweza kuta mchina Na kina Sony quality ikawa Sawa.
Hivyo ukitaka kupata ile TV quality inabidi mfuko uwe vizuri pia, kuna Tech mpya inakuja inaitwa Micro led ambayo itakuwa nzuri kushinda oled, pengine ikija Oled itashuka bei.