TV Ya JF: Paukwaaa....!!! Pakawaaa...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV Ya JF: Paukwaaa....!!! Pakawaaa...!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jun 23, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Last wiki Televisheni ya luninga ya JF, ilipata nafasi ya kumtembelea mmoja wa wanazuoni ambaye anafanya kazi Katika chuo cha Ualimu Vikindu kama Mkufunzi hapo. Siku hiyo chuo hicho kilikuwa kinafanya mahafali ya saba tangu kiwe chuo cha Ualimu japo kilijengwa mwaka 1936. Kina mazingira mazuri japo majengo yake ni chakavu sana. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Naibu katibu mkuu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  Televisheni ya Lininga ya JF inapenda kushiriki pamoja nanyi kwenye sehemu ya ujumbe uliokuwa umewasilishwa mbele ya mgeni rasmi kwa njia ya majigambo kama nilivyounakili kutoka kwenye waraka aliokuwa ameandaliwa mgeni rasmi.


  MTAMBAJI: Paukwaaaaa!!

  HADHIRA: Pakawaaaa!!

  MTAMBAJI: Paukwaaaa!!!!(kwa sauti ya juu zaidi)

  HADHIRA: Pakawaaaaaaaa!!!!

  MTAMBAJI: Hapo zamani za siku hizi kulikuwapo na nchi moja. Nchi hiyo ilibarikiwa saaaana… kwa kuwa na ardhi kubwa, nzuri na yenye rutuba. Nchi hii (akionyesha kidole ardhini)ilijengeka katika pande kuu nne ikizungukwa na mito,maziwa na bahari. Pia ilikuwa na mbuga nyingi za wanyama na Madini ya aina kwa aina. Watu wake walikuwa na vichwa vikubwa sana,lakini visivyoweza Kupambanua mambo, Pua zao zilikuwa ndefu,lakini zisizoweza kunusa harufu.Walikuwa na macho makubwa na yaliyoona sana,lakini si zaidi ya urefu wa ncha za vidole vyao. Na masikio yao yalikuwa makuubwaaa (akionyesha kwa ishara)kama tembo,lakini yasiyosikia sauti.

  Viongozi wake walikosa kiasi katika matendo yao na kuyafanya maisha ya watu wake kuwa yabisi. Nyuso zao haziku tahayari kwa aibu ya matendo yao maovu ingawa hatari yake haikuhitaji elimu ya unajimu kuibaini. Kwao swala lolote la maandalizi kwa ajili ya ustawi wa taifa kwa siku za usoni lilikuwa ni upuuzi. Waliamini kuwa hasara za wakati huo ujao hazitakuwa juu yao na kusahau kuwa watakaoishi wakati huo ujao ni watoto wa watoto wao wenyewe. Aaaah![Anatoka jukwaani]
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Pia nji hiyo watoto wao wenyewe wanawaandaa kuwa malaisi miaka ijayo,si wasomi lkn wanapachikwa usomi...hakika tutakwisha...
   
 3. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  khaaa ndiyo tansania hiyo
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na ndio watakao pata tabu.
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Heading na content tofauti kabisa..
  Anyway, wa TZ tumeshazoea kulia lia badala ya kufanya kaz kwa bidii
   
Loading...