TV gani nzuri na imara kwa ajili ya biashara ya kuonesha mpira?

Hisense na TCL au starx ndo nazionaga sana kweny vibanda umiza hata sehemu za betting na zinapiga kazi asubuhi mpaka saa sita usiku zikiwa on zaidi ya mwaka wa pili hapa kitaa nilipohama naziona.
 
TV yoyote unayoweza kutumia nyumbani hata mpira unaonyeshea...

Nikukumbushe kuwa TV sio gari useme linapita Rough Road
 
Sikiia boss chukua double glass namaanisha tv yoyote yenye vioo viwili kwajili ya usalama wa tv yako na biashara yako
 
Tv za brand za kati na chini kiubora kama
Hesense
Tlc
StarX
Boss and the co
Hizi hazipendi sana kushikwa shikwa zinataka uziweke fixed sehemu kazi iwe ni kuwasha kwa remote na kuzima

Lakini kama utakua unazihamisha hamisha kwa kuzibeba kuingiza ndani na kutoa zina wahi sana kufa screen

Mi ninayo StarX na TLC nimezifix ukutani naonyesha mpira
Zinapiga kazi vizuri sana tu

TLC ya kwanza ilikufa mapema sana sababu ya kuhamisha ndani usiku halafu asubuhi naitoa
 
Back
Top Bottom