Livino Haule
Member
- Mar 22, 2015
- 21
- 22
*LEO TV1 IMEPWAYA KATIKA KIPINDI CHAKE*
(NAIKOSOA KWA UVIVU WAKE)
Leo tarehe 12 January 2017 katika kipindi chake maarufu _*MAWAZO PEVU*_ baada ya habari mada ilikuwa ni MIAKA 53 YA MAPINDUZI NA MAENDELEO YA UCHUMI WA ZANZIBAR.
Japo mimi siyo msomi wa Habari lakini baada ya kutazama mjadala wa mada hiyo nimeona kimeandaliwa bila kufuata ladha halisi iliyotakiwa ili kupata mjadala wenye WATU HALISI wenye HABARI HALISI juu ya hali ya uchumi wa ZANZIBAR.
1. Mtangazaji au mwandaaji amekusanya maoni kwa Wakazi wa dar es Salaam katika kujadili hali ya Uchumi wa Zanzibar ktk uwepo wake miaka 53 ya Mapinduzi.
MTAZAMO WANGU: Hili ni kosa la kiufundi na ni kujiandaa kupata majibu yasiyo ya kweli na ya kubashiri au kutumia mambo ya Tanganyika kuelezea Zanzibar.
Wakazi wa Dar es Salaam wanajua nini kuhusu maendeleo ya Zanzibar? Wanajua nini juu ya hali huduma za jamii Zanzibar;
a) huduma ya maji
b) huduma ya umeme
c) hali ya elimu na mafunzo ya ufundi
d) hali ya huduma ya afya
e) huduma za usafiri na uchukuzi
f) huduma ya mawasiliano
g) hali ya kilimo, uvuvi, ufugaji, na pembejeo husika,
h) kiwango cha mfumuko wa bei Zanzibar, etc. Watu wa Dar es Salaam wanaguswaje na mambo haya?
_Are these poeple of Dar es Salaam credible sources to narrate the economic situation in Zanzibar?_
_Do they possess the truth?_
_Are they relevant interviewees to the topic?_
Kwani waandaaji hawajui kama huduma nyingi kati ya nchi hizi mbili husimamiwa na wazira tofauti, serikali tofauti, Marais tofauti, sera na bajeti tofauti?
Wakazi wa Dar es Salaam wanaguswaje na mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zao za kila siku? Chumvi, sabuni, vinywaji, vyakula, mafuta,samani, viwanja, majengo, etc. Wanawezaje kujua bei ya bidhaa au huduma mwezi Disemba na bei ya sasa Januari wakati wapo nje ya Zanzibar?
NILICHOKIONA: Wakazi wa Dar wengi waliohojiwa wamepwaya kujibu uhalisia na waliojaribu wametumia uzoefu wa hali ya Tanzania Bara na sio Zanzibar.
2. Mtangazaji amemwalika Dr. KABOGA (tazama picha) ambaye naye ameonekana kupwaya kabisa...not fully informed, not researched, ameongea kama 'Layman' anayetumia uzoefu wa story za mtaani.
Hii ni kwa sababu (naamini) yeye ni mkazi wa Tanzania Bara anayeishi mkoa Dar (kwa kazi yake ya Uhadhiri) kwahiyo mambo ya Zanzibar hayajui kabisa beyond habar za jumla ambazo hata mtu wa Kigoma (magharibi mwisho wa Tanzania) anajua.
Dr. Kaboga hajui hali ya uchumi wa Zanzibar ya sasa, hajui bei za huduma na bidhaa kwa Zanzibar ya sasa, hajui hali halisi ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar "comparativley" na hali ilivyokuwa wakati au kabla ya mapinduzi (kwa data na vielelezo/evidence).
_MJADALA WA LEO UMEPWAYA NA_ umekosewa kabisa.
NB: TV1 msiwe wavivu wa kufikiri na kufanya utafiti. Zanzibar siyo mbali mmejichimbia Dar na kurusha kipindi kilichoonekana kupoteza uhalisia na umahiri kwamba kimeandaliwa na wasomi wa Mass Media.
By Livino Ngalimitumba Haule (Lingaha)