Tuzungumzie matatizo ya figo

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,456
2,179
Figo ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mnyama na binadamu kwa kufanya kazi nyingi ikiwemo kutoa taka mwili n.k
Figo hukumbwa na matatizo mbalimbali ambazo huathiri utendaji wake kazi.
Leo ningepende tushirikishane mambo kadhaa ambayo hupelekea kiungo hiki muhimu kisifanye kaz yake ipasavyo .kwa mtu yeyote ambae alishapata tatizo hili tushirikishane na jinsi alivyokabiliana nalo .
Nianze kwa tatizo ambalo lilinikuta mm miaka miwili iliyopita nalo ni

Mawe katika figo(kidney stones)
Hili ni tatzo la figo ambapo hua inatokea inakua na vijimawe .ambavyo hupelekea maumivu makali yasio kifani kuelezea na ikiwezekana ukakojoa mpaka damu .na huwez vumilia mpaka uchomwe sindano za maumivu kwan vidonge vya maumivu mda mwingine hua havifanyi kazi.

Ni kwann nilipata hili tatzo?
-nilikua napenda sanaa kula chumvi nyingi
-nilikua nakula sanaa dagaa (hasa Shule,chuo)
-unywaji wangu wa maji ulikua kiasi
-nilikua nakunywa bia japo sio Sana
-nilikua navuja sana jasho hasa baada ya kuhamia dar(mkoa wenye joto Kali)
N.b babangu Alikua na tatzo la figo1 (sasa sijui kama ni la kirithi pia)

Jinsi nilivyokabiliana nalo
-kumwona daktari na kupigwa ultrasound (nilikutwa na mawe na maji kwenye figo (hydronephrosis)
-nilipewa dawa za kulainisha mawe
-nilianza kunywa maji mengi sanaa kusaidia kusukuma mawe yaliyokua yanashuka yakiambatana na maumivu makali mno

Hitimisho
- Afya ya figo ni muhimu sanaa na ni moja ya tatizo linalo ua watu wengi sanaa life style zetu zinachangia sanaa kwenye tatzo hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hitimisho umepona au bado unasumbuliwa mpk sasa
km umepona ulitumia dawa gani za hosptari au tiba mbadala

Na je tangu ulivyoanza kuhisi haupo sawa ilichukua muda gani mpk ukagundua kwa ultra sound kuwa una vijiwe

Pia ulikuwa unasikia maumivu pande zote mbili au moja tu

Wakati ukiwa katika hayo maumivu ni kitu gani kingne kiliathiliwa

Je kiasi cha mkojo ulikuwa unatoka kawaida au ulikuwa unatoka kwa presha ndogo lakini mrefu
Au ulikuwa unatoka kwa uchache sana (kuhuradhimisha uje)
na asubuhi mkojo wa kwanza ulikuwa unatoka kwa wingi au kwa uchache sana kujilazimisha mpk kibofu kinauma ?
 
Jitahidi ujiandae kisaikolojia ..acha
kbs urithi kwa maandishi😂😏jokes aside

QUOTE="dubwang, post: 30619927, member: 268710"]Mkuu niko mkoa wenye barid ila napenda sana chumvi yani mimi chakula lazima niongeze chumvi hata kabla sijaonja na chumvi ninayoweka mimi watu wengi wakionja huwa hawawez kula, nmeshazoea ila maji nakunywa wastani wa 2lt per day asubui had jion[/QUOTE]
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hitimisho umepona au bado unasumbuliwa mpk sasa
km umepona ulitumia dawa gani za hosptari au tiba mbadala

Na je tangu ulivyoanza kuhisi haupo sawa ilichukua muda gani mpk ukagundua kwa ultra sound kuwa una vijiwe

Pia ulikuwa unasikia maumivu pande zote mbili au moja tu

Wakati ukiwa katika hayo maumivu ni kitu gani kingne kiliathiliwa

Je kiasi cha mkojo ulikuwa unatoka kawaida au ulikuwa unatoka kwa presha ndogo lakini mrefu
Au ulikuwa unatoka kwa uchache sana (kuhuradhimisha uje)
na asubuhi mkojo wa kwanza ulikuwa unatoka kwa wingi au kwa uchache sana kujilazimisha mpk kibofu kinauma ?

Nimeuliza maswari mengi 7bu nasumbuka sana kupata mkojo sawasawa nimepima vpimo vingi. MUHIMBIRI vya figo wanadai niko sawa lkn upande mmoja unauma ila si sana maumivu yanakuja na kuacha na mkojo wangu presha ndogo sana tena Asubuhi huwa napata tabu mno kukojoa mkojo unahisi unauma lakini kibofu hakitaki kuachia

JE INAWEZA IKAWA DALILI ZA HIVYO VIJIWE ?
Pole sanaa tatizo lilipona .
-mkojo ulikua unatoka kidogo kidogo
-maumivu yalikua upande mmoja wa figo
-maumivu mwanzo yanakuja na kukata badaye yanakaza
-nilikua nakojoa mpaka damu yakichanganya
-kuhusu mawe inabd upate radiologist mzuri mwenye uwezo wa kusoma vizur picha za ultrasound (sio wote wanaweza nilienda zaida ya hospital 3 kuhakikisha jibu )
- chumvi punguza mm nilikua nakula sanaa pia
-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dalili za ugonjwa wa figo ni zipi mkuu?
na vipi sisi tunaotumia vinywaji vyenye spirit hatuwezi pata hiyo shida kweli?
 
Watu wengi huepuka usumbufu wa kuamka usiku lakini saa bora kabisa ya kunywa maji ni kupata glass kabla hujaingia kitandani. Wakati mwili ume pumzika maji haya yata kusaidia kuweka sawa mapigo ya moyo na usafirishaji wa damu.

Utaamka ukojoe na wanaofanya hivi hupata choo kikubwa mara tu wanapoamka asubuhi.

1551666092161.jpeg
 
View attachment 1037338
Mhhhh Choo kikubwaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa wa figo kama kisukari na cancer kwa asilimia kubwa yanakua triggered na lifestyle and eating habits.
 
Back
Top Bottom