Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,460
Wengi wetu humu tuna watoto na si ajabu wengi ni young parents kama sie.
Hebu leo tuzungumzie mapenzi kwa watoto wetu, wengi tunawapenda watoto wetu sana na kila mmoja anatamani mtoto wake awe ni mwenye mafanikio siku za mbeleni.
Jamaa yangu wiki hii alipokea ugeni wa mama yake mzazi ambaye ni bibi wa watoto wake (anakaa mkoa mwingine) na ndiyo ilikuwa ni first time kufika kwake, kikubwa alifurahia maisha ya pale lakini alitoa ujumbe kuwa mwanae hawapendi wajukuu zake!!! Kumuuliza kwa nini akajibu hawajui kupika kwa kutumia kuni au mkaa .!! Namnukuu Huyu wa kike ataolewa na nani kama hajui kupika kwa kuni au mkaa afadhali hata huyo wa kiume, au unadhani ataolewa na matajiri kama wewe??
Ukweli nikwamba jamaa ana deep-fryer, rice cooker, pressure cooker na jiko la gesi lenye oven. Hapo hakuna sababu ya kutumia mkaa au kuni na huo ndiyo ukweli halisi na mbaya zaidi tangu watoto hao wamezaliwa wanajua mapishi kupitia vifaa hivyo tuu.
Je, katika malezi ya kileo kuna ulazima wa watoto kujua matumizi ya kuni na mkaa kama ziada na advantage ya maisha yao ya ndoa/kimapenzi siku za mbeleni???