Tuzungumzie kuhusu ulezi...

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,713
Habari zenu marafiki,
Leo ningependelea tuzungumzie kuhusu ulezi wa watoto wetu,taifa lijalo na majukumu yetu kama wazazi.Mzazi ni mfano wa kuigwa kwa mtoto.Kile anachofanya mzazi kiwe kizuri au kibaya ndicho mtoto anaona ni mfano maridhawa kwake.Tulio wengi tunawadharau watoto,kwamba wana uelewa mdogo,lakini si kweli watoto wanauelewa wa hali ya juu na wanakumbukumbu maridhawa.Watoto walio wengi wapo very manipulative.Katika umri mdogo kabisa atajaribu kukufanyia kila visa kukujaribu na kukupima.Lakini wewe kama mzazi unatakiwa uwe na msimamo juu ya maamuzi yako na kanuni unazomuwekea.Na anakujaribu wewe kama mzazi kwasababu wewe ndio mtu alokuzoea na anaekuamini kuliko wote.Na ndio maana mtoto huyohuyo ambae anakufanyia vituko wewe akiwa na wengine anakuwa na adabu na hekima ya hali ya juu.Jinsi mtoto unavyomlea ndivyo jinsi anavyokuwa,tuwalee watoto katika misingi bora kwa manufaa yao ya baadae,wakati huohuo tusiwanyime haki zao za kuwa watoto.
Nafurahishwa sana na uhalisia/ukweli(honesty) na innocence ya watoto,their curiosty to learn and discover new things,its amazing.
Inanishangaza na kunisikitisha mno ninaposikia mzazi anamuadhibu au kumchapa mtoto wa miaka 3 au 5?Haswa kwa makosa ambayo ukifikiria ni wewe mzazi wa kujilaumu na kujihukumu.Kama una stress zako za maisha tafadhali tafuta suluhu ya kuzimaliza bila kuhusisha watoto.Hivi nyinyi wenzangu mnalichukuliaje suala hili?mnaona ni sahihi mtoto mwenye umri huo kuadhibiwa kwa viboko?na wewe kama mzazi mtoto wako wa miaka 5 akileta utovu wa adabu unachukulia hatua gani?utampa adhabu gani?Utamkanya?
Karibuni wapendwa tujadili suala hili!
 
Kwahiyo conclusin ni nini?tuchape au tusiwachape?

Maana wengine ukiwatandika mpaka wanazoea wanakuwa sugu!

Wengine bila kuwachapa hawajifunzi
 
Watoto wa siku hizi very manipulative
 
Kwahiyo conclusin ni nini?tuchape au tusiwachape?

Maana wengine ukiwatandika mpaka wanazoea wanakuwa sugu!

Wengine bila kuwachapa hawajifunzi
kwa mtazamo wangu si sahihi kwa mtoto kuchapwa.kuchapa kunajenga uoga from personal experience!mtoto akikosea apewe adhabu kutokana na ukubwa wa kosa na umri.mfano kumnyima kitu anachokihitaji au anachokipenda kama toy au kumnyima uhuru wa kufanya yale mambo anayoyapenda!na wakati huohuo umsomee risala ili ajue makosa yake!
 
Kwa mtazamo wangu kiboko siyo suluhisho.....watoto wetu wana njia nyingi za kujifunza na.kuenenda katika haya maisha.....wanajifubza kwa njia ya uzoeshi na kuiga toka kwa jamii inayowazunguka...cha kufanya ni kuhakikisha kwamba maisha yetu yanakwebda katiknamna ambayo wataiga na kutenda mambo mema....kisaikolojia unapomwadhibu mtoto hususan mdogo kama huyo unamjengea nidhamu ya woga na hakuna atakalofanya ambalo litakuwa real bali kuhofia tourture anayoweza kuipata baada ya kukengeuka...madhara yake ni kwamba mtoto anafikia mahali anwaza ndani ya boksi na ukimtoa nje ya mazingira yabayomzunguka inakuwa tabu kwake kucope na mazingira yale..uwezo wake kiakili unafungwa na kuwa limited..tusiwachape watoto.....tutumie mbinu mvadala ya kuwaelekeza kwaupole...wana akili kiasi cha kuweza kibadilika haraka bila kutumia nguvu kubwa....ISIPOKUWA KAMA MTOTO HUYO ATAKUWA AMESHINDIKANA KWA KUTUMIA NJIA YA AWALI UNAWEZA KUTUMIA ADHABU HIZO
 
Nashukuru mno kaka yaani kakwangu ni 8month hakasikiii natamani nikapige naishia kukafokea kako so curious kanataka kushika kila kitu nashindwa kuelewa nitadeal nae vipi na kila an achoona an a imitate. He is my firstborn sitaki aje kua mtoto mtundu I started feeling guilty akipanda vitu na kuanguka I feel irresponsible sometimes. Kiukweli kuzaa si kazi!Lakini bila kiboko kweli tutaweza? Na nchi za watu hizi ndo tutaitiwa polisi.
 

Kwahio unakubali kiboko kama njia ya kuadhibu?what if kama ni mgonjwa mfano mtoto mwenye ADHD yupo hyperactive!
Kawaida mtoto ukimfokea mara kwa mara anazoea na kuona kawaida,na ndio maana tunatakiwa tuziwagombeze watoto saa zote ili ile siku akigombezwa ajue leo pameharibika na kama ni mtoto mwenye nidhamu atajirudi baadae ukimsema na kuomba samahani!
 
Kweli kabisa mzazi ni kioo kwa mtoto. Mtoto kuchapwa si sahihi kabisa, mara nyingi wazazi hawana busara kwa kosa analofanya mtoto, mtoto afanyapo kosa kwake inakua si kosa bali ni kutokuelewa kua anafanya kosa, akili ya mtoto inakua haina kitu kwa umri wake, utakachomfundisha ni rahisi kwake kutii....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…