Tuzungumze kidogo 🤒

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,176
Reaction score
900
Je, wanaume waoaji wenye malengo ya kuanzisha familia wameisha? Je, soko la wanaume wasiochezea wanawake na kuwazalisha limekuwa gumu? Nachelea kuamini waoaji wameisha. Ingawa hakuna anayelazika kuoa, na watu wana sababu mbalimbali za kuamua kutokuoa, bado wanaume wenye malengo ya kuanzisha familia wapo na unakutana nao. “Shida ni nini?” unauliza swali zuri.

Kwanza, viashiria vyote vinaleta taharuki kuwa huenda ‘wewe’ wa hapo kibaruani, supermarket na coffee shop huenda sio mtu halisi. Sura uliyonayo ukiwa baa, huenda sio sura unayoamka nayo asubuhi. Hili linatia mawazo sana. Wanaume waoaji wanakua kama hawana uhakika huyo ‘wewe’ waliyevutiwa nae hapo coffee shop na picha wanazoona mitandaoni ndio ‘wewe’ huyo huyo vipodozi vikiisha? Je, kamera ikikosa ubora utabaki na urembo huo huo? Sio kwa ubaya lakini sura yako halisi haifahamiki.

Kingine kinachotia mashaka zaidi ni urahisi wako. Hujui kumzungusha mtu aone unahitaji muda kufikiria ombi. Unasema wanaume wenyewe hawa wahuni siku hizi. Ukijivuta vuta harudii tena. Hata wahuni kuna saa nao wanapenda kusikia uko bize kidogo na jambo fulani na kuonana na wewe ni mipango. Mwenzetu siku hiyo hiyo tayari unatandika hadi kitanda na unaosha kabisa mabakuli kwa mwanaume kwa nini asiogope?

Lakini kibaya kingine ni kukosa kwako kiasi. Kijana kakuita mzungumze mfahamiane kidogo kabla hajaamua kutoa ratiba ya hatua ya pili. Unakula utafikiri ulikuwa kwenye mfungo wa kukuombea taifa zima? Halafu hushibi. Unaomba hadi ufungiwe ukamalizie nyumbani. Kijana wako anapata mawazo, hii njaa ya pizza, firigisi na vifumbatio vya kuku muda wote ataiweza? Siku hiyo ndio una dharura ya laki mbili ya karibu, huna bando la kujibu maswali yake. Kweli unaona mtatoboa? Tunapenda maisha ya gharama lakini kiasi ni muhimu.

Usinielewe vibaya. Sio kwamba watu wanaingilia maisha yako lakini kuna vitu vinatisha na hatujazoea kuviona. Saa nane usiku mtoto wa kike uko mitaani na wala huonekani kuwa na haraka ukapumzike. Kweli? Haya unasema huwa hulewi lakini kweli ndio umalize bia kumi na hupepesuki? Huoni unamtisha kijana wa watu? Inaogopesha ati. Huyu mtu anayegida mvinyo mkali hivi kuna mahali tutaenda au abaki kuwa chombo cha burudani? Ujue hata walevi wanaogopa walevi. Wanaume waoaji wapo wewe ndio unajiamulia mambo. Samahani sana kwa kukuambia ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…