Bakari Chijumba
Member
- Mar 22, 2019
- 46
- 55
Na Bakari Chijumba,Mtwara.
Afisa habari wa mkoa wa Mtwara, Evaristy Masuha amepongeza uongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara (MTPC),kwa kutoa tuzo kwa wanahabari wanne mkoani humo kwa mchango wao katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Tuzo hizo zimetolewa mjini Mtwara juzi tarehe 3 Mei 2019, katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani (World Press Freedom Day) ambayo kitaifa yalifanyika Mjini Dodoma.
Waandishi waliopewa tuzo hizo ni Bakari Chijumba(Beca Love) kupitia uwakilishi wake wa habari mitandaoni(Blogs mbalimbali,Onlive Tv, Forums nk), Haika Kimaro wa gazeti la Mwananchi, Juma Mohammed wa Clouds TV na Karim Faida wa Jamii Radio mkoani Mtwara.
Afisa habari huyo amesema kwa kuzingatia kigezo cha uandishi unaoleta manadiliko chanya katika jamii waandaji wa tuzo hizo hawakukosea.
Ametolea mfano wa habari iliyoibuliwa na mwandishi wa Mwananchi ya shule ya Chikotwa yenye darasa moja na mwalimu mmoja katika wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
“Kwa ujumla kigezo hiki mlikitendea haki. Mfano mmoja utakaowakilisha washindi wote ni uandishi wa Haika. Huyu ametufungua wengi, amefungua milango ya fursa ya maendeleo kwa mkoa huu. Mfano mzuri ni makala zake nyingi ikiwemo ile shule yenye mwalimu mmoja pale Nanyumbu.Dunia iliweza kulifahamu hilo. Hivi sasa fursa ya mabadiliko ya shile hiyo iko wazi,”amesema Masuha
Mwingine ni huyu aitwae Becalove(Bakari Chijumba),kabla sijamfahamu,
Mara nyingi nilikuwa nikijiuliza huyu kijana ni nani!?.. Kuna kipindi nilijua ni wewe(Katibu Mtwara Press) kutokana na jinsi ulivyo active kushare taarifa zake ambazo ziko very interested na zinazogusa kila sekta..Tuzo hizi Kwa ujumla niwapongeze kwa kutenda haki, Mungu aendelee Kuwaongoza,”amesema Masuha
Katibu wa Mtwara press club, Bryson Mshana amesema kwa mwaka wa pili mfululizo wametumia maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari kutambua mchango wa wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari, ambao kwa mwaka 2018 waliandika habari ambazo ziliibua uwajibikaji kutoka kwa wahusika na kuleta mabadiliko makubwa.
Amesema Tuzo hizo zinalenga kuwaimarisha zaidi katika kazi wanayofanya na kuchochea wanahabari wengine kujituma kwa bidii.