Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Ni jambo la kawaida kuona magari ya taka yakiwa yameharibika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Moshi na hata Arusha. Magari hayo yanapoharibika hukaa kwenye eneo yalipoharibikia kwa siku kadhaa kabla hajatolewa. Cha kushangaza zaidi ni kwamba yanakuwa yana uchafu/taka ambazo wakati likiwa hapo lilipoharibikia uchafu huo huendelea kuoza na kutoa harufu mbaya.
Kwanza hali ya magari hayo ni mbaya kiasi yanakatisha tamaa. Mimi binafsi huwa nashindwa niyaite magari ya taka au yenyewe ni aina ya taka au uchafu. Na baada ya kufanya uchunguzi na kusikiliza kipindi za Mazingira kinachorushwa na Radio One nimegundua kwamba wakati wa kuomba tenda watafuta tenda hupeleka magari mazuri na hata mapya. Baada ya kupata tenda magari yalioonyeshwa wakati wa tenda hayaonekani na hayajulikani yanapopelekwa.
Kuna haja ya serikali kuu, serikali za mitaa kuwa na utaratibu wa kufuatilia magari ya kubebe taka na kuhakikisha checkup zinafanyika kila baada ya muda fulani. Ila mtoa huduma ya taka akilegalega achakuliwe sheria kulingana na taratibu za tenda.