Tuwe wazalendo na tuziheshimu tunu za taifa

LUCAS KISIMIR

Member
Sep 11, 2012
29
4
KIPEPERUSHI.jpg KIPEPERUSHI.jpg
SURA YA KWANZA
Tanzaniani nchi yetu sote tuliozaliwa humu (wazawa) pamoja na waliojiandikisha kuwaraia. Sisi sote kwa mchanganuo huo tunalo jukumu la kuiendeleza na kuilindanchi yetu kupitia uzalendo uliotukuka na wenye kujipambanua wazi wazi kila wakati,hususan kwenye masuala ya mustakabali na ustawi wa nchi yetu.

Masuala yamustakabali wa nchi na ustawi fanisi wa watu wake hutawaliwa na mfumo ambaosehemu zake ndizo TUNU za taifa husika. Tunu za taifa ni masuala ya msingiambayo hulitambulisha taifa na utaifa wa watu wake, nayo yakipungua,yakikorofishwa, yakitiwa dosari na ama kukosekana, nchi huingia matatani.

Kwaumuhimu wake huo, siasa potofu hazipewi mwanya wala fursa ya kuvuruga tunu zanchi husika hata kama ikiwa ni kwa jina la demokrasia. Viongozi wa juu katikautawala wa nchi, ndio wasimamizi na walinzi wakuu wa tunu za nchi yao.Mwananchi akizitambua, kuziheshimu na kuwajibika ipasavyo katika kulinda tunuza nchi yake, huingia katika daraja la uzalendo. Mzalendo ni mwananchi-mwajibikajikatika masuala ya mustakabaki wa nchi yake.

Sote tunawajibika kuzifahamu TUNUza taifa letu kwa ukamilifu. Tunapaswa kuzijifunza, kuzikariri, kuziheshimu,kuzilinda na kuzirithisha kwa vizazi vyote vya jamii yetu ili tunu hizo zipatekuwa historia inayoishi.
Kamailivyokuwa katika kipindi cha uhuru na kipindi cha Azimio la Arusha hadi palelilipokuja lile la Zanzibar, Tunu za Taifa zilijulikana kwa wote nazo zilikuwazikitamkwa bayana na kwa sauti ya juu sana.

Kwa bahati mbaya hatukuendelezautamaduni huo na kueneza kwa juhudi za wazi elimu inayomfunulia kila mmoja wetukuweza kupambanua ikiwa suala fulani ni tunu ya taifa au la. Katika kipindinilichokitaja, hakukuweko na misamiati mingi isiyotamkika kama hii mipyatuliyonayo leo inayotufundisha kuitana kwa majina yasiyoitikika.

Katika zamahizi, kama matokeo ya mwenendo mpya uliotuzukia, wengi wetu kwa nadra, hujikutatukichakura huku na kule tukisaidiwa na masalia ya historia katika fikara zetu,kujaribu kutafuta, kudadisi, kubuni na kujenga uelewa mpya katika kuchambua nakupambanua masuala yaliyo tunu, kati ya yale yasiyohitimisha vigezo vya sasavya kuwa tunu ya taifa letu.

Elimu ya kutufumbua juu ya hili imeachwaikining'inia ili kila mwenye chembechembe ya uzalendo fikarani mwake na yulemwenye kujitolea kutumia muda wake kujishughulisha nayo, huchupa na kuchuma uelewakwa kadri ya majaliwa yake.
Kiladola yaani mamlaka na utawala katika kipande cha ardhi juu ya uso wa dunia kinachojipambanuakwa alama za mipaka yake na kwa kujumuisha watu wake, rasilimali zinazopatikanahumo, siasa ya utawala na uongozi, lugha, tamaduni, nembo, bendera, fedha naKatiba hujitambulisha kwa umma wake na ulimwenguni kupitia TUNU zake.

Kilammoja miongoni mwetu anao ufahamu kwa viwango vinavyopishana kuhusu ukwelihalisi juu ya TUNU za Taifa letu. Hata hivyo, tunu ni masuala ya pamoja yawananchi katika nchi yao ambayo kimsingi hutajwa vile vile kwenye katiba yao nakutekelezwa kwa ufanisi, uaminifu na usimamizi thabiti kama msingi wa maishayao na sheria yao kuu.

Tunu hugusana moja kwa moja na maisha ya watu katikanchi yao na kwa ujumla hutawala mfumo wa maisha yao. Watu na tunu zao ni kamavipingili vinavyounda mnyororo-kila kimoja huingia ndani ya kingine na nje yautaratibu huo hakuna myororo wa kipingili kimoja. Nionavyo mimi, baada yakutafiti na kuchambua kusikohimiliwa na vigezo na masharti, najikuta katikamaelezo yafuatayo Kuhusu TUNU za Taifa letu.
Baadhiya tunu ninazofahamu mimi ni hizi zifuatazo;-


  1. Kiswahili kama kiunganishio thabiti cha jamii zote kinachovuka mipaka dhidi ya ukabila,
  2. Haki za kibinadamu na usawa wa kijinsia,
  3. Amani, utulivu, kuheshimiana na kuvumiliana,
  4. Umoja wa kitaifa,
  5. Wimbo wa Taifa na Bendera ya Taifa,
  6. Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar,
  7. Usawa, wajibu, kutambua na kuheshimu utu,
  8. Uchaguzi wa viongozi kwa misingi ya kidemokrasia,
  9. Utawala bora, utii wa sheria na ulinzi wa mipaka yetu iliyo urithi wetu wa sasa na vizazi vijavyo,
  10. Mfumo bora na sahihi katika usimamizi na mgawanyo wa rasilimali za taifa ili kunufaisha umma kama kipaumbele muhimu,
  11. Haki ya kila raia kumiliki na kuendesha uchumi,
  12. Ushiriki sawa wa watu katika majadiliano, mipango na utekelezaji wa masuala ya umma,
  13. Kujitegemea kama msingi wa maendeleo ya watu,
  14. Azimio la Arusha nalo lilikuwa tunu muhimu mno.

Pamojana tunu zingine unazozijua weye na pengine sahihi zaidi kuliko hizi nilizotaja,nchi yetu imebarikiwa kufikia hapa ilipo kwa kuwa tunu hizo zilienziwa kwamujibu wa tawala za awamu nne tangu kipindi cha mapambano ya kupigania uhuruwetu.
Kitendochochote cha kuhatarisha na kuziharibu tunu hizi ni kuitikisa nchi kunakoitianyufa za kimustakabali. Kwa leo naishi hapa.

KARIBU TUJADILIANE

SURA YA PILI
Safariyangu ya kujadili TUNU za Taifa ndiyo kwanza inaanza kupamba moto. Safari yanguhii, ina lengo la kuhitimu kwenye kuwianisha mtazamo wa kizazi cha leo nauhusika wa kimustakabali kwa taifa letu kwa kipimo kinachoainisha kiwangohalisi cha sasa cha heshima yetu kwa Tunu za Taifa letu.

Kama nilivyosimuliakatika sura iliyotangulia, tunu za taifa ndizo uendelevu wa taifa na Viongoziwa juu wa Taifa letu ndio waliokabidhiwa jukumu la kuzilinda kwa gharama yoyotena kuzihuisha kila wakati ili kuzitilia uhai mpya kwa kadri ya maisha ya kizazichao na awamu yao. Jukumu hili ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanapomaliza vipindivyao vya utawala wanajitathmini kwa utashi wao wenyewe ni kwa kiasi gani tunuzimeimarika na ama kuteketea.

Wanapong'atuka na kukabidhi uongozi na utawala kwenyeawamu nyingine, licha tu ya kukabidhi ofisi, wanatakiwa kujipima ni kiasi gani jamiiyao inazielewa, inazikubali, inazithamini, inazitii na kuzienzi tunu za taifa lao?Huku ndiko kuwa waaminifu wa kweli kwa taifa lao na wazalendo wenye mfano borawa kuigwa. Hii ndiyo siri kuu ya nguvu ya Taifa la Wamarekani kwa zaidi yamiaka 200 ya kujitawala kwao na kuitawala dunia.


Tunuza taifa letu ziliazishwa wakati tulipopata uhuru kwa kutambua na kuthaminimifumo ya kijamii na kiuchumi, nazo zimeendelea kutulea kwa pamoja kama taifamoja katika nchi moja bila wanajamii kuona umuhimu wa kutambuana kwa mujibu wa makabilayetu na wala dini zetu.

Marehemu Baba wa Taifa, Rais wa Awamu ya Kwanzaalipong'atuka madarakani alimwachia Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi jamii yenyekiwango kikubwa cha utii kwa Tunu za Taifa lao baada ya miaka 23 yakuzitumikia, kuzisimamia na kuziimarisha tunu hizo.

Rais wa awamu ya Pilialimkabidhi Mheshimiwa Benjamini Wiliam Mkapa jamii yenye kiwango fulani chautii kwa Tunu za Taifa. Rais wa Awamu ya Tatu naye alimkabidhi Mheshimiwa, Dr.Jakaya Kikwete jamii yenye kiwango fulani cha utii kwa tunu za taifa. Hapandipo tulipo sasa, kipindi chetu, awamu yetu na kizazi chetu.


Nia yangu ni kugonga kengele kwa sauti inayoonya na kuwatazamisha WaTanzaniawenzangu juu ya umuhimu wa kuziheshimu Tunu za Taifa letu kwani ndizozinazotufanya kuwa wamoja na salama. Ikiwa Baba wa Taifa alimkabidhi RaisMstaafu Ali Hassan Mwinyi pipa (pekee) liliojaa heshima ya jamii kwa Tunu zaTaifa, jambo la kujiuliza hapa nalo lijibiwe kwa uaminifu mkubwa ni hili; Je, baadaya Mwinyi kulipokea pipa hilo na kukaa nalo, alipolikabidhi kwa Rais MstaafuMkapa na baadaye kukabidhiwa kwa Rais Kikwete, pipa lingali limejaa pomoni?

Sio hoja yangu tuulizane ni kipindi gani au awamu ipi hasa ilihusika nakupungua sana kwa kiwango cha ujazo katika pipa. La hasha! Hoja yangu nikujiuliza ikiwa kama, kwanza, tunatambua kwamba pipa limepungua na hoja ya pilini kwa kiwango gani na kuainisha sababu za kupungua huko. Suala jingine lakujiuliza ni kwamba, kwa kupungua huko kwa pipa letu la kipekee, ni sehemu ganiya jamii yetu kimaumbile inaathirika zaidi na hivyo kujikuta kuwa wahanga wakimatokeo?

KARIBU TUJADILIANE…………..

SURAYA TATU

Tuliachiamajadiliano yetu pale kwenye kituo cha pipa tukiulizana ikiwa bado lingalilimejaa pomoni au vipi? Tulilichungulia na tukauona ukweli wa hali halisi ukiashiriana kutuelekeza kwamba pipa limepungua sana. Hatujui kama limepungua kwakuchotwa ama kwa kuvuja!

Ukweli unabaki pale kwamba pipa limepungua! Ikiwa kamalimepungua kwa kuchotwa, yawezekana likawepo tumaini kwamba tutauthibiti uvamiziwa hali ya kuchotwa kwa kulilinda sisi sote kama jukumu la msingilisiloturuhusu kuzembea na wala kuchoka. Walakini, ikiwa kama limevuja lenyewe kwenyekitako, itakuwa vigumu sana kuthibiti uvujaji huo kwani katika mchakato itatubidikwanza tumimine kilichopo humo ili kuligeuza pipa juu-chini, chini-juu ndipotulizibe!

Hili la pili ni tukio la gharama kubwa kwa kuwa maisha hayasimami kwahoja ya mpito. Ikiwa mazingira yanatulazimu hivyo, tutawajibika kuthibiti mpitosanjari na kule kuvuja kwa wakati mmoja, jambo ambalo ni gumu na hutatiza. Katikakuliziba, yamkini tutakuwa tunalibahatisha tundu na kama twalijua lilipo, tutakinzanana kupambana sana na uchakavu wa kitako kwa mnasaba na ubora wa awali katika kuundwakwake, na kwa sasa, idadi ya matundu tutakayoshughulika nayo.

Hii ni kazi ngumuisiyo na mbadala bali uchacharikaji shirikishi na wakati wenyewe ni huu.
Jambolikeralo lisiposemwa huku lingalipo, huvia na kutoweka kimantiki na katikahili, kutoweka ni kwa milele katika mantiki na nadharia tu na sio katikauhalisia wa uwepo wake. Jambo hilo huwa limetoweka katika orodha ya masuala ya kushughulikiwaingawa lenyewe lingaliko likiendelea kuathiri bila waathirika kwa chanya na hasi kujihusisha nalo.

Jambo muhimu linapotoweka, kulirejesha huhitaji mchakato wa kuvizia usiopitia njia namisingi ya awali. Kwa mantiki hiyo, ubunifu mwingi huhitajika katikakufanikisha urejeshwaji huo. Tunu za taifa bado zingaliko ila hazizungumzwikatika kuzihuisha na kuzifanya sehemu ya maisha ya watu. Tunu za Taifa ni ngumukuzifuata na kuzitekeleza katika utafutaji wenye matokeo ya ufanisi wakustukiza, kwani zenyewe bila ulegevu wa kimaudhui, husimamia na kuimarishauzalendo, maadili na kusimamia kanuni na sheria kwa mkazo usiopenyeka.

Tunu zingine tumezitoweshwa kwa mtindo wa kuvuja polepole kupisha utaratibu na mbinumpya ya unufaikaji haraka wa ubinafsi. Hili limefanikiwa kwa mtindo wakinyonga! Kinyonga hutembea taratibu, mbele mbili, nyuma moja ili asigundulikekwamba anasonga mbele! Chembe na chembe,mkate huwa.
Somahadithi fupi ifuatayo; Jaribio la siku ya kwanza, mtoto alichovya kidole kwenyekopo la sukari, mama hakusema kitu. Katika zoezi la marudio, alichota kidogo nakuitia mfukoni mwake ili ailambe akiwa shuleni, lakini pia, mama hakusemalolote.

Tukio jingine lililofuatia ni mtoto huyo kulichukua kopo la sukari nakwenda nalo chumbani mwake akasherehekee ulambaji wa sukari iliyotapakaakitandani mwake mwote kwa raha zake zilizothibitiwa na usingizi uliotokana nauchovu wa shughuli za kitoto. Asubuhi na mapema mama hakuliona kopo jikoni naakamtuma mtoto mwingine kwenda dukani kununua sukari iliyoletwa katika Mfuko waRambo, naye, alipika chai iliyonywewa pia na Mlamba-Sukari.

Asubuhi hiyo watoto walikwenda shuleni naye mama kaamua kufanya shughuli za usafi wa nyumba zilizomwezeshakuligundua kopo la sukari katika chumba cha mhusika na kulirudisha mahala pake.Mlamba-sukari aliporudi jioni, mama akazungumza naye kwa lugha nyepesi akimulizasababu za kuliweka kopo chumbani mwake na wala hakuhoji uhalifu wa kuila sukariiliyokuwemo koponi.

Hakukuwa na jibu kwa swali hilo bali ahadi ya mama kwambasiku nyinginewe, atamshtakia mhusika kwa baba yake.
Sikumoja mtoto huyo asubuhi na mapema aliingia chumbani kwa baba na mama na kutwaashilling elfu mbili zilizokuwepo mezani na kukimbia nazo shuleni ambako alirudijioni. Mama aligundua kutoweka kwa shilingi elfu mbili.

Baba hakushughulishwana suala la kutoweka kwa shilingi elfu mbili kwa fikra kwamba mama alizitumia.Mama hakumwarifu baba kuhusu kutoweka kwa fedha hiyo ingawa alifahamu ya kwambazilikuwepo mezani mara baada ya baba kuondoka kwenda kazini kwake. Utundu huombaya wa kijana uliendelea kukomaa na siku moja alitoweka na gurudumu labaiskeli ya baba yake na kwenda kuliuza.

Tukio hili lilimkereketa sana baba huyona hivyo akaamua kumwuliza mkewe lilipo gurudumu hilo. Alipata majibu yakiutetezi kwamba pengine hakulileta gurudumu hilo kutoka kwa fundi ambako alilipelekakwa marekebisho. Huu ulikuwa uongo, kwa kuwa mama alifahamu fika kwambagurudumu lilikuwepo mle nyumbani likisubiri nafasi ya baba kulifunga katika baiskeli.

Huo ulikuwa utetezi tu wa mwanaye huku akijua ukweli halisi. Siku zilisongambele katika matukio ya aina aina na siku moja kijana akamletea mama yake gaunialilokwapua gulioni. Mama alilipokea gauni hilo kwa furaha na shukrani bilakuuliza zilikopatikana fedha za kulinunua gauni ambalo halikuzingati kimo chamama yule. Kwa kijana, hiyo ilikuwa funga kinywa ili apate kuendeleza majaliwa yakeharamu kwa ulaini na utetezi.

Kuku walianza kupungua bandani bila manyoyakuonekana. Vitu vya kigeni vikaanza kuongezeka chumbani kwa kijana mtundu, hukumama mfagia vyumba akiwa hajihusishi katika kujua asili ya upatikanaji wa vituhivyo kwa kuwa hakuijua vile vile kazi ya mwanaye.

Baba ndio kabisa, hana habarikuhusu yanayojiri kati ya mama na mwanaye. Mwisho wa hadithi hii ni pale ambapowazazi hao walipewa habari ya kijana wao kuweza kutambulika kwa mabaki ya sehemuza mwili zilizosalia baada ya kuunguzwa moto uliokolezwa kwa gurudumu chakavu lagari.

Haya ni matokeo ya kunyamazia mambo kwa kuyaona madogo, kunakohimiliwa piana mahusiano yatiayo kiza na kigugumizi katika kuyakemea! Kijana huyoaliyaharibu maisha yake pamoja na matumaini ya wazazi wake. Katika suala laTunu za Taifa, baba, mama na mtoto mtundu ndilo lifaalo kuchambuliwa nakujadiliwa kwa kina
na uaminifu ili kukwepa matokeo hasi. TUJADILIANE………….. KIPEPERUSHI.jpg KIPEPERUSHI.jpg
 
Back
Top Bottom